'Nilivyokuona nikajihisi niko na mtu niliyemzoea. Sikujisikia kama niko na mtu nisiyemjua na kusema kweli najihisi furaha. Nadhani wewe ni rafiki yangu asilia na sihitaji kujieleza sana ili ujue kuwa mimi ni rafiki yako. Napenda kampani yako na nahisi hata wewe unaipenda kampani yangu. Nakukaribisha lunch leo na ukikubali nahisi hii itakuwa lunch special sana kwangu'......
Mtongozwa.... ..... .. Enhee, asante. Ila maneno yako kiboko.
Mtongozaji .... .... ... Achana na maneno, hayo yapo tuu, nitakupitia wakati naenda lunch.
Mtongozwa ..... .... Haya asante ..
Mtongozaji .. ... ... Sasa nitakupataje ofisini kwenu wapi? au nipe namba ya simu nitakupigia nitakuelekeza sehemu, uje.
........................
Mwanzoni unatakiwa uonyeshe ishara kuwa kuna kitu unataka, ila ghafla hamishia mazungumzo kwenye kitu kingine kitakacho fanya muwe karibu zaidi. Baadaye unakomelea msumari. Usiwe fasta sana, lakini vile vile usiwe longo longo sana. Unataka shoka we unaenda kuongea masaa matano. Wenzio wanakuwahi.
Amini usiamini huyo wa mazungumzo hayo hapo juu ilikuwa mara ya kwanza kuonana tena kwenye dala dala. Katika kipindi cha wiki mbili alishafungwa gori.
Ofcourse inategemeana na mwanamke. Kutongoza ni kitu natural na kwa kweli ukijaribu kanuni utashindwa kwa sababu wanawake wanatofautiana. Wapo wanaopenda longo longo, wapo wanaopenda moja kwa moja ila zingatia yafuatayo;
1/ Mwanzoni kabisa lazima uoneshe nia yako nini hasa (kufunga bao) na endelea kugonga mlango kila unapopata fursa.
2/ Ukiona anataka kuchomoa fasta, badilisha mazungumzo lete ishu nyingine kabisa
3/ Onesha kuwa unamjali, si kuwa unamtaka
4/ Usizidishe chochote. Hata kwenye mshiko onesha kuwa una limits
5/ Wiki moja kama hujaona mwelekeo ... chomoa, tafuta mwingine
6/ Usiogope kutongoza wanawake watatu, wanne, kabla ya kufanikiwa. Mwanaume umeumbwa ili utongoze. Usizame saana kabla hujapata!
7/ Kila unaposhindwa, chukua somo .. kwa nini hakuingia laini. rekebisha kitu unachohisi ulikosea
Mara nyingi kama ameingia laini, ukichomoa utaona yeye sasa anakufuatilia. Huo ndo wakati wa kutikisa nyavu. Ukichomoa na yeye asijali, ujue hapo sipo.
Ndani ya wiki moja lazima uwe na mwelekeo.