Unatumia mafuta gani ya kujipaka? Mimi niliteseka sana na vipele kama hivyo nikiwa chuo vilikuwa vinanitokea mikononi vinapotea baada ya muda vinarudi tena...nilitumia dawa nyingi bila kuona matokeo mwisho nikasema basi ni maumbile yangu, sikujua tatizo ni nini. Kipindi hicho nilikuwa najipaka cocoa butter, nilikuwa nayapenda sana hayo mafuta. Nilipoanza kazi sikuwa natumia tena hayo mafuta na sikuwa napata vipele, ila mwaka juzi nikayakumbuka mafuta yangu nikayanunua kutumia mara moja tu kesho yake vipele hivyo vimerudi ndio nikagundua nina allege nayo japo ni mafuta mazuri sana. Ilibidi nifanye research ndio nikagundua kuna watu huwa wana allergy na cocoa butter na mimi ni mmoja wapo. Jaribu kuacha mafuta unayotumia kwanza uone kama vipele vitapotea.[/QUOTEnikweli naamini kabisa kwasababu nilikua natumia vaciline nimeacha wiki iliyopita baada ya kupata ushauli kwa watu sahisi naona haviwashi vinazid kupotea