Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
WATU wasiojulikana wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbali mbali kisiwani Pemba vyenye ujumbe wa kuwataka watu wenye kuweka vikwazo kwa wananchi kujiandikisha wajitayarishe mwaka 2010 utakuwa ni wenye mateso kwao ikiwa wataendelea kuwapinga watu wanaotaka vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Wete, Khamis Juma Silima alisema tayari wamepokea taarifa za kuwepo kwa kundi hilo lenye kusambaza vipeperushi ambapo vyombo vinavyohusika vinalifanyia kazi suala hilo.
Alisema kwamba uchunguzi wa kina unafanyika kuhusiana na kundi hilo kabla ya hatua kuchukuliwa na watakaopatikana na hatia watachukuliwa sheria kali dhidi yao kwa kuendesha vitisho dhidi ya wananchi ambapo lengo alisema ni masheha.
Afisa huyo alisema kwamba kundi hilo limeundwa kwa dhamira ya kufanya vitendo vya hujuma ambapo tayari wameanza kuwatisha baaadhi ya Masheha kutokana na msimamo wa viongozi hao katika kusimamia sheria ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
Amesema Afisa Tawala huyo alisema kuwa kundi hilo ndilo linalohusishwa na kumwagia tindikali Sheha Mussa Kombo Omar ambaye ilibidi apelekwe kwa matibabu zaidi Unguja.
Mbali ya hatua hiyo, kundi hilo linahusishwa na kufanya vitendo vya kutaka kuhujumu kazi ya usajili na utoaji vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na hivi karibuni limetoa vitisho kwa kumwandikia vipeperushi Sheha wa Shehia ya Kambini, Ali Said Ali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Saleh Bugi alisema kwamba Polisi inatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi kinachotaka kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na kwamba wanafuatilia suala hilo.
Kamanda Bugi alisema wamefanikiwa kupata moja wapo ya kipeperushi kilichosambazwa kwa Sheha wa Shehia ya Gando wakimtishia maisha.
Ole wako tukupate, tutakuua wejifiche, lakini 2010 ufikapo utaona Alikariri Kamanda Bugi sehemu ya ujumbe kwenye kipeperushi alichotumiwa Sheha wa Gando.
Vipeperushi hivyo amekabidhiwa Mkuu wa Wilaya na anavifanyia kazi kwa sasa,aliongeza Afisa Tawala Khamis.
Bugi alisema uchunguzi dhidi ya kundi hilo linalojiita kundi la kuhujumu masheha liliandika vipeperushi vya kumtisha sheha huyo na kwamba: Usipokubaliana na mahitaji yetu kitakachokukuta usitulaumu.
Katika suala zima la usajili na utoaji wa vitambulisho katika wilaya ya Wete ambayo awali liliripotiwa kuwa na vurugu, kazi hiyo tangu Jumatatu iliyopita ilikuwa ikiendelea vizuri.
Wakati huo huo watu wanane wakazi wa Kijiji cha Kiuyu Minungwini Mkoa wa Kaskazini Pemba jana wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na fomu za kughushi za Idara ya usajili Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kisiwani hapa.
Watu hao walifikishwa Mahakamani mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Kaskazini Pemba, Makame Khamis wakituhumiwa kujipatia usajili huo kinyume na kifungu 312 cha sheria ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 2004.
Mwendesha mashtaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Abdallah Issa Mgongo ameiambia Mahakama kwamba watuhumiwa hao Agosti 18 wakiwa katika Afisi ya Usajili wa Vitambulisho ya Wilaya ya Wete waliwasilisha fomu za kughushi kwa nia ya kutaka kupewa kitambulisho.
Walioshitakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Bakar Hamad Ali (20), Fatma Ali Nassor(20), Bakar Khamis Haji(18), Saada Ali Pandu (22), Fatma Mohammed Ali(18), Sophia Said Salum(18), Fatma Malik Bakar(20) na Shamte Hamad (19).
Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande hadi Septemba 2 wakati kesi hiyo itakapotajwa tena ambapo Mahakama itazingatia pia ombi la upande wa utetezi la kutaka watuhumiwa hao kupewa dhamana kwa mujibu wa sheria.
Wakili wa washtakiwa, Ussi Khamis aliambia Mahakama kwamba wateja wake ni watoto wadogo na ambao ni wanafunzi hivyo, aliomba wapewe dhamana kwani kosa lenyewe sio kubwa kiasi cha kutopewa dhamana.
Licha ya ombi hilo, Hakimu Makame Khamis alisisitiza kwamba Mahakama yake itazingatia na kutoa uamuzi wa ombi la dhamana Septemba 2, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Watuhumiwa hao ni wanafunzi wa Shule mbali mbali katika Jimbo la Ole, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.