Vipi Utavunjwa Msikiti wa mwaka wa 1826 Kujenga Barabara?

Vipi Utavunjwa Msikiti wa mwaka wa 1826 Kujenga Barabara?

Inapokuja swala la maendeleo then tunaangalia faida ipo wapi hatuangalii watu watajisikia vipi. Swala la maendeleo ni process ya kimantiki sio la kihisia.

Sawa ni jengo la kihistoria,je hiyo ina msaada gani kwa wanainchi eneo hilo,je ni wote wanalihitaji hilo jengo kwa shughuli zake?

Nadhani kudhania hilo jengo ni muhimu kuliko barabara itakuwa ni uzembe wa kufikiria na ni kukosa utashi wa kizalendo kwa taifa letu na ni aina ya ubinafsi wa kujifikiria faida au tija binafsi au kundi la wachache kwa hasara na mateso ya wengi.

Imagine wale watu waliokuwa wanakataa kubomoa nyumba zao,misikiti,makanisa,shule,frame na kadhalika hii barabara ya morogoro. Hivi magufuli angekuwa sio kauzu na mtata na kufanya maamuzi ya kiume kukaza njia isafishwe leo tungepata barabara ile za kisasa vile?🤔

Hebu tuwe wazalendo.
 
Huu msikiti uko Mbeya sehemu gani? Maana msikiti wa kwanza kujengwa Mbeya mjini ulijengwa mwaka 1992 akauzindua Rais Mwinyi pale Matola
Acha uongo,misikiti ilikuwepo kabla labda useme msikiti mkubwa na wenye hadhi kwa maana ya uzuri hata wa muonekano.
 
Upi huo uliokuwepo?
Binafsi niliwahi kufika mwanjelwa kabla ya mwaka huo uliotaja na mwenyeji wangu alikuwa akienda msikitini kuswali na mimi mwenyewe nimewahi kuswali swala ya eid el fitr tukuyu sehemu moja wanapaita Bagamoyo kabla 1992.
 
Binafsi niliwahi kufika mwanjelwa kabla ya mwaka huo uliotaja na mwenyeji wangu alikuwa akienda msikitini kuswali na mimi mwenyewe nimewahi kuswali swala ya eid el fitr tukuyu sehemu moja wanapaita Bagamoyo kabla 1992.
Sawa. Ila anaongelea Mbeya na ukisema Mbeya ni mjini siyo Tukuyu.
 
mwananchi_official
Siku moja baada ya Mwananchi kuchapicha habari kuhusu kuvunjwa kwa msikiti wenye miaka 198 huko Mbalizi, mkoano Mbeya, mkuu wa mkoa huo, Juma Homera amesema msikiti huo hautavunjwa, huku akitoa maelekezo kwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuangalia namna ya kuchepusha barabara hiyo.

Wakati Homera akitoa maelekezo hayo, wadau wengine wamejitokeza kutaka historia ya msikiti huo itunzwe, badala ya kubomolewa, kwani jengo la msikiti limekuwepo kabla ya kujengwa kwa barabara hiyo.

Msikiti huo uliodumu kwa miaka 198 tangu ulipojengwa mwaka 1826, umekuwa wa kihistoria na kivutio ambapo mbali na waumini kuutumia kwa ibada, umekuwa kumbukumbu na kuenzi kazi na mchango wa wazee wa zamani.

Akizungumza na Mwananchi leo Oktoba mosi, 2024, mkuu huyo wa mkoa, amesema katika kikao cha Kamati ya Usalama Mkoa iliyo chini yake, pamoja na mambo mengine, kimesitisha kuvunjwa kwa msikiti huo ili ubaki kama historia.

Amesema licha ya msikiti huo mkongwe kuwa katika eneo la hifadhi ya barabara, tayari Tanroads mkoani humo wameelekezwa kuwakwepa wananchi wa eneo hilo pamoja na msikiti huo.

Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
Wavunje hata hiyoo misikiti yote Tanzania ivunjwe dini ni upuuzi mtupu
 
Back
Top Bottom