Vipaumbele 10 vya Wizara ya Afya kupitia Bajeti ya Tsh. Trilioni 1.3

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
  1. iKuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa;
  2. Kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa na vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Taifa;
  3. Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini;
  4. Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga;
  5. Kuimarisha upatikanaji na uendelezaji wa wataalam katika Sekta ya Afya kwa fani za kati, ubingwa na ubingwa bobezi;
  6. Kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi nchini;
  7. Kuendeleza na kusimamia afua za Tiba Asili na Tiba Mbadala;
  8. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na magonjwa ya mlipuko;
  9. Kuimarisha huduma za afya ya akili, huduma za utengamao hususan kwa watoto, wazee na watu wenye ulemavu;
  10. Kusimamia Tafiti na matumizi ya matokeo ya tafiti mbalimbali za afya

============














 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…