Vipimo vya COVID19: Dr. Mwele na Dr. John Nkengasong(Africa CDC) walitumika kupotosha ukweli wa kisayansi (wasaka tonge kazini)

Nilichogundua hapo ni kuwa wapambe wa Kayafa walioelekezwa wachukue sampuli hawakuwa na ujuzi wowote wa kuchukua sampuli kwa ajili ya vipimo vya Covid-19...!!
Na hii inadhihirisha kuwa baadhi yao walikuwa na maambukizi ya Covid-19 na wali-contaminate sampuli walizochukua...!!
 
Kwanza kabisa naomba nianze kwa kudeclare “interest" kwenye suala ya Covid-19. Mimi ni mtafiti kwenye utengenezaji wa madawa haswa kwa kutumia "Computer Aided Drug Design (CADD)". Tangu janga hili la Covid-19 lianze, tumejikita kwenye kutafuta dawa itakayoweza kutibu Covid-19 kama ilivyo kwa wenzutu walioko maabara kote duniani.

Tukirudi kwenye mada; tokoa Mh. Rais John Pombe Magufuli alivyotoa matokeo ya unchunguzi dhidi ya ubora wa vifaa vinavyotumika kupima sampuli za corona, kumekwepo upotoshwaji wa makusudi dhidi ya hatua aliyochukua Mh. Rais. Kundi kubwa la watu wanadangwa mchana kweupe na watu wenye nia ovu dhidi ya usalama wa nchi, na taifa kwa ujumla.

Imekuwa kawaida ya kujkwa hili kushiriki upotoshwaji huu kwa kuleta makala ya watu wanaotumikia matumbo kupotosha ukweli na kuteka mjadala wa Covid-19.. Hivi karibuni, katika kupambana na ukweli Mh. Rais tumemsikia Dr. Mwele kupitia mtandao wa twitter akidhihaki hatua aliochukua Mh. Rais. Kama ni kweli twitter ile ilikuwa ya kwake basi nikiri wazi anauwezo mdogo sana kwenye sayansi ya upimaji.

Dkt. Mwele: Kipimo ulichokicalibrate kwa ajili ya COVID kitapima COVID ukiingiza sampuli ambazo siyo umeivuruga! Majibu yatakuwa hayana mantiki! - JamiiForums

Baada ya hapo kundi hilo likaja na hoja ya nyota ya Dr. Nyambura wakijaribu kuonyesha kwamba kasimamishwa kimakosa.

Nyota ya Dr Nyambura Moremi itang'aa Kimataifa - JamiiForums

Khali khadhalika, kwa kudhalalisha jukwa hili, kundi hili ovu likaja na hoja ya Dr. John Nkengasong wa (Africa CDC), wakishadadia maelezo yasio na “substance”kutoka kwa huyu mtalaam anaetumikia tumbo lake. Nikiri tena wazi, kama sio utumwa kwa mwajiri wake, basi mtalaam huyu atakuwa na shida mahali.

CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri - JamiiForums

Kwa heshima na taadhima, naleta kwenu maelezo ya kitaalam juu ya upimaji wa virusi vya corona kutoka kwa Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nikiri wazi kwamba simjui Dr. Ally wala sijawahi kumuona.

Hata wapotoshe, Kutakucha tu!

Tukiwa tupo kwenye taharuki juu ya kipimo cha corona (covid-19) hapa nchini, baada kutoa majibu ya positive kwa mbuzi na papai, naomba nitoe maoni yangu kama mdau katika tansia hii ya vitendanishi vya maabara (diagnostics).

Nianze kwa kutangaza maslahi yangu binafsi kwenye mada husika. Mimi ni mtafiti kwenye eneo hili la vitendanishi (Medical and clinical diagnostics). Tasnifu (thesis) yangu ya umahiri (MSc in Biotechnolgy) iljikita kwenye kutengeneza njia (method) ya kutambua kwa haraka na wepesi uwepo wa protini zinazoashiria uwepo wa saratani kwa binaadamu. Ama tasnifu yangu ya uzamivu (PhD in (Bio) Engineering) ilijikita kwenye kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajili ya kutendanisha vimelea vya maradhi (bacteria) kwa binaadamu. Tafiti zote zikiwa zimefanyika chuo kikuu cha Lund, Sweden. Kwa sasa tunaendelea na utafiti wa kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajilia ya kutendanisha kirusi kinacho shambulia simba na mbwa, kwa ufadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Pia kwa kutambua umuhimu wa kuwa na kitedanishi kinachoweza kutoa majibu haraka lakini pia kutumika nje ya maabara (rapid test strip) kwa ajili covid-19, tumetuma ‘concept note’ kwa mamlaka husika hapa Tanzania ili tuweze kuungwa mkono kwenye kutengeneza ‘rapid test’ itakayoweza kutendanisha mgonjwa covid-19 na asiye mgonjwa. Tungali tunasubiria mrejesho!

