BS na MRDTHabar wakuu nauliza ni vipimo vipi vyakupima ili kuthibitisha kuwa Figo zimefi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
BS na MRDTHabar wakuu nauliza ni vipimo vipi vyakupima ili kuthibitisha kuwa Figo zimefi
Moja ya mambo mhimu ya kuzingatia ni:Nin kinafanya zifeli Hali creatinine na urea viko sawa
Hili tatizo linakua kubwa sana kadiri siku zinavyosogea.... Tunaomba wahusika watupatie elimu zaidi...Figo kufeli ni ugonjwa, kwa hiyo kuna dalili zake ambazo mtu huona hata kabla ya vipimo.
Sijajua kama una tatizo hilo au unataka tu kujua vipimo.
Ukienda hospitalini baada ya kutoa maelezo (shida zako ) yako kwa daktari ambayo pengine huashiria tatizo la figo kufeli basi utafanyiwa vipimo vya damu, mkojo na ultrasound.
Katika vipimo vya damu utapimwa damu kwa ujumla wake (full blood picture, FBP) pamoja na viwango vya sumu ambazo hutolewa na figo mwilini (creatinine, blood urea) ili kujua hali ya utendaji kazi wa figo. Figo kufeli husababisha upungufu wa damu (anemia) pamoja na viwango vya juu sana vya sumu kwenye damu (creatinine, blood urea).
Kwenye mkojo wataangalia vitu mbalimbali ambavyo pia huashiria tatizo la figo kufeli mfano uwepo wa damu na protein kwenye mkojo nk
Ultrasound hutumika kuangalia muonekano na muundo wa figo nk. Mara nyingi figo lililofeli muonekano wake kwa ujumla hubadilika.
Kila la kheri.
Hili tatizo linakua kubwa sana kadiri siku zinavyosogea.... Tunaomba wahusika watupatie elimu zaidi...Moja ya mambo mhimu ya kuzingatia ni:
1: Vipimo hupimwa baada ya kuchukua historia ya mgonjwa/mpimwaji.
2: Historia ya mgonjwa huusisha mwenendo wa maisha ya mgonjwa/mpimwaji na mienendo yake ya kimaisha pia.
3: Utendaji kazi wa figo hutathiminiwa kwa kuangalia kazi za msingi za figo.
Pia, mwili huweza kuziba pengo kabla ya dalili/compasation. Ukija mapema unaweza kukuta mwili unaendele na utaratibu wa kufidia tofauti zilizojitokeza.
4: Vinavyopimwa kama utendaji kazi wa figo: madini, creatinine, urea na kiasi cha damu kwa kutaja vichache huweza kuathiriwa na vitu vingine nje ya figo yenyewe. Hivyo, tathimini nzuri ya mtoa huduma huitajika kabla ya kutoa jibu la mwisho.
5: Vitu vya nje ya figo vinaweza kusababisha vinavyopimwa kwenda juu au chini ya kiwango hivyo huwezi kurushia tatizo kuwa ni figo mpaka uwe una uhakika kuwa inahusika kwa mjumuisho sahihi. Kama ilivyoelezwa hapo juu.
6: Hivyo, wakati mwingine tunahitajika kupima kilichopo mwilini na kile ambacho figo inatoa ili ujue shida iko wapi. Matatizo nje ya figo vs figo yenyewe?
Mfano:
Creatinine inayopimwa ni zao la kuvunjwa kwa misuli/nyama ambayo ni utaratibu ndani ya mwili wa seli kufa. Unaweza kukuta creatinine iko juu kwenye figo kwa sababu mtu anafanya mazoezi makali au anatumia nyama kwa wingi sana vitu ambavyo huongeza taka mwili husika kwa kiasi kikubwa. Na hivyo, kuzalisha taka mwili kwa wingi ambapo huzidi uwezo halisi wa utendaji kazi wa figo. Ukipima kwenye mkojo kwa kipindi husika unaweza kukuta creatinine inayotolewa kwenye mkojo/iliyotolewa inaonyesha kuwa kwenye kiasi kinachotakiwa basi figo husika inaendelea kufanya kazi vyema kwa kutoa kiasi kinachotakiwa. Bali mlundikano unatokana na wingi wa taka mwili zilizozalishwa.
Au unakuta creatinine nyingi kwa sababu mtu hanywi maji ya kutosha hivyo yuko na kiasi kidogo cha maji/dehydration au anaharisha au kutapika.
Pia, unaweza kuwa na kiasi cha creatinine kidogo kuliko inavyotarajiwa kama mtu amepoteza kiasi kikubwa cha misuli ya mwili wake/hana misuli ya kutosha kama kwa wazee au mtu aliyekonda sana. Hapo huwezi kusema figo ziko vyema sana, kwani kuna uwezekano uchafu unaokuja ni kidogo sana kutoka kwenye misuli husika.
NB: Huwezi kumlaumu mtupa taka bila kuangalia wazalisha taka kwa upande wao au kama mpeleka taka kafikisha dampo kiasi mlichokubaliana kukipeleka kwa muda husika na kusema hatimizi wajibu.