Vipi umeshawahi kuharibu kitu cha rafiki yako? Mlimalizanaje?

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
901
Reaction score
3,112
yaani unaachiwa kitu na rafiki yako mfano laptop mara inakuzimikia na bahati mbaya kuna vingine hata ukipeleka kwa fundi havifai tena kutibika au spea unakosa.

hapo ni mawili ulipe pesa au urafiki pia ufe mazima.

mm kama mimi sinaga tabia ya kulipisha mtu kitu.

iliwahi nitokea nimenunua headphone nimetumia siku mbili kisha rafiki yangu akalalanazo kuamka asubuhi zimekatika nilinunua tu 15,000

unaweza jikuta umeharibu kitu cha fhamani sana na ukasamehewa vile vile unaweza kuharibu kitu cha 500 na urafiki ukafa mazima.
 
KWANINI UMUAZIME MTU KITU?

ME NISHAKOMAGA KUAZIMA WATU VITU BROO KWANZA UKIMUAZIMA MTU KITU HAKITUNZI KABISA

ME KUNA JAMAA NILIMPA KITU CHA ELFU 25 ANAKAA GHETTO PEKE YAKE NA ALIKIWEKA CHINI YA KITANDA SAIVI ANANIAMBIA HAKIONEKANII!!
 
Niliachiwa simu na jamaa yangu ilikuwa ni itel, lock ya simu ilikuwa ni PASSWORD lakini cha ajabu asubuhi naamuka nakuta lock imebadilika na kuwa PIN sasa sielewi niandike namba gani wakati mwanzo nilikuwa natumia herufi. Sema sisi ni marafiki tulioshibana, nilimwambia acha ufala mtoto wa kiume una lalamika kisa itel huo ni umama. Basi kesi ikaisha mambo mengine yakaendelea.
 
Hua nakua na uoga wa kuazima kitu kwa mtu mana mm sina naazima kikiharibika kwenye mikono yangu ataelewaje? Hapana kama sina hua natulia naamin shida hazijawah kudumu
 
Busara ndiye tegemezi la yote kwa upande wake n upande wako.

Kwa upande wako; uwazi, ukweli pamoja na kujali.
1. Namaanisha kama umeharibu kweli ni hekima kurekebisha kitu cha watu. Na sio halali kukimbia au kutaka mchangie gharama na mmiliki ilihali wewe ndiye muhusika wa tatizo. Itategemea kama unajitambua

2. Ikiwa haujaharibu na una uhakika ubovu wa hicho kitu wewe sio sababu. Kwa hapa ni kumwelezea hali halisi kwa uwazi huku kutathimini matokeo yake. Kama unaona kabisa anatupia lawama kwako na hakubali ukweli huo basi una mawili.
A) Kukubali kuumia na kumuachia mungu (unaingia hasara, ijapokuwa unalinda heshma yako au utu)
B) Kama mbwai na iwe mbwai hata akikuona mbaya basi. (Hauingii hasara lakini kuna kitu kinapungua)
Maamuzi ni yako.

3. Kama ubovu huo umetokana na matumizi yenu wote. Yani unakuta kitu kilikuwa na matatzio fulani nawe alipokuazima ukasababisha jengine, ambalo limefanya sasa hiko kitu kuwa kibovu kabisa (hakitumiki).
Mfano amekuazima baiskeli, ilikuwa break zake haizkamati, nawe ikatokea unataka kujitetea kwenye mteremko mkali, nyororo ikakatika.
Basi ni vyema na ni hekima walau ukashiri kwenye matengenezo au gharama za matengenezo. Yani usiwe mzigo wa mmoja, hiyo haijakaa sawa

Na kwa upande wa mmiliki; Huruma, Moyo wa ujasiri na Ukweli
1. Unaweza kuamua kusamehe yote. Hii itokane na nadhiri yako mwenyewe moyoni. Haijalishi yeye ndiye sababu. Huenda ikasaidia kuepusha sintofahamu za hapa na pale (Ila ni kukubali kuingia hasara na unatakiwa ulitambue hilo)

2. Kama kitu chako hakikuwa na dosari basi unastahili kudai stahiki yako kwa lugha yenye staha na busara ndani yake. Na endapo ataonyesha ukaidi kuna mawili.
A) Kudai kwa kufuata misingi au taratibu salama, pasiopo ghasia.
B) Acha kiumane, potelea pote...waarabu wanasema "Fal yakun, Ma yakun". Atalipa tu atake asitake

