Vipimo vipi vitathibitisha kuwa Figo zimefi

Habar wakuu nauliza ni vipimo vipi vyakupima ili kuthibitisha kuwa Figo zimefi

Figo kufeli ni ugonjwa, kwa hiyo kuna dalili zake ambazo mtu huona hata kabla ya vipimo.
Sijajua kama una tatizo hilo au unataka tu kujua vipimo.

Ukienda hospitalini baada ya kutoa maelezo (shida zako ) yako kwa daktari ambayo pengine huashiria tatizo la figo kufeli basi utafanyiwa vipimo vya damu, mkojo na ultrasound.

Katika vipimo vya damu utapimwa damu kwa ujumla wake (full blood picture, FBP) pamoja na viwango vya sumu ambazo hutolewa na figo mwilini (creatinine, blood urea) ili kujua hali ya utendaji kazi wa figo. Figo kufeli husababisha upungufu wa damu (anemia) pamoja na viwango vya juu sana vya sumu kwenye damu (creatinine, blood urea).

Kwenye mkojo wataangalia vitu mbalimbali ambavyo pia huashiria tatizo la figo kufeli mfano uwepo wa damu na protein kwenye mkojo nk

Ultrasound hutumika kuangalia muonekano na muundo wa figo nk. Mara nyingi figo lililofeli muonekano wake kwa ujumla hubadilika.

Kila la kheri.
 
Mkuu
 
Mungu apishilie mbali,nilisumbuliwaga na mawe kwenye figo baada ya kupima pale Rabbininsia hosp,
Wakati natumia dawa ya kuyalainisha yatoke kwa njia ya mkojo, basi kijiwe kimoja kikakwama katikati ya uume, mkojo unauma,kutoka hautoki, walahi siku iyo nilizunguka ndani,mara chooni nikiwa uchi wa mnyama uku navuja jasho,

Kijiwe kilikuja kutoka na chembe ndogo za damu juu, kwakweli maradhi ni mtihani
 
Hapana mkuu,
Hii ndiyo ya kwanza.
Mkuu nimetokea sana ku kubali the way unatoa maelezo hapo juu...

Hivo naomba uwe miongoni mwa watu nao watag kwenye issue mbali mbali ambazo zinahitaji michango ya afya..

Pia kama unaona kuna mpya yotote ambayo unaweza ku share na sisi kubusu figo unaweza anzisha hata uzi pia kule jukwaa la afya ili kusoma na kupitia.

Ni hayo tuu mkuu...
Ila kwa hyo maelezo uliyoto daaah upo vzr boss
 
Ahsante sana mkuu, ndiyo kazi yangu.

Wala usiogope kuni tag, nitafurahi sana kwa sababu nipo kwa ajili hiyo.
 
Figo kufeli ni ugonjwa, kwa hiyo kuna dalili zake ambazo mtu huona hata kabla ya vipimo.
Sijajua kama una tatizo hilo au unataka tu kujua vipimo.

Ukienda hospitalini baada ya kutoa maelezo (shida zako ) yako kwa daktari ambayo pengine huashiria tatizo la figo kufeli basi utafanyiwa vipimo vya damu, mkojo na ultrasound.

Katika vipimo vya damu utapimwa damu kwa ujumla wake (full blood picture, FBP) pamoja na viwango vya sumu ambazo hutolewa na figo mwilini (creatinine, blood urea) ili kujua hali ya utendaji kazi wa figo. Figo kufeli husababisha upungufu wa damu (anemia) pamoja na viwango vya juu sana vya sumu kwenye damu (creatinine, blood urea).

Kwenye mkojo wataangalia vitu mbalimbali ambavyo pia huashiria tatizo la figo kufeli mfano uwepo wa damu na protein kwenye mkojo nk

Ultrasound hutumika kuangalia muonekano na muundo wa figo nk. Mara nyingi figo lililofeli muonekano wake kwa ujumla hubadilika.

Kila la kheri.
Je mtu creatinine na blood urea vikawa sawa pia Kuna uwezekano Figo zikawa zimefeli na Hali hizo blood urea na creatinine ziko sawa
 
Mungu apishilie mbali,nilisumbuliwaga na mawe kwenye figo baada ya kupima pale Rabbininsia hosp,
Wakati natumia dawa ya kuyalainisha yatoke kwa njia ya mkojo, basi kijiwe kimoja kikakwama katikati ya uume, mkojo unauma,kutoka hautoki, walahi siku iyo nilizunguka ndani,mara chooni nikiwa uchi wa mnyama uku navuja jasho,

Kijiwe kilikuja kutoka na chembe ndogo za damu juu, kwakweli maradhi ni mtihani
Ulipata dalili Gani za mawe kwenye figo
 
Je mtu creatinine na blood urea vikawa sawa pia Kuna uwezekano Figo zikawa zimefeli na Hali hizo blood urea na creatinine ziko sawa

Ndiyo, inawezekana kabisa hiyo hali kutokea.

