Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Majanga ya asili duniani yapo na yanaweza kutokea muda wowote. Kuna maeneo mfano Asia nchi kama za Japan, China, Indonesia, Uturuki, Iran n.k wao matetemeko ya ardhi ni sehemu ya maisha, nchi kama Marekani wao vimbunga ni sehemu ya maisha. Hizi nchi wanajipanga sana kupunguza madhara ya haya majanga muda wowote endapo yatatokea.
Sisi inawezekana hatuko kwenye ukanda wa majanga ya aina hii lakini haimaanishi kwamba hayatatokea kabisa. Sasa tujiulize endapo siku moja tetemeko hata la wastani tu litatokea Dar haya maghorofa ambayo watu wana mashaka na viwango vyake vya ujenzi, nondo hazielweki, yataweza kuhimili kweli hali hiyo? Hii miundombinu ya Kariakoo ambayo hata sehemu za wazi za kukusanyia watu 3,000 ni kama hakuna itaweza kuhimili? Hizi timu au tume za uokozi za kujivuta zina uwezo kupunguza maafa ya vifo??
Tunaweza kuendelea kufanya maombi na kusema "tusiombee hayo"