3. Kama unaona tatizo limesababishwa nanyi nyote kama kwenye ile baiskeli, unamweleza uhalisia na kutokana na kupungukiwa basi usingewa kumudu gharama zote peke yako. Hivyo unamhitaji naye achangie walau turudishe kitu hicho katika matumizi

TATIZO LILILOPO
Busara siku hizi ni gharama ijapokuwa hakina hata bei fulani.
Kuipata ni sawa na kusema inauzwa na haijulikani ni senti ngapi
 
Mimi jambo nililomuharibia rafiki yangu bado hajalisahau mpaka leo tumekuwa watu wazima,tukikutana huwa ananikumbushia.
Ilikuwa miaka ya 90 kwenye Mitihani ya Mock ya Kidato cha 2.
Tukiwa kwenye mtihani wa hesabu,yeye akiwa mbele yangu,nilimuomba anipatie mtihani wake nigelezee,maana mimi sikuwa vizuri kwenye hesabu.
Jamaa akanipatia kupitia chini ya kiti,baada ya msimamizi kuzubaa.

Bwana ndugu yenu nikacopy karatasi yote(ilikuwa karatasi ya kujibia zile plain).
Nilipomaliza nikajua ni rafu tu,kwahiyo sikumrudishia.

Baadae kidogo,msimamizi akatuamuru tusimame muda umeisha,kila mtu apange karatasi zake alizojibia na karatasi ya maswali ili yeye apite kuzibana.

Kwa hofu ya kuonekana nina karatasi nyingi,nikatafuna ile ya jamaa.

Sasa wakati msimamizi amekaribia kwa jamaa yangu,jamaa akanicheki na kunipa ishara nimpe karatasi yake.
Nikapagawa nikamjibu nimechana na kutafuna.. daaah aliumia akakusanya karatas yake moja tu aloyomalizia maswali sijui manne ya section C.

Majibu ya mtihani yakatoka nimefauru jamaa amefeli ana Mswaki wa hesabu, me nna B.

Dah.. tumekuwa watu wazima sasa ila huwa ananikumbusha . Inaniumizaga sanaa
 
NDOA YAKO IKO MATATANI PIA
😆🙌
 
Nimewahi aisee tena cha mwanaJf... She was cool ila mimi nilijisikia vibaya sana
 
Cisco alikuwa ameniazima paperback novel ya Harold Robins,tulipokuwa shule.
Nikaikunjakunja sana Ile paperback.
Akasema,"What have you done to the book? Hiki kitabu ameniazima Chande"
Nikasema," Kitabu kitachakaa day after day,kwani kitakuwa kipya kila siku?"
Akasema,"Oh,ndio jibu lake rahisi? Kwamba kitabu lazima kichakae?"
 
Mimi jambo nililomuharibia rafiki yangu bado hajalisahau mpaka leo tumekuwa watu wazima,tukikutana huwa ananikumbushia.
Ilikuwa miaka ya 90 kwenye Mitihani ya Mock ya Kidato cha 2.
Tukiwa kwenye mtihani wa hesabu,yeye akiwa mbele yangu,nilimuomba anipatie mtihani wake nigelezee,maana mimi sikuwa vizuri kwenye hesabu.
Jamaa akanipatia kupitia chini ya kiti,baada ya msimamizi kuzubaa.

Bwana ndugu yenu nikacopy karatasi yote(ilikuwa karatasi ya kujibia zile plain).
Nilipomaliza nikajua ni rafu tu,kwahiyo sikumrudishia.

Baadae kidogo,msimamizi akatuamuru tusimame muda umeisha,kila mtu apange karatasi zake alizojibia na karatasi ya maswali ili yeye apite kuzibana.

Kwa hofu ya kuonekana nina karatasi nyingi,nikatafuna ile ya jamaa.

Sasa wakati msimamizi amekaribia kwa jamaa yangu,jamaa akanicheki na kunipa ishara nimpe karatasi yake.
Nikapagawa nikamjibu nimechana na kutafuna.. daaah aliumia akakusanya karatas yake moja tu aloyomalizia maswali sijui manne ya section C.

Majibu ya mtihani yakatoka nimefauru jamaa amefeli ana Mswaki wa hesabu, me nna B.

Dah.. tumekuwa watu wazima sasa ila huwa ananikumbusha . Inaniumizaga sanaa
😂😂😂Daah mwaneyu
 
Back
Top Bottom