1) Wabunge 20 wataalamu waongezwe
Tofauti na wabunge wa majimbo.
- Hawa watakuwepo bungeni kuwakilisha taaluma au fani mojawapo muhimu katika maisha ya watanzania. Mifano ya fani hizo ni Elimu, Kilimo, Biashara, Uvuvi, Afya, mazingira, uwekezaji, utalii, michezo nk.
- Hawa hawatalipwa mshahara kama wabunge, bali watapewa malipo ya kuhudhuria vikao vya bunge siku za fani husika. Baada ya hapo, watarudi kuendelea na majukumu yao ya kila siku kwa waajiri wao ambako wanapokea mishahara yao.
Namna ya kuwapata wabunge wataalamu.
- Utengenezwe utaratibu mzuri ili wachaguliwe na raia wanaotambua sekta/ fani hizo. Nashauri kura zipigwe mtandaoni kupitia intaneti. Wapiga kura wajiandikishe mtandaoni na kuhakikiwa kabla ya siku za uchaguzi. Uchaguzi ufanyike zaidi ya siku 3 ili kutoa fursa kwa wapiga kura mtandaoni. Pia Tuangalie kama tunaweza kuruhusu wapiga kura wenye vigezo kutoka nje ya nchi ✍️
- Wagombea waandike mtandaoni kwa nini wanataka nafasi hizo. pia waelezee sifa zao na uzoefu wao katika sekta husika. Moja ya vigezo vya kuzingatia kwa wapiga kura ni angalau Elimu ya stashahada. Namba za chuo zitumike kuhakiki wapiga kura.
- Mpiga kura awe na uwezo wa kutumia mtandao wa intaneti maana kura zitapigwa kwa njia hiyo.
Faida za wabunge hawa
-Wanauzoefu wa kutosha wa kitaalamu katika sekta husika, mawazo yao yataleta tija kwa taifa. Watasaidia sana kuishauri serikali katika mipango ya muda mrefu.
-Kwasababu hawatalipwa mshahara wa bunge, itasaidia sana kupata watu wazalendo na wenye nia ya dhati kulisaidia taifa hili. Na uhakika wataalamu wengi tayari wana kipato chao cha kujikimu na hawataigeuza nafasi hiyo kama ajira bali kusaidia maendeleo ya taifa hili.
-Kuna wataalamu wanaotamani kupata fursa ya kuongea bungeni, ila hawana fursa kwa sababu ya namna ubunge unavyopatikana. Wengi si wazuri kwenda majukwaani kuomba kura na kufuatilia mambo yote ya watu wa jimbo fulani. Wengine si wafuasi sana wa vyama vya kisiasa. Kuna wanaoogopa usalama wao maana kampeni zina vitimbwi kibao, kama uchawi, vitisho, rushwa nakadhalika. Wakifikiria purukushani za kampeni wanaona bora waendelee na majukumu yao. Ila kupitia utaratibu huu, tutakuwa na uhakika kupata mchango wao.
2) Wakurugenzi na viongozi wengine wanaopangiwa majukumu mengine.
- Katika katiba iwepo kifungu, kwa kiongozi ambae anapangiwa majukumu mengine, basi mshahara wake uwe wa kule anakopelekwa. Hii itasaidia uwajibikaji kwa viongozi katika nafasi zao, maana kufanya kazi chini ya kiwango ni kupoteza nafasi na marupurupu yake. itasaidia pia umakini wa mteuwaji katika kuchagua mtu sahihi utakuwepo.
- Pia itasaidia kupunguza upotevu wa pesa kuwalipa watu ambao hawafanyi majukumu husika. Haileti picha nzuri kuwa na wakurugenzi wawili au watatu katika eneo moja kupata mishahara ya ukurugenzi wakati aliyepo kwenye nafasi ni mmoja tu, wengine waliondolewa kupangiwa majukumu nyingine.
3) Utoaji wa mikopo unaohamasisha kusoma, Elimu ya juu.
- Hasara ya kupendelea husababisha kupata viongozi wasio weredi baada ya kumaliza chuo. Mtu alisoma kitu asichokipenda kwa sababu alifuata mkopo. Hivo akiwa kiongozi msitegemee ubunifu, ushawishi wala maendeleo makubwa katika fani aliosoma kwa kufuata mkopo 🙁.