Hizo sumu (blood urea na creatinine) zinaweza zikapimwa na kuwa sawa lakini tayari figo imefeli. Hii hutokea tu katika hatua za mwanzo kabisa za figo kufeli na kadri uharibifu/ugonjwa unavyoendelea ndivyo viwango vyake hupanda juu kwenye damu.

Mpaka viwango vya urea na creatinine zinapanda walau mara mbili ya kiwango kinachotakiwa kwenye damu uharibifu kwenye figo (figo kufeli) utakuwa umefikia asilimia 50. (50%).
 
[/QUOTEnini kinasababisha kufeli Sasa nahali blood urea na creatinine ziko sawa..
 
Ndiyo, inawezekana kabisa hiyo hali kutokea.

Hizo sumu (blood urea na creatinine) zinaweza zikapimwa na kuwa sawa lakini tayari figo imefeli. Hii hutokea tu katika hatua za mwanzo kabisa za figo kufeli na kadri uharibifu/ugonjwa unavyoendelea ndivyo viwango vyake hupanda juu kwenye damu.

Mpaka viwango vya urea na creatinine zinapanda walau mara mbili ya kiwango kinachotakiwa kwenye damu uharibifu kwenye figo (figo kufeli) utakuwa umefikia asilimia 50. (50%).
Nin kinafanya zifeli Hali creatinine na urea viko sawa
 
Figo kufeli ni ugonjwa ambao huanza taratibu na kuendelea kuharibu figo kidogo kidogo mpaka linashindwa kabisa kufanya kazi yake ya kuchuja damu na kuondoa sumu mwilini.

Katika ugonjwa huu kinachoathiriwa au kuharibiwa ni vichujio vya figo (glomerular capsule filters). Uharibifu huo hutokea taratibu mpaka vichujio vyote vinapoharibika kabisa.

Figo kufeli haitegemei tu kipimo kimoja ili kuthibitisha. Kwanza huwa kuna dalili ambazo mtu huwa nazo, pili kunakuwa na visababishi (risk factors). Halafu kuna vipimo vya damu, mkojo na ultrasound ambavyo hufanyika ili kuweza kufikia hitimisho.

Blood urea na creatinine vinakuwa sawa tu wakati figo kufeli ndiyo inaanza (ikiwa katika hatua za mwanzo kabisa: early stages).

Katika hatua za mwanzo kabisa sehemu ya figo ambayo bado haijaathiriwa na ugonjwa hufanya kazi mara dufu kuondoa (compensatory mechanism) hizo sumu (creatinine na urea) kwa hiyo mwanzoni mwa ugonjwa huo creatinine na urea zinaweza kuwa sawa tu lakini kadri ugonjwa unavyoendelea ndivyo figo zinashindwa kufanya kazi kabisa.
 
Utajuaje Figo imeanza kufeli taratibu taratibu Hali yakuwa vitu vingine viko sawa kama blood urea,creatinine ....naumesema Figo kufeli haitegemea kipimo kimoja labda hivo vipimo vingine ni vipi hivo
 
Mkuu jaribu kusoma tena kwa umakini nilichoandika.

Nimesema figo kufeli cha kwanza kuna dalili ambazo mgonjwa hupata.

Vipimo vingine ni vipimo vya mkojo na ultrasound,,,vyote lazima vifanyike.

Figo kufeli huwa na hatua ambapo kwenye hatua za mwanzo kabisa (early stages) creatinine na urea zinaweza kuwa sawa (kwa sababu ya kazi kubwa inayofanywa na sehemu ya figo ambayo bado haijaathirika, compensatory mechanism).

Creatinine na urea kuwa sawa hakuondoi tatizo la figo kufeli wakati mtu tayari ana dalili na pengine hivyo vipimo vingine vimeonesha viashiria vya figo kufeli.

Kwa hiyo vitu vyote dalili ambazo mgonjwa hupata pamoja na vipimo (vya damu, mkojo na ultrasound) hutumika kufikia hitimisho kwamba figo zimefeli. Kama vipimo vyote vipo sawa basi tatizo la figo kufeli halipo.
 
Back
Top Bottom