LGE2024 Vipi, mtaani kwako muamko kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kauli ya kiume sana hii,.unajua mkuu
Plato, katika kazi yake "The Republic," alikuwa na mtazamo hasi kuhusu demokrasia. Aliona demokrasia kama mfumo ambapo watu wengi, ambao wanaweza kukosa elimu au hekima ya kutosha, wanapewa mamlaka ya kuchagua viongozi. Alisema kuwa katika demokrasia, kuna uwezekano mkubwa wa watu wasio na ujuzi, maarifa, au maadili bora kushinda uchaguzi kwa sababu wanavutia kwa hotuba nzuri na ahadi za kuvutia.

Kwa Plato, demokrasia inaweza kusababisha uongozi mbaya kwa sababu umati wa watu unaweza kushawishiwa kirahisi na wale wenye uwezo wa kuvutia hisia zao, hata kama hawana sifa za kuongoza. Hivyo, alihisi kuwa demokrasia inaweza kumruhusu "wajinga" kushinda uchaguzi na kuwa viongozi, jambo ambalo linaweza kudhuru jamii kwa sababu ya maamuzi mabaya ya kisera yanayotokana na uongozi usio na sifa. Plato alipendekeza kwamba jamii inapaswa kuongozwa na "wafilosofa wafalme"—watu wenye hekima na elimu ya juu—ambao wana ujuzi wa kujua kilicho kizuri kwa jamii nzima.
 
Mtaani kugumu Maji hakuna wala umeme..duh
 
Mtaani kugumu Maji hakuna wala umeme..duh
Siku hizi umeme na maji mgao, upatikanaji ni changamoto nyingine Hali kadhalika gharama za umeme nazo zinapaa sababu ya kumuongezea Kodi ya huduma mlaji licha ya ahadi tamu kuwa Bwawa likikamilika gharama ya umeme itashuka na ziada tutauza nje.
Ogopa wajinga wakiwa wengi, wanaweza kuchagua Rais
 
Hapo kwenye kuuza nje, ndo pagumu
 
Wala hakuna mwamko
Huu uchaguzi utadoda

Ova
Madhara aliyofanya dhalimu magu kwenye chaguzi zetu, yatafanya chaguzi zetu kuwa na wapiga kura wachache sana. Na viongozi watazidi kuwa na mbali na wananchi kwani hawatakuwa na ridhaa ya umma.
 
Muitikio ni mdogo sana hii imetajwa kuwa sababu ni watu kutokuwa na imani na viongozi wanaowachagua tena.

Siasa inatumika kama njia ya kujinufaisha.
 
wanainchi wakishaamua bana,

hata ufanye ushirikina wa aina gani au ufanye matambiko sijui ya kuchoma vitenge au kuchukua vijana misukule,

hawabadiliki, ni CCM tu kila kona ya nchi dah 🐒
Ulianza kuandika vizuri halafu ulipoitaja CCM ukawa umeharibu kila kitu,yaani wananchi wamegoma kabisa kama hamna kinachoendelea
 
Kesho nitaleta mrejesho maana ndo siku ya kwenda kujiandikisha kwenye daftari hapa mtaani kwangu
 
Kitufe cha ku ignore huyu mpuuzi please
 
Kitufe cha ku ignore huyu mpuuzi please
rest silence in peace gentleman,

wacha kubabaika na mayowe yako hapa na huna hoja. peleka mihemko yako huko

kwendraaa dhako hapa, alaaaa
 
Ulianza kuandika vizuri halafu ulipoitaja CCM ukawa umeharibu kila kitu,yaani wananchi wamegoma kabisa kama hamna kinachoendelea
wamegoma maandamano haramu yaliyochochewa na mlevi kwa usaliti wa kiwango cha juu sana cha uzalendo,

eti wewe unasema nin gentleman?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…