Tukirudi kwenye mada kuu, kwanza nitoe pongezi kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa uwamuzi wake wa kuamua kujiongeza ili kujiridhisha kama ni kweli Maabara yetu ya Taifa (NHL) inatoa majibu sahihi au la! Ni uamuzi sahihi na wakiuongozi!

Maswali tunayojiuliza: Jee njia zilizotumika (kupeleka sampuli (swab) za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu? Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini? Ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalam ndio tatizo? Au vyote? Kabla sijajibu maswali haya kwanza nianze kwa kuelezea jinsi covid-19 inavyopimwa:

Mpaka sasa kuna vipimo (vitendanishi) vya aina kuu mbili vinavyotumika kupima covid-19. Aina ya kwanza ni kile kinacho pima covid-19 kwa kuangalia uwepo wa kinasaba cha kirusi chenyewe (RNA). Kipimo hiki hujulikana kama ‘Real-time Reverse Transcription Polymerase Chain Reaction’ (RT-qPCR) au al-maarufu PCR! Hichi ndo kipimo mashuhuri na ‘standard’ kinachotumika ulimwenguni kwa sasa. Sampuli zake huchukuliwa kwa kurambisha (swab) kijiti cha pamba (cotton swab) ndani-nyuma ya pua (nasophyaryngeal swab) na/au ndani-nyuma ya mdomo (oropharyngeal swab).

Aina ya pili ni ile inayopima kwa kuangalia kinga (antibody) inayozalishwa na muathirika pindi anapopata maambukizi ya kirusi cha corona. Kipimo hichi hujulikana kama ‘Immune Rapid Test, na vipo vya aina tofauti. Aina maarufu kwa sasa ni ya ‘strip’, kama ile strip inayopima ujauzito kwenye mkojo (UPT strip) – aina hii hujulikana kama “Lateral flow immunochromatographic assays” au lateral flow test! Kipimo cha aina hii sampuli yake ni damu inayochukuliwa kwenye kidole (finger prick) au kwenye mkono (venepuncture). Kipimo hichi kwa sasa sio standard ila kuna kampuni mbali mbali duniania zinazalisha na zimepata vibali vya dharura kutoka FDA (USA) na mamlaka nyengine duniani kuingiza kwenye matumizi.

Kwa maelezo hayo bila shaka Maabara yetu ya Taifa huchakata sampuli za covid-19 kwa kutumia kitendanishi ambacho ni standard – PCR. Kitendanishi ambacho sampuli zake huchukuliwa ‘swab’ ya puani/ mdomoni! Sio mate, mkojo, damu wala kinyesi kama wengine wanavyo hoji!

Jee njia zilizotumiwa (kupeleka sampuli za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu?

Kuna wanaosema kitendanishi ukisha ki-calibrate kwa ajili ya sampuli flani ukipeleka sampuli tofauti majibu yanakuwa haya maana! Hivyo kwa sababu PCR hii ya covid-19 ilikuwa calibrated kwa ajili ya sampuli za swab ya pua na mdomo wa binaadamu kupeleka swab ya papai au mbuzi inafanya majibu ya kipimo yasiwe na maana! Kukubaliana au kupingana na hoja hii kwanza ni vyema kuelewa japo kwa muhtasari covid-19 ina pimwaje kwa PCR!

1.Sampuli ile, pamba (swab), hupokelewa maabara na kuandikishwa (registered) taarifa muhimu kama vile: taarifa za aliekusanya sampuli, taarifa za alieleta sampuli maabara, taafira za aina ya sampuli (swab ya pua au mdomo), taarifa za aliechukuliwa sampuli n.k.

2. Sampuli hiyo (pamba) hupitishwa hatua tofauti kwa kutumia kitenganishi maalum cha kinasaba cha RNA, kwa jina la kitaalamu ni ‘Viral RNA Extraction Kit’: kama vile, kuosha pamba hiyo (kuondoa kirusi kwenye pamba kiwe kwenye tube), kukipasua kirusi (lysis) ili kutoa kinasaba (RNA) ndani ya kirusi, na mwisho ni kusafisha (purification) ili kubaki na kinasaba cha kirusi tu. Kabla ya kupeleka kwenye PCR, kinasaba (RNA) hicho kilichosafishwa huangaliwa ubora wake (quality)! Ubora wake huhusisha wingi (concentration) na usafi (purity). Kuna kiasi na usafi maalumu ambao kama sampuli haijafikisha hutakiwi kuendelea nayo kwa hatua ya PCR, maana ni ubora usiofaa kwa kutoa majibu sahihi! Kifaa kinachotumika kupima ubora wa kinasaba (RNA) ni ‘spectrophotometer’ - modo maarufu ni ‘Nanodrop’. Sampuli (extracted RNA) ikikidhi vigezo (quality) ya kuendelea kwenye PCR, hupelekwa kwa ajili ya kusomwa ili ijulikane ni kinasaba cha kirusi kinachosababisha covid-19 au la!

