Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Mshikaji wangu baada ya kunusurika kwenye ajali nyingi na misukosuko ya mahusiano ikabidi aanze kushirikisha watu Ili apate mke sahii wa kuoa.
Kwenye harakati hizo huku akiendelea kumuomba Mungu (Kwa mujibu wake), jamaa yake mmoja aliepo kigoma akamwambia Kuna Binti anamuona kanisani na inaonekana katulia, jamaa akafunga safari kutoka Dodoma mpaka kasulu vijijini kwenda kumuona mchumba 😁😁.
Kufika huko akakutanishwa na mchumba, jamaa ananiambia binti sio mzuri sana akimaanisha sio yule akipita watu wote lazima wamuangalie, ni binti wa kawaida tu, wala sio mbaya heshima hiko asilimia 99.99 kwa jinsi alivyomuona.
Jamaa akamuuliza kuhusu habari za washikaji zake binti wa nyuma binti akamuhakikishia yuko bikira, yaani tokea kuzaliwa hajawahi kuguswa. Aliniambia alimuuliza maswali mengi ya kiintelijensia lakini binti licha ya kua ni wakijijini sana lakini alijibu maswali vizuri.
Mwisho wa siku jamaa akakata shauri ya kumuoa kabisa na hapa tumeshaungwa kwenye group la whatsapp ya harusi. Ndoa inafungwa mwezi wa 8 huko.
Imenifanya nitafakari kidogo, hivi hawa wanawake wa kutafutiwa wanadumu kweli? Mimi nadhani upendo wa kweli lazima umuone mwanamke/mwanaume ndio umpende ukishampenda ndio unakata shauri.