Vipi Kuhusu Madaktari Bingwa wa Masikio Arusha?

Vipi Kuhusu Madaktari Bingwa wa Masikio Arusha?

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
5,313
Reaction score
2,646
Habari wana JF

Kuna ndugu yangu mmoja kanipigia simu akaniambia kuwa kuna mabingwa wa kutibu masikio wapo Arusha na wanatibu bure, nilipo muuliza kuwa kaambiwa na nani akasema ameona katika TV wakitawataka watu wenye matatizo ya masikio waende kutibiwa.

Kwa kuwa mie ni miongoni mwa wagonjwa wa ugonjwa wa masikio nimeona ni vyema niulize hapa ili nipate uhakika kabla sijaenda huko arusha.

Hivyo kama kuna yeyote ambae amesikia taarifa ya habari ya saa mbili anaweza kunisaidia kwa kunifafanulia zaidi. Copy kwa Mzizi mkavu King'asti
 
Back
Top Bottom