3. PCR, hutendanisha kinasaba (RNA) kwanza kwa kukigeuza kutoka RNA kwenda DNA, kisha hutoa kopi nyingi (amplification) kwa kulenga maeneo mawili maalumu ya kinasaba, maeneo ambayo humtofautisha kinasaba cha corona anaesabisha covid-19 na kinasaba cha kirusi chengine chochote hata vile vya jamii moja na yeye, kama virusi vinavyoosababisha MERS na SARS. Kukopika kwa maeneo haya muhimu husomeka moja moja kwenye mashine hii ya PCR na ikifika kiwango kinachokubalika - mashine husoma-positive. Kama kopi itakuwa ni ya eneo moja tu kati ya hayo mawili mashine husoma – indeterminate (inconclusive), na kama hakuna kopi ya eneo hata moja- mashine husoma negative. Kwa majibu ya inconclusive maana yake kunahitajika sampuli nyengine kurudia kipimo.

Muhimu: Sampuli ya mgonjwa mara zote husomwa pamoja na sampuli za kukontroli (control samples) kwa ajili ya kuhakikisha kama PCR (mashine) inafanyakazi sawa sawa. Sampuli za kontroli hizi ni sehemu ya kinasaba cha kirusi cha covid-19 ambacho hutumika kama positive kontrol na maji maalum (buffer) yenye kila kilichowekwa kwenye sampuli halisi isipokuwa kinasaba (RNA) ambayo hutumika kama negative kontrol. Hivyo majibu hayo hapo juu hukubalika tu endapo postivive control itasoma positive na negative control ikisoma negative.

Kwa kuangalia hatua hizo, utaona kwamba kinachokwenda kwenye mashine ya PCR si mate wala makamasi, ni kinasaba (RNA) safi (purified RNA), haijalishi kimetolewa wapi! Lakini pia ile ‘Viral RNA Extraction Kit’ imetengenezwa kutenganisha na kusafisha kinasaba (RNA) cha kirusi kutoka specimen yoyote, iwe binaadamu, papai, mbuzi, bata, udongo n.k, kama swab ya hiyo specimen (mfano mbuzi) ina kirusi cha RNA basi RNA ya hicho kirusi itapatikana tu. Hivyo basi sampuli zilizopelekwa zilikuwa sahihi na hazileti mkanganyiko wowote kwenye mashine ya PCR wala kwenye extraction kit.

Lakini, jee kulikuwa na njia nyengine ya kujua ubora wa kifaa na wataalam husika?

Ndio! Kwenye utendaji kazi wa maabara, ili maabra kujiridhisha na majibu inayotoa, huwa inashirikisha maabara nyengine kupata majibu ya sampuli hiyo hiyo kulinganisha majibu yake, kitaalam inaitwa Inter-Laboratory Comparisons (ILC). Hivyo badala ya kupeleka sampuli ya papai au mbuzi kwenye maabara yetu ya taifa, tungetuma sampuli za baadhi ya waloambiwa positive na wale waloambiwa negative (na maabara yetu) kwenye maabara za nchi jirani kisha tukalinganisha majibu yao na ya kwetu!

Kwanini PCR kiwe kitendanishi standard cha covid-19?

PCR ina sifa mbili bora na muhimu za kipimo cha kimaabara zinazofanya kitendanishi hiki kiwe ndio standard:

1.‘High Sensitivity’: (a) ‘High analytical sensitivity’ (uwezo kusoma hata kiwango kidogo cha virusi) kwa maana hata kukiwepo na uzi mmoja tu wa kinasaba (single RNA strand) basi PCR inaweza kutendanisha! (b) ‘High clinical sensitivity’ (>95%), kwamaana kama kuna watu 100 wenye covid-19 (positive), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya positive kwa watu wasiopungua 95 miongoni mwa hao 100! Ijulikane, mpaka sasa hakuna kitendanishi chenye clinical sensitivity ya 100%!

