Vipi likitokea tetemeko la Ufa au Tsunami Dar? Ghorofa za mji zitahimili?

Hakuna neno linanikera kama kutaja awamu za viongozi kila wakati. Kwani angesema tunaishukuru serikali kwa kufanya ......... angepungukiwa na nini? Uchawa unapunguza kitu kwenye ubongo wa machawa.
Kabisa uchawa ni laana, ingekuwa hivyo alivyosema haya si wangeyabaini mapema na kuzuia? Kwa sababu huwezi kufanya marekebisho bila kibali kutoka serikalini na hapo ingekuwa sehem ya kuanzia kubaini changamoto ambayo ingeleta haya madhara yaliyotokea.
 
Sasa mbona hata huo moto kuzima ajali zake bado ni changamoto sana!
 
Maaamae imebidi nicheke tuu
 
Hivi hatujafanya risk assessment kujua tuna janga kubwa la ajali za barabarani nchini ili tuwe na Air ambulance za kuwahisha majeruhi hospitalini??
 
Inachekesha sana kwa ujinga wanaofanya baadhi ya machawa ila inauzunisha mno kuona watu wakipoteza uhai alafu kuna wachache kazi yao ni kuimba mapambio.
Mm hua natamani sana haya majanga yawapate hao hao wapiga mapambio halafu wasife bali wapate kilema cha maisha ili waendelee kuimba mapambio wakiwa kitandani.
 
Vibali vyenyewe vinatolewa kwa kutoa kitu kidogo. Wakishapewa kitu kidogo wenye mamlaka hawaangalii tena ishu ya viwango na masharti ya ujenzi. Pakitokea janga ndiyo wanaanza kumtafuta wa kumwangishia zigo.
 
Sasa mbona hata huo moto kuzima ajali zake bado ni changamoto sana!
Sijasema tuko perfect huko ndiko tunatakiwa kuboresha lakini pia maujenzi yetu ya nyumba ni sababu moja kuu yenye shida fikiria kama kuna moto mfano nyumba Manzese katikati hiyo gari itafikaje hapo? na huo ni mfano mmoja tu ila ni eneo linahitaji maboresho sana tu. Nchi za wenzetu hizi huduma unazilipia mpaka ambulance hakuna bure.
 
Hivi hatujafanya risk assessment kujua tuna janga kubwa la ajali za barabarani nchini ili tuwe na Air ambulance za kuwahisha majeruhi hospitalini??
Ajali za barabarani asilimia 90 ni uzembe wa madereva solution sio kujaza ambulance barabarani ni elimu na sheria kali kuzuia uzembe wa matumizi ya barabara. Juzi tumekemea kuweka majeneza nje ya Hospital sio busara japo nafasi kubwa au wateja wengi ni walioko Hospital lakini sio busara sasa kujaza ambulance barabarani ni kama unawaambia abiria tuko hapo mpigwe mwereka tuwabebe. Tujiulize kwanini ajali nyingi? je ni barabara zetu au watu wazembe ukipata jibu ndio nguvu unapeleka huko.
 
Mama anapewa shukrani hadi kwa watu waliopoteza maisha 🤣 hili taifa linatia aibu
 
Kwa hiyo unataka kusema hili jengo lililodondoka ndio imetokea mara ya kwanza?Haya tangu enzi ya uhuru hadi leo miaka 60 imepita ndio imeshindikana kununua vifaa vyote muhimu vya uokozi?
 
Vibali vyenyewe vinatolewa kwa kutoa kitu kidogo. Wakishapewa kitu kidogo wenye mamlaka hawaangalii tena ishu ya viwango na masharti ya ujenzi. Pakitokea janga ndiyo wanaanza kumtafuta wa kumwangishia zigo.
Hili ni tatizo kubwa linaloendekezwa na uongozi ambao sio makini.
 
ovyo kabisa,
 
Kwa hiyo unataka kusema hili jengo lililodondoka ndio imetokea mara ya kwanza?Haya tangu enzi ya uhuru hadi leo miaka 60 imepita ndio imeshindikana kununua vifaa vyote muhimu vya uokozi?
Vifaa gani unaongelea hapa? wewe unalaumu kijumla jumla tu vifaa gani unaongelea. Tuache tabia za kulalamika tu. Sasa sema wewe ni jumba la ngapi kuanguka toka tupate uhuru? chukua majanga yote nchi angalia vitu hivi Potential + Frequency + likelyhood + financial loss utapata jibu unahitaji nini.
 
Kwa hiyo unataka kusema hili jengo lililodondoka ndio imetokea mara ya kwanza?Haya tangu enzi ya uhuru hadi leo miaka 60 imepita ndio imeshindikana kununua vifaa vyote muhimu vya uokozi?
Wewe nyumbani kwako una hata first aid kit? au fire extinguisher? ukiendesha gari unafunga mkanda? wengi tunadharau mkanda japo tunajuwa mkanda unaweza kuokoa maisha yako ukipatwa na ajali, lakini kwanini watu wanadharau, sababu anadhani hawezi kupata ajali yeye dereva mzuri au haamini mkanda ila siku likimpata ndio atakumbuka muhimu wa mkanda au fire extinguisher. Kiuhalisia hakutakiwi jumba kuanguka labda livunjwe kusudi lakini kwetu yanatokea sasa tujiulize kwanini? Nyumba haitakiwi kuongezwa kitu ikishajengwa na kupitishwa shida kuu kwetu kuvunja vunja kuongeza vyumba sijui maduka hapo ndio shida. Unataka kubadilisha matumizi ya nyumba vunja yote jenga upya huwezi marufuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…