Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mwaka 2005 watu waliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania. Wapo wengi walioamini hiyo ahadi lakini mimi sikuwa mmojawapo. Nilijua tu ni zile zile blah blah za kila siku.
Sasa basi kwa vile kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndiyo zimeshapamba moto, nadhani itakuwa vyema kwa Dr. Slaa kuazima mstari kutoka kwenye 'playbook' ya Ronald Reagan na kuanza kuwauliza watu "are you better off than you were five years ago"?
Siyo lazima (w)autumie huo mstari kama ulivyo katika lugha ya Kiingereza. (W)anaweza kuupa tafsiri inayofaa kuendana na mazingira yetu lakini maana ikabaki palepale.
Kama kuna ambao hawajui nazungumzia nini au kama umesahau nazungumzia nini, hapo chini ni kipande cha mdahalo kati ya gavana Ronald Reagan na raisi Jimmy Carter katika mdahalo wao wa mwisho ambapo inasemekana mstari huo ndiyo ulikuwa 'game changer' katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 1980 ambao gavana Reagan alimshinda raisi Carter kwa kishindo.
YouTube - Reagan 1980 Are you better off than you were four years ago?