2. ‘High Specificity/Selectivity’: (a) ‘High analytical specificity’ kwa maana ina kopi maeneo mawili ya kinasaba, maeneo ambayo ni maalumu kwa nCov tu, hivyo hata kirusi cha familia moja na nCov hakiwezi kusomwa (haichanganyi), achilia mbali wale wa mbali kama HIV na wengine. (b) High clinical Specificity (99%), kwa maana kama watakuja watu 100 ambao hawana covid-19 (negative), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya negative kwa watu 99 miongoni mwa hao 100! Hivyo PCR ikisoma positive ujuwe ni positive kweli!

Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini (ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalamu ndio tatizo au vyote?

Kwanza kabisa niseme kwamba kirusi hichi, SARS-CoV-2 au nCov, kinachosababisha ugonjwa wa corona (Covid-19), bado ni kipya, wanasayansi ndo kwanza wanajaribu kukielewa! Bado kila kukicha wanagundua kitu kipya juu ya kirusi hiki, kuanzia uwepo wake kwenye viumbe mbali mbali, uwepo wake sehemu mbali mbali za miili yetu, anavyojibadilisha (mutation), ushambuliaji wake, na hata hatari yake yakusababisha vifo. Ila kwa maarifa yaliyopo mpaka naandika makala hii kirusi hichi hakijaonekana kwenye sampuli zote zote katika hizi zilizopelekwa kwenye maabara yetu ya taifa (papai, mbuzi, n.k). Hivyo basi tulitegemea majibu yawe negative! Kuna sababu nyingi, moja au mchanganyiko zinazoweka kuwa zimepelekea majibu ya covid-19 positive kwa mbuzi na papai! Lakini katika sababu zote hizi, iwayo yoyote huwezi kuwaondoa kwenye mashaka wataalamu walopima sampuli hizi.

1. Inaweza kuwa ni ‘contamination’ wakati wa kuchukuwa sampuli, huenda mchukuaji hakuwa na ujuzi wa kuchukuwa sampuli, kupelekea ku-contaminate sampuli kwa namna moja au nyengine yoyote ile! Hivyo kimsingi alieonekana kuwa na covid-19 positive si mbuzi au papai bali ni mchukuwaji wa sampuli.

2. Au ‘contamination’ wakati wa kusafirisha na ku-process sampuli (extraction and purification) pale maabara kabla ya kupeleka kwenye PCR mashine! Hivyo sample ika pass kwenye Nanodrop na PCR ikasoma positive! Kimsingi positive sio papai wala mbuzi bali alie process sampuli maabara au msafirishaji wa sampuli!

3. Au ‘contamination’ wakati wa kuandaa sampuli kwa ajili ya PCR, huenda kwa bahati mbaya sampuli ya positive Kontrol iliingia bila kujua kwenye sampuli ya papai au mbuzi! Hivyo majibu yakasoma positive!

Kama ni moja katika hayo au yote basi kunatatizo la kiujuzi (lack of competence) katika kuchukuwa, ku-handle na ku-process sampuli. Hata kama aliechukuwa sampuli sio sehemu ya wataalamu wa maabara ya taifa, basi kuna tatizo katika kupokea sampuli (ambayo ni sehemu ya handling ya sampuli). Sampuli lazima zipokelewe kutoka kwa watu maalumu walopewa kazi hiyo wakiwa na ujuzi uliothibitishwa wa kufanya kazi hiyo! Sio kila mtu tu.

4. Jee vipi kama kitendanishi (PCR) ndio bomu? Ni kweli mashine inaweza kuwa imeharibika au ni kimeo kimeletwa kwa makusudi na "mabeberu", na wala hakukuwa na ‘contamination’ popote ila tu mashine inasema uwongo.

Kama ni hivyo, basi walitakiwa wao wataalamu wa maabara waling’amuwe hilo kabla ya mkuu wanchi kutilia mashaka na kuamua kuhakiki kwa njia zake. Utaratibu wa upimaji wa covid-19 kwa PCR (Standard Operating Procedure (SOP)) na utendaji kazi nzuri wa maabara (Good Laboratory Practice (GLP)) kama vitafuatwa ipasavyo vinawapa nafasi kwa wataalamu wa maabara kujua makosa/ubovu wa kifaa kabla yakukitumia na hata ubora wa sampuli kabla ya kuipima. Na hata baada ya kupelekewa sampuli za papai au mbuzi (sampuli ambao hazina nCov), utaratibu hapo juu unawawezesha kujua kwamba hii sampuli haifai hata kwenda kwenye PCR kwa kuangalia tu quality ya RNA (kinasaba) kwenye Nanodrop! Ila haiyondoi uwezekano kwamba kwenye papai au mbuzi kunaweza kuwa na kirusi chengine (RNA virus) na hivyo ukapata quality RNA kwenye Nanodrop! Lakini bado wangeweza kujua kwa kulinganisha majibu ya PCR ya sampuli ya negative kontrol na sampuli husika! Kama sampuli ya negative kontrol nayo inasoma positive, basi mashine ina matatizo!

