Ujumbe sio mbaya unaonyesha kuleta umoja miongoni mwa WaZanzibari maana Tanzania nzima kunafanyika uchaguzi haijaonekana mikoa ya nyanda za juu kupelekwa majeshi na vifaru,Mbeya kuna mauaji toka walikuwa wanachunana ngozi hadi kufikia kufanya biashara ya kuuza viungo vya albino hatujaona kupelekwa majeshi,Mara mapigano ya kikabila kila siku hatujaona kupelekwa majeshi ,Dar majambazi kila siku tena wanatumia silaha za kisasa hatujaona kupelekwa majeshi ,mikoa ya kaskazini kila siku watu wanavuka mipaka na kuiba ng'ombe hatujaona kupelekwa majeshi ,Kikwete anatuambia nini hili la kupeleka majeshi Pemba ,kama kulinda usalama alete vipimo vya usalama unaohitajika hata kufikia kupelekekwa majeshi. Kama kujitenga kwa Pemba hakuhitaji majeshi maana walishaandika barua ya wazi na habari zao kuandikwa magezetini ,hili la kupeleka majeshi ni lazima litakuwa na maana nyingine ambayo haikubaliki ndani ya visiwa viwili vya Zanzibar ,jini likujualo halikuli likakwisha ,hivyo WaZanzibari kama watauwana au watamezana ,WaTanganyika inawauma nini ? Kama kweli mna imani mungezuia uchunaji wa ngozi,uuzaji wa viungo vya binadamu mauaji ya koo na kikabila humo ndani ya Tanganyika kwanza ndipo mkarukia Zanzibar ,Tanganyika imejaa mauaji tena ni ya kila siku mpaka wananchi wa huko wamekufa ganzi na kuona ni jambo la kawaida ,leo hii mnapeleka majeshi kila kona ya dunia eti kulinda amani ,huku ni kujipendekeza kwa serikali ilipo madarakani ,kwani wengi wa wanaokufa wamo humu Tanganyika kuliko huko wanakokwenda linda amani.
Hii inahitajika Waziri wa ulinzi atoe tathmini ni WaTanzania wangapi wanauwawa kila siku ,atupe japo wastani ya vifo vinavyotokea kwa ujambazi ,mauaji ya kwa ajili ya kupata viungo vya binadamu na kuviuza,uchunwaji ngozi ,vita vya koo,mauaji yanayosababishwa na wizi wa ng'ombe ,atuonyeshe na kuona kama humu Tanganyika mna amani ?
Kinachotokea ni kuwapeleka wanajeshi wa Tanganyika nchi za nje kwa kisingizio cha kwenda kulinda amani wakati ndani ya Nchi hii hamna amani ,huko ni kuwapeleka waTanzania kama chambo na hata data za wanaokwenda na wanaorudi hazitolewi ,kitendo cha kuwapeleka majeshi nje ya nchi ni kutaka misifa jambo ambalo iko siku mtalia kilio cha mbwa mdomo juu.Watakapopata kisago huko,hatuombei hilo litokee lakini kwa mnavyowafanyia watu wa Pemba basi dua zipo njiani.
Umoja wa Zanzibari ni muhimu sana kwa jinsi Tanzania inavyoendeshwa kama WaTanganyika wanaridhika hilo ni lao na wao ndio watajua dawa ya kujinasua na kasumba hizi za KiCCM za kulindana na kufikia kulisimamisha bunge lisikemee viongozi wahujumu uchumi ,hilo ni moja ya jambo ambalo WaZanzibari wanaliona limevuka mipaka ya kiutawala.