Vipi Utavunjwa Msikiti wa mwaka wa 1826 Kujenga Barabara?

Vipi Utavunjwa Msikiti wa mwaka wa 1826 Kujenga Barabara?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1727753792494.jpeg
 
Kama upo hapo kinyume cha sheria, uvunjwe tu. Lakini pia kama ni kwa ajili ya maslahi ya umma, uvunjwe, wapewe fidia wakajenge mbali na barabara kama yalivyo makanisa mengi ya RC
 
nahisi umeongea hivyo kutokana na muonekano wake. utakua uliboreshwa kwa kupakwa rangi
Uko sahihi. Lakini huo inaelekea umejengwa kwa matofali ( ya udongo au simenti). Na paa za asili katika maeneo hayo yalikuwa yanavuka kuta ili kulinda kuta na kutengeza vibaraza. Hili jengo sio la 1826.

Ila pamoja na kusema hivyo sioni umuhimu wa kuuvunja.

Amandla...
 
Ukiangalia style yake hauna zaidi ya miaka 100. Ujenzi wa aina hiyo haukuwepo nyakati zile katika eneo lile. Ujenzi ulikuwa wa fito na udongo na nyasi. Ila huu unaweza kuwa ni msikiti uliojengwa sehemu palipokuwepo msikiti wa 1826.

Amandla...
Bado haujanishawishi
Nyumba yako inawezekana ikawa na nyufa lakini yale mapiramidi kule Giza yapo strong hadi kesho....

Weka nukta hapo
 
Bado haujanishawishi
Nyumba yako inawezekana ikawa na nyufa lakini yale mapiramidi kule Giza yapo strong hadi kesho....

Weka nukta hapo
Msikiti wa Kizimkazi Dimbani ulijengwa kwa mara ya kwanza 1107 lakini sehemu kubwa iliyobaki ilijengwa karne ya 18. Ulijengwa kwa mawe na washirazi. Msikiti huo bado unatumika. Hapa tatizo ni kuwa katika eneo hilo hakuna historia ya majengo ya aina hii.

Mbalizi haimo katika njia zilizotumika na watumwa kiasi cha kufikiria kuwa utamaduni huo uliletwa na wageni. Nyumba za asili ziliendana na hali ya hewa ya eneo hilo ndio maana mapaa yake yalihakikisha kuta haziathiriki na mvua na watu waliweza kukaa kwenye hayo mabaraza wakati wa mvua.

Hili jengo tunalolizungumzia haliendani na utaalam huo. Hata hivyo inawezekana palikuwa na msikiti wa zamani katika eneo hilo na hili tunaloliona ni replacement yake.

Amandla...
 
Back
Top Bottom