5.Au jee wataalam wetu walizidiwa na wingi wa sampuli, wakachoka, ikawa badala ya kupima sampuli zote, wakaamua kucheza mchezo wa ‘ana- ana-do”, hii positive, hii negative, hii positive, hii negative…Sidhani, wala sifikirii kwamba wataalamu wetu walojitolea mstari wa mbele kupigana vita kwa ajili yetu dhidi ya corona eti wafanye hivyo! La hasha! Na kama itakuwa hivyo basi tatizo ni kubwa sana!

Mwisho siku haya yoote ni nadharia kwenye kitendawili cha kipimo cha covid-19 hapa nchini, kitendawili ambacho TUME iliyoundwa na waziri wa afya tutegemee italeta majibu sahihi ili waTanzania turudishe imani kwa majibu tunayopata! Kwa hakika jua litachomoza tena, kutakucha!

Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, UDSM

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Niwaombe viongozi wa Jamii Forum kupunguza mada zinazookana wazi kupotosha ukweli wa kisayansi ili kuwaokoa hawa wasaka tonge.

Ahsantenii
Makala yako ingependeza kama ungekuwa objective. Tupe facts bila kupiga vijembe kwa watu wengine kama kwamba wewe ni "I know it all'. Hatuna shida na maneno yako ya shombo eti "wasaka tonge"! Wewe unasala nini sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyesoma anipe summary kwa sentensi moja tu.
Huyu pamoja na usomi wake uchwara, hitimisho lake ni kuwa kwanini wataalamu wa maabara walishindwa kujua sampling iliyoletwa siyo ya binadamu,

hana hoja ya maana kuthibitisha kuwa vipimo halali vya binadamu vilivyotangungulia kupimwa kabla ya papai vilikuwa vinamakosa
 
Bomboclaat...mleta mada Unataka kupotosha

Anayoyasema Huyu msomi yalikwishasemwa, imemchukua wiki 2 kuandika maoni yake kwa sababu alihitaji kudesa waliyoyasema akina Dr.Mwele

Anyway, Uzuri mtaalam amekiri kwamba anaomba "Kazi" kwa Jiwe
 
Oil chafu nayo ilitoa RNA? Yes, indeterminate (pronounce please!!!)
 
Hahaha, mnatupa shida sana kuamini kama kweli nyie ni binadamu, kwa taarifa yako furaha yangu kubwa ni kuchangia kwenye upatikanaji wa dawa na sio ajira. Kama kazi tayari ipo yenye uhakika. Ahsante
 
Nimesoma kila kitu alichokiandika, na haya ndio ninaweza kueleza.

-Msingi wa ulichokiandika umekosa mantiki, maana umeeleza mambo mengi kiujumla na kwa kina, huku ukishindwa kueleza ni Vipi wakina Mwele Malecela na CDC wamepotosha. Maelezo ya Mwele yalikuwa yakiujumla, mafupi, yenye kueleweka moja kwa moja na hayakuwa mahsusi dhidi ya Mheshimiwa Rais (Tafsiri zetu zilielewa wazi Mwele alikuwa akijibu Shutuma za Mheshimiwa Rais kwa kusema madai ya Rais hayakuwa na mantiki yoyote ya kisayansi) na CDC walitetea ubora wa vipimo vya kimaabara unaotumika kupima COVID hapa Tanzania kuwa ni sahihi na ndio standard za dunia nzima. (Kimsingi CDC walikuwa wanalinda taarifa za maumbukizi yaliyotokana na majibu ya maabara hapa duniani dhidi ya upotoshaji uliokuwa umeanza kuzagaa duniani ambapo ulichochewa na kauli ya Mheshimiwa Rais)

-Mleta umeshindwa kabisa kuonyesha mapungufu ya kauli ya Magufuli, ambapo kitaalamu unajua kabisa matamshi ya Magufuli yalikuwa ni upotoshaji wa kiwango cha SGR. (Kwanini? Uwezi kupima ubora wa vipimo vya maabara kwa kutumia sampuli isiyo sahihi (wrong specimen) na kamwe huwezi kutafsiri majibu ya maabara yaliyotokana na sampuli isiyo sahihi. Wrong specimen=Wrong test=Wrong result=Unexplainable science)