Mapendekezo ya utaratibu iwe hivi;
- Mkopo wa kuanzia wote uwe 80% kwa ufaulu wa daraja la pili na la kwanza. Daraja la tatu pia mnaweza mkawakadiria. tuchukulie 80% kama mfano kuelekezana.
- Mwaka wa kwanza wa masomo ukiisha, Matokeo yatumike kupandisha mkopo au kupunguza mkopo kwa kigezo kizuri. Mfano, Msingi ni GPA ya 3 Ni sawa na 80%, watakaopata chini ya hapo basi kuna asilimia ziwe zinashuka, kwa mfano kila GPA 0.1 inayoshuka unashusha mkopo kwa 2%. Na watakaopata juu ya GPA ya 3 kuwe pia kuna asilimia zinapanda za mkopo, mfano Kwa kila gpa 0.1 mkopo upande kwa 1%. Kwa ufupi mfumo mzuri wa kimahesabu uwekwe, huu ni mfano.
- vyuo visiruhusiwe kubadili ada baada ya kusikia hili, au kuwe na kiwango cha juu cha mkopo ili kuweka mipaka ya ulaghai na ujanja kutoka vyuoni kubadili ada ili wajinufaishe.
Kupunguza uonevu wa maksi, na kingono kwa wanafunzi kwa kigezo cha mkufunzi kuharibu gpa.
- Mkufunzi atakaebainika, iwekwe hesabu ya kupunguza mshahara kwa asilimia kadhaa, kwa sababu mkufunzi huyo ana pesa nyingi mpaka anasumbua wanafunzi wake na kutumia cheo au nafasi vibaya.
-itolewe namba maalum kwa mkoa au wilaya, ili takukuru waweze kufatilia malalamiko ya mwanafunzi. Uwekwe utaratibu mzuri ili kukwepa uonevu au kusingizia.
4) Tume huru ya uchaguzi
Nami naungana na watanzania wengine wanaoomba kuwepo na tume huru ili kuondoa upendeleo, udanganyifu na ukataaji wa Matokeo kwa hisia za kisiasa.
- Moja ya sifa inayopendekezwa na wengi ni vyama vya upinzani wawe pia na wawakilishi wao katika tume ambao watawapendekeza wao. Tume iwe pia na wataalamu wa mahesabu na tehama kwa ajili ya ulinzi na uelewa wa matokeo yanapokuwa tayari.
- Mwenyekiti na viongozi wengine wa tume wapatikane kwa kupigiwa kura na wajumbe na sio kuteuliwa.
- Wasimamizi wakuu wa uchaguzi wa wabunge wasiwe walioteuliwa na Raisi, maana Raisi nae ana chama. Uwekwe utaratibu mzuri wa kuwapata. Na ikiwezekana vyama vipendekeze wawakilishi wao, kisha wawakilishi hao wapige kura kutafuta viongozi kati yao.
- Tume iwe tayari kusimama mahakamani ikiwa mjumbe au wajumbe wake watakuwa na maelezo ya msingi kupinga yaliyotendeka. Mtu ambaye si mjumbe hataruhusiwa kufungua kesi ili kuepusha watu wa mbali kuingiza siasa.
Haya ni baadhi ya mawazo ningependa yaangaliwe na yawepo au yaboreshwe kwenye katiba mpya kwa ustawi wa taifa letu, Tanzania. Nakaribisha kuongezea mawazo au kuboresha wazo ili kunufaisha taifa letu.
Tanzania nchi yangu nakupenda.
NB; Ikiwa umependa mawazo haya usisahau ku-like ili wengine pia waweze kuyasoma na kuyaboresha.
Shukrani.

- Mikopo itolewe kulingana na ufaulu na bidii ya wanafunzi.
- Kupendelea fani fulani, Ni kufanya wanafunzi wasio na mapenzi na fani husika kuomba nafasi ili wapate mikopo. Hivyo kuua vipaji na nyota zao walizokirimiwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuifaidisha jamii na taifa kwa ujumla. Wanaacha fani zao wazipendazo kwa sababu hazina mikopo. Ila Katika dunia ya sasa fani zote ni muhimu katika mfumo wa maisha na maendeleo.
- Tuna mifano halisi, kuna watu wamefanikiwa katika mziki, wengine kushona nguo, wengine mpira nk, sio lazima wote tung'ang'anie sayansi wakati huipendi. kufanikiwa kwa kila fani ndiko kunakotengeneza mfumo wa maisha wa kutegemeana katika jamii, na kufanikiwa kila mmoja katika eneo lake.

Upvote
0