Vipers SC Kuipamba Wiki ya Mwananchi 06.08.22

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Mabingwa wa Uganda wanatarajiwa kushiriki katika kilele cha Wananchi hapo Agosti 6.

Pia Mabingwa wa LigiKUU Tanzania Bara watatumia mtanange huo pia kufanya tathmini ya Mchezaji Ceaser Manzoki kama long time replacement ya Heriethier Makambo ambaye mkataba wake unafikia ukingoni majira ya joto.

Baada ya Coach Nasreddine Nabi kuletewa jina lako hapo July mosi, alipendekeza kumuona na kutathmini uwezo wake. Hiyo ndio sababu ya Mabingwa wa Nchi kuwaalika Vipers SC kwenye kilele hiko.

Aidha Ceaser Manzoki anamaliza mkataba wako Oktoba 2022. Hivyo ataendelea kuwako klabuni hapo mpaka muda huo au endapo itatokea offer nono ya dau lisilopungua la Miliono 200.

Hapo awali Klabu ya Yanga SC ilikuwa kwenye mipango ya kuwaalika mabingwa wa Angola.
 
Manzoki amesaini Pre Contract na Simba SC, nachojua atakuja kuwafunga hiyo siku yenu halafu mwishowe anaenda Msimbazi.

Mmefanya vizuri sana kumpa mazoezi.
 
Manzoki amesaini Pre Contract na Simba SC, nachojua atakuja kuwafunga hiyo siku yenu halafu mwishowe anaenda Msimbazi.

Mmefanya vizuri sana kumpa mazoezi.
Pre contract ni kama barua ya posa, unaweza ukaposa lakini akaoa mwingine.
Sitegemei Yanga kujihususha na Manzoki, Tayari walisha jifunza Kwa Juma Balinya
 
Red arrows si hadi walitangaza kwenye facebook yao? Hahahahaha so vipers wamefatwa kisa Manzoki?
 
Mazuzu mlisema mshamalizana na Phiri ila mwisho wa siku akawapiga dole la kati kumbuka Yanga wachezaji wanafuata hela ila simba ni super brand sasa eneleeni kujidanganya.
 
Pre contract ni kama barua ya posa, unaweza ukaposa lakini akaoa mwingine.
Sitegemei Yanga kujihususha na Manzoki, Tayari walisha jifunza Kwa Juma Balinya

Sasa Manzoki na balinya wana uhusiano gani? Utopolo mna nini lakini jamani.
 
Wale red arrows vipi tena, walijipamba bure, au yanga wameghairi sababu ya kiherehere cha red arrows kuanza kuvujisha tarehe ya ndoa kabla muoaji hajatoa tamko.

La clube pesidente Hersi Said Ali
La Proffeseri Nabi

Hao wote wanataka kumfanyia tathmini Ceaser Manzoki.
 
Asec Mimosas kama asingecheza na Simba SC, leo hii Aziz Ki tusingemuona Yanga.

Lobi Manzoki kama asingehusishwa na Simba SC, leo hii tusingesikia kuwa ni mpango wa replacement ya Makambo.

Sasa ubishi unatoka wapi mkiambiwa kuwa Simba SC ni Timu Kubwa..Khaaa!
 
Pre contract ni kama barua ya posa, unaweza ukaposa lakini akaoa mwingine.
Sitegemei Yanga kujihususha na Manzoki, Tayari walisha jifunza Kwa Juma Balinya
Sasa balinya umlinganishe na Manzoki? Yule Balinya ilikuwa ni bahati tu kama ilivyotokea kwa Mpole ila kwakua nyinyi mlikuwa majinga mkaona ni bonge la striker, ila huyo Manzoki alikuwa anamkalisha hata huyo Mcongo wenu huko walikotoka.

Kuwa na heshima na adabu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan Manzoki anawauma vichwaa utopolooo, vipi DOMOLEPEE hana mpyaaa???
Itokee katua Msimbazi mioyo itawauma sana aiseeh.
 
La clube pesidente Hersi Said Ali
La Proffeseri Nabi

Hao wote wanataka kumfanyia tathmini Ceaser Manzoki.
Funguka useme kwamba, moyoni mwako ukitulia vizuri na ukaacha kufikiria kwa kutumia makalio (kama ambavyo huwa unafanya), unaona kabisa kuwa Manzoki ni striker mzuri kuliko striker yoyote mliyenaye hapo kwenu.
 
Aziz KI Ameonekana kabla hata hamjacheza nao.

Lobi Manzoki yeye ndiye aliyeshawishika kutamaniwa na Mabingwa Watetezi.

Funguka useme kwamba, moyoni mwako ukitulia vizuri na ukaacha kufikiria kwa kutumia makalio (kama ambavyo huwa unafanya), unaona kabisa kuwa Manzoki ni striker mzuri kuliko striker yoyote mliyenaye hapo kwenu.

Ukisoma uandishi kwa Makingi.

Utagundua kuwa nimeandika habari ya Manzoki kuchukua nafasi ya Makambo.

Hatutafuti mshambuliaji bali tunatafuta back up bora au mshambuliaji bora wa ziada.

WE ARE CURRENTLY COMPLETE AS A TEAM.
 
Ili mchezaji aonekane lazima acheze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…