Mwisho kabisa mleta mada nimeona kama unatafuta ajira ya kuteuliwa ili kushika nafasi katika maabara kuu ya Taifa mara baada ya aliyepo sasa kusimamishwa au nafasi ya bure bure kutoka kwa mheshimiwa Rais. Sijaona mantiki ya wewe kujieleza ulivyo, kutoa wasifu wako, ulichosomea, wapi ulisomea, ulisomea nini nk. Huo ni utoto sana kwa msomi.
Yote kwa yote sote tunajua mheshimiwa yuko desperate kwa sababu ya sakata la COVID hivyo anaweza kuokota mtu yoyote yule mwenye kuonyesha uwezo wa kumcover katika hili, hivyo unaweza kuvuna chochote. Hivyo usisahau pia kuweka na kadi yako CCM mtandaoni kama unayo ili mheshimiwa ajue wewe ni kada mwaminifu ama sio.
 
Oil chafu nayo ilitoa RNA? Yes, indeterminate (pronounce please!!!)
Ndio hapo sasa, Mwele na wenzake hawakujua test kits zinatumi RNA na sio vinginevyo. Wataalam wakashinda hata kujua oild kwa macho. Kimsingi, hawa wote ni wahujumu afya.Unaweza kuendelea kumuamini ili kutimiza hamu yako. Ahsante
 
Ulimwengu umejaa wajinga sana hawahitaji kufikiri.
Hata ungeandika kwa utalaam gani kama hautakuwa aganist na serkali iliyopo madarakani hutapata support.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serlikali yenyewe inajicontradict, maabara ni ya serikali wataalamu ni waajiliwa wa serikali, vifaa kama ni vibovu vimenunuliwa na serekali,
Labda useme wachangiaji wako against upotoshaji wa magu
 
Nimesoma kila kitu alichokiandika, na haya ndio ninaweza kueleza.

-Msingi wa ulichokiandika umekosa mantiki, maana umeeleza mambo mengi kiujumla na kwa kina, huku ukishindwa kueleza ni Vipi wakina Mwele Malecela na CDC wamepotosha. Maelezo ya Mwele yalikuwa yakiujumla, mafupi, yenye kueleweka moja kwa moja na hayakuwa mahsusi dhidi ya Mheshimiwa Rais (Tafsiri zetu zilielewa wazi Mwele alikuwa akijibu Shutuma za Mheshimiwa Rais kwa kusema madai ya Rais hayakuwa na mantiki yoyote ya kisayansi) na CDC walitetea ubora wa vipimo vya kimaabara unaotumika kupima COVID hapa Tanzania kuwa ni sahihi na ndio standard za dunia nzima. (Kimsingi CDC walikuwa wanalinda taarifa za maumbukizi yaliyotokana na majibu ya maabara hapa duniani dhidi ya upotoshaji uliokuwa umeanza kuzagaa duniani ambapo ulichochewa na kauli ya Mheshimiwa Rais)

-Mleta umeshindwa kabisa kuonyesha mapungufu ya kauli ya Magufuli, ambapo kitaalamu unajua kabisa matamshi ya Magufuli yalikuwa ni upotoshaji wa kiwango cha SGR. (Kwanini? Uwezi kupima ubora wa vipimo vya maabara kwa kutumia sampuli isiyo sahihi (wrong specimen) na kamwe huwezi kutafsiri majibu ya maabara yaliyotokana na sampuli isiyo sahihi. Wrong specimen=Wrong test=Wrong result=Unexplainable science)

Mwisho kabisa mleta mada nimeona kama unatafuta ajira ya kuteuliwa ili kushika nafasi katika maabara kuu ya Taifa mara baada ya aliyepo sasa kusimamishwa au nafasi ya bure bure kutoka kwa mheshimiwa Rais. Sijaona mantiki ya wewe kujieleza ulivyo, kutoa wasifu wako, ulichosomea, wapi ulisomea, ulisomea nini nk. Huo ni utoto sana kwa msomi.
Yote kwa yote sote tunajua mheshimiwa yuko desperate kwa sababu ya sakata la COVID hivyo anaweza kuokota mtu yoyote yule mwenye kuonyesha uwezo wa kumcover katika hili, hivyo unaweza kuvuna chochote. Hivyo usisahau pia kuweka na kadi yako CCM mtandaoni kama unayo ili mheshimiwa ajue wewe ni kada mwaminifu ama sio.

Sihitaji kujitetea kwa sababu hunijui, na endelea hivyo hivyo. Kila ulichikiandika kina kasoro ya uelewa. Kukusaidia ni shule na si vinginevyo. Pole.
 
