Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mabingwa mara nne wa Ligi Kuu Uganda, Vipers SC wameweka dau mezani kwa nia ya kumshusha kikosi hapo straika matata wa Yanga, Fiston Mayele msimu ujao.
Chanzo chao kimeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umeanza mazungumzo yakimuhusisha meneja wa mchezaji huyo pamoja na uongozi wa Yanga.
"Ndiyo, Vipers wameonyesha dhamira ya kumsaini Mayele kupitia wakala wake na Yanga wenyewe," kilieza chanzo hicho na kuongeza;
"Wameshaweka ofa yao ya kwanza mezani ambayo ni kati ya Dola za Marekani 50,000 (Sh117milioni) hadi Dola 100,000 (Sh230milioni) na mazungumzo yanaendelea.
"Vipers inataka kuwa na kikosi imara wakati itakapocheza michuano ya CAF, hasa kama itashinda ubingwa wa ligi au wa Kombe la Uganda."