Elections 2010 Vipi Dr.Slaa akianza kuuliza hili....???

Elections 2010 Vipi Dr.Slaa akianza kuuliza hili....???

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Mwaka 2005 watu waliahidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania. Wapo wengi walioamini hiyo ahadi lakini mimi sikuwa mmojawapo. Nilijua tu ni zile zile blah blah za kila siku.

Sasa basi kwa vile kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndiyo zimeshapamba moto, nadhani itakuwa vyema kwa Dr. Slaa kuazima mstari kutoka kwenye 'playbook' ya Ronald Reagan na kuanza kuwauliza watu "are you better off than you were five years ago"?

Siyo lazima (w)autumie huo mstari kama ulivyo katika lugha ya Kiingereza. (W)anaweza kuupa tafsiri inayofaa kuendana na mazingira yetu lakini maana ikabaki palepale.

Kama kuna ambao hawajui nazungumzia nini au kama umesahau nazungumzia nini, hapo chini ni kipande cha mdahalo kati ya gavana Ronald Reagan na raisi Jimmy Carter katika mdahalo wao wa mwisho ambapo inasemekana mstari huo ndiyo ulikuwa 'game changer' katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 1980 ambao gavana Reagan alimshinda raisi Carter kwa kishindo.

YouTube - Reagan 1980 Are you better off than you were four years ago?
 
Kila kitu kwako ka hisani ya Watu wa Marekani! Kuandika Katiba kwa hisani ya Watu wa Marekani! Kupiga Kampeni kwa hisani ya Watu wa Wamerakani!
 
Nyani Ngabu,
Hili wazo zuri sana ktk agenda za mkutano mzima wa Dr.Slaa kwa wananchi. Na kwa kuongezea tu kila mkutano wake adai kuwa tayari kupambana na JK ktk mdahalo uwanja wa TBC au kokote anakochagua JK..afanye hivyo kila anapokwenda na maadam JK atachomoa, wananchi (kwa desturi zetu) watamwona JK zuga tu hana ubavu wa kupambana na Dr.Slaa. Ni muhimu sana Chadema kuwaweka CCM ktk kujihami muda wote tokea Ufisadi, miaka 50 ya Umaskini, Ahadi za JK na pia kuonyesha nguvu ya Dr.Slaa dhidi ya JK..
 
Sio dr slaa pekee yake anayetakiwa kuuliza hivyo, bali kila mgombea anapaswa kuwauliza wananchi maswali hayo pia kuwakumbusha kuhusu ahadi ya maisha bora ya mwaka 2005, kwa hakika kutokana na staili ya kuwabombard wapiga kaura na aahdi kibaoa chadema inatakiwa kuja na strategy ya kufanya uchambuzi wa kina wa ahadi zilizotolewa 2005 na zilivyotekelezwa.

Utoaji wa ahadi mopya na nyingi ni kakati maalum wa ccm na jk kuwachanganya wapiga kura ili wasiwasilkilize wapinzani.

Hivyo wapinzani wanatakiwa kuchuakua hatua haraka iwezekanavyo kuzuia wapiga kura kuchanganywa na ahadi hizi ambazo hazitekelezeki
 
Kila kitu kwako ka hisani ya Watu wa Marekani! Kuandika Katiba kwa hisani ya Watu wa Marekani! Kupiga Kampeni kwa hisani ya Watu wa Wamerakani!

Je ni swali halali au sio halali kuuliza/kuulizwa?
 
Ilo swali ni la msingi ila watu hupumbazwa na khanga,elfu kumi,kofia,
 
IMG_1766.JPG


Sijui hapa Kibunango atanishawishaje nimchague yule alie toa ahadi ya Maisha bora kwa kila Mtanzania
 
I guess Companero is better off than he was five years ago....
 
Back
Top Bottom