5.Au jee wataalam wetu walizidiwa na wingi wa sampuli, wakachoka, ikawa badala ya kupima sampuli zote, wakaamua kucheza mchezo wa ‘ana- ana-do”, hii positive, hii negative, hii positive, hii negative…Sidhani, wala sifikirii kwamba wataalamu wetu walojitolea mstari wa mbele kupigana vita kwa ajili yetu dhidi ya corona eti wafanye hivyo! La hasha! Na kama itakuwa hivyo basi tatizo ni kubwa sana!
Mkuu najuwa wengi wanaweza kusema hili haliwezekani kabisa.

Mimi nasema kwa tanzania hili linawezekana sana.

Ngoja hapa leo nilipue bomu moja kubwa sana kwenye sekta ya Telecom.

Kuna kampuni zinazopewa kandarasi na wenye minara ya simu ya kutembelea minara yote na kukagua ubora au nguvu ya signal husika kama ni 3G au 4G kuelekea pande husika zilizolengwa na waliosimika minara.
Vijana wengi wanaotumwa kufanya hizi kazi wanalipwa pesa ndogo na kupewa pesa kiasi kidogo sana cha kufanyia shughuli husika au ya kujikimu huko mikoani.
Kinachotokea vijana kutokana na kutaka kubana matumizi au wengine wamefanyia starehe pesa ya kukodi usafiri wa kufanyia Test drive hivyo wanapika baadhi ya hizi data kwenye software flani na kupata ripoti husika.

Hili jambo lipo tena kwa hakika kabisa na nisingependa kuzitaja kampuni zinazofanyiwa uhuni huu.
Kwa watanzania hili la kuchoka na kupika matokeo ya vipimo baada ya kuchoka au kuziharibu kimakosa kama kuangusha na kuogopa kuomba sample zingine inawezekanan kabisa.
 
Kuendelea kusoma ambavyo huvijui. Karibu kwenye darasa letu la "Drug Design"
Umeshauriwa andika hizo blablah zako kwenye lugha ya kisomi peleka kwenye vyuo makini duniani kama Hopkins au havard ipate ithibati alafu ndo uje kusifu na kuabudu, ili upate UDC

Vinginevyo unajifichaficha huku kwa wajinga wa fani hii ili kumfurahisi mtukufu akupandishe cheo
 
Ahsante sana kwa kuuliza swali hili, kwa kifupi ni kwamba wataalam wa analysis walitakiwa wawe na uwezo wa kutambua kuwa sample husika inakasoro hata kabla ya kuingiza kwenye mashine. Kazi ya tume itakuwa ni kutuambia nia yao haswa ilikuwa ni nini mpaka wakashindwa kutofautisha mafuta na human samples
Kuna ushahidi gani kuwa kuna sample za mapapai zilipelekwa maabara ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anyway, kuua kirusi kwa fumigation ni kichekesho, virusi vinahitaji living cells ili kuendelea kuishi, fumigation inafanyika kwenye objects which does not necessarily host viruses.
Swala la kunyunyuzia dawa lilielezwa mia yake na haikuwa kuua virusi bali kuua mbu na wadudu wengine wanaosababisha maradhi mengine yanayoweza kusababisha udhaifu kwa mtu, na endapo atapata virusi basi mwili hautaweza kuvimudu.
 
Kitaalamu, maelezo uliyotoa yanaeleweka. Tatizo ni MUKTADHA.

1) Umeeleza vizuri kwamba kama kulikuwa na haja ya kutathmini ubora wa hizo mashine kwenye hiyo maabara, zipo njia rasmi kabisa za kufanya hivyo, hakuna haja ya kuleta oili au mapapai. Sasa imekuwaje hayo yamefanyika, shida ipo kwenye Muktadha wa kisiasa. Kupima oili na mapapai ni more sensational. Inapamba headline za magazeti. Pia jiulize lengo kuu la Magufuli. Hataki data za Tanzania za covid19 ziwekwe wazi. Sababu? Data zinaonesha Hypothesis za Magufuli zimekwama. Hivyo anatafuta sababu za kufanya UHAKIKI wa maabara, INDEFINITELY .

Unakumbuka kisingizio cha kwanza alichotoa Magufuli kukwepa ishu ya kuboresha mishahara ya wafanyakazi, ambayo ilikuwa ahadi yake katika kampeni 2015? UHAKIKI. Uhakikivwa wafanyakazi hewa. Alisema anaomba mwezi mmoja au miwili. Matokeo yake? Mwaka wa tano huu hakuna maboresho ya mishahara, ila bei za vitu na huduma zimepanda sana. Maisha Magumu. Uhakiki unaendelea. Mpaka sasa serikali haitoi taarifa za maambukizi. Kisaikolojia, wengi watachukulia kwamba korona imekwisha! Taifa linapoteza nguvu kazi, ali mradi ego ya Magufuli itunzwe.

2) Suala la ubovu wa vifaa ni administrative, nchi nyingi zimekutana na hiyo changamoto. Wameipatia ufumbuzi haraka tu na upimaji unaendelea, data zinatolewa, hadi tunaambiwa Malkia wa Uingereza kapata covid, waziri mkuu Boris naye kapata hadi kalazwa ICU. Sasa kwetu kuna kipya chepi?

3) Ukitaka kujua Magufuli kaficha mbuzi kwenye gunia, angalia anachora ardhi kwa vidole vya miguu, wanaume kina Kagame na Kenyata wanapomuita waongee kiume. Si angekutana nao tu akawaeleza Theories zake?
You nailed it, Thank u.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kila kitu alichokiandika, na haya ndio ninaweza kueleza.

-Msingi wa ulichokiandika umekosa mantiki, maana umeeleza mambo mengi kiujumla na kwa kina, huku ukishindwa kueleza ni Vipi wakina Mwele Malecela na CDC wamepotosha. Maelezo ya Mwele yalikuwa yakiujumla, mafupi, yenye kueleweka moja kwa moja na hayakuwa mahsusi dhidi ya Mheshimiwa Rais (Tafsiri zetu zilielewa wazi Mwele alikuwa akijibu Shutuma za Mheshimiwa Rais kwa kusema madai ya Rais hayakuwa na mantiki yoyote ya kisayansi) na CDC walitetea ubora wa vipimo vya kimaabara unaotumika kupima COVID hapa Tanzania kuwa ni sahihi na ndio standard za dunia nzima. (Kimsingi CDC walikuwa wanalinda taarifa za maumbukizi yaliyotokana na majibu ya maabara hapa duniani dhidi ya upotoshaji uliokuwa umeanza kuzagaa duniani ambapo ulichochewa na kauli ya Mheshimiwa Rais)

-Mleta umeshindwa kabisa kuonyesha mapungufu ya kauli ya Magufuli, ambapo kitaalamu unajua kabisa matamshi ya Magufuli yalikuwa ni upotoshaji wa kiwango cha SGR. (Kwanini? Uwezi kupima ubora wa vipimo vya maabara kwa kutumia sampuli isiyo sahihi (wrong specimen) na kamwe huwezi kutafsiri majibu ya maabara yaliyotokana na sampuli isiyo sahihi. Wrong specimen=Wrong test=Wrong result=Unexplainable science)

Mwisho kabisa mleta mada nimeona kama unatafuta ajira ya kuteuliwa ili kushika nafasi katika maabara kuu ya Taifa mara baada ya aliyepo sasa kusimamishwa au nafasi ya bure bure kutoka kwa mheshimiwa Rais. Sijaona mantiki ya wewe kujieleza ulivyo, kutoa wasifu wako, ulichosomea, wapi ulisomea, ulisomea nini nk. Huo ni utoto sana kwa msomi.
Yote kwa yote sote tunajua mheshimiwa yuko desperate kwa sababu ya sakata la COVID hivyo anaweza kuokota mtu yoyote yule mwenye kuonyesha uwezo wa kumcover katika hili, hivyo unaweza kuvuna chochote. Hivyo usisahau pia kuweka na kadi yako CCM mtandaoni kama unayo ili mheshimiwa ajue wewe ni kada mwaminifu ama sio.
(Msingi wa ulichokiandika umekosa mantiki, maana umeeleza mambo mengi kiujumla na kwa kina,)

Kipengere hicho hapo juu kwenye mabano ulichokiandika mkuu, ndicho kilichokuondolea uhalali wa swali lako na umebakia kuwa na wewe umeegemea sehemu Fulani Kwa kujilazimisha hata kama umeuona ukweli,

Hata hivyo sishangai Kwa sababu kila mtu hutaka kuonekana kwamba anaweza kuliko mwingine hata kwenye mambo asyokuwa Nayo uelewa,

Ifike pahala tujikubali na kuwakubali wengine,

Kifaa kilichopimia mapapai ndicho hichohicho kilichompima Dereva wa Lori wa Kenya mpakani mwa Uganda, na aliporudishwa Kenya ikabidi apimwe tena Kwa kifaa hichohicho kikaonesha hakuwa na Maambukizi, Kwa nini vifaa hivi vistiliwe mashaka?
 
Back
Top Bottom