Vipimo vya COVID19: Dr. Mwele na Dr. John Nkengasong(Africa CDC) walitumika kupotosha ukweli wa kisayansi (wasaka tonge kazini)

Ahsante sana kwa maswali mazuri, hapo ndipo JPM anapopata shida dhidi ya wazungu na mawakala wao. Anapojaribu kusimama mwenyewe anaonekana anatenda kinyume na matakwa ya wenye nguvu (World Order). By the way, aliyeleta ugonjwa kaleta na vifaa vya kupimia na analazimisha kutumia hivyo vifaa hata kama ni vibovu.
Wewe ni researcher, kitu cha kwanza, ethically umekosea misingi ya research; kwanza hauko impartial, ushakuwa biased, rsearcher yeyote hajabisha, bali ameonesha "iaccurracy" ya vipimo "kiasi fulani"; upo very political- qualitative; you want to promote somebody. unasema "hapo ndipo JPM anapopata shida dhidi ya wazungu na mawakala wao" ukamalizia "aliyeleta ugonjwa kaleta na vifaa vya kupimia na analazimisha kutumia hivyo vifaa hata kama ni vibovu" in other words hivyo vifaa vingetoka from third party ungeviamini?
 
Vipi kama wewe ndiye msaka tonge hata ukaja na mada ya kutetea? Mimi bado na naswali mengi tu ya hizo RNA zinavyotenganishwa. Kwahiyo sijaridhika na maelezo ya huyu Dr
Kwanza kabisa naomba nianze kwa kudeclare “interest" kwenye suala ya Covid-19. Mimi ni mtafiti kwenye utengenezaji wa madawa haswa kwa kutumia "Computer Aided Drug Design (CADD)". Tangu janga hili la Covid-19 lianze, tumejikita kwenye kutafuta dawa itakayoweza kutibu Covid-19 kama ilivyo kwa wenzutu walioko maabara kote duniani.

Tukirudi kwenye mada; tokoa Mh. Rais John Pombe Magufuli alivyotoa matokeo ya unchunguzi dhidi ya ubora wa vifaa vinavyotumika kupima sampuli za corona, kumekwepo upotoshwaji wa makusudi dhidi ya hatua aliyochukua Mh. Rais. Kundi kubwa la watu wanadangwa mchana kweupe na watu wenye nia ovu dhidi ya usalama wa nchi, na taifa kwa ujumla.

Imekuwa kawaida ya kujkwa hili kushiriki upotoshwaji huu kwa kuleta makala ya watu wanaotumikia matumbo kupotosha ukweli na kuteka mjadala wa Covid-19.. Hivi karibuni, katika kupambana na ukweli Mh. Rais tumemsikia Dr. Mwele kupitia mtandao wa twitter akidhihaki hatua aliochukua Mh. Rais. Kama ni kweli twitter ile ilikuwa ya kwake basi nikiri wazi anauwezo mdogo sana kwenye sayansi ya upimaji.

Dkt. Mwele: Kipimo ulichokicalibrate kwa ajili ya COVID kitapima COVID ukiingiza sampuli ambazo siyo umeivuruga! Majibu yatakuwa hayana mantiki! - JamiiForums

Baada ya hapo kundi hilo likaja na hoja ya nyota ya Dr. Nyambura wakijaribu kuonyesha kwamba kasimamishwa kimakosa.

Nyota ya Dr Nyambura Moremi itang'aa Kimataifa - JamiiForums

Khali khadhalika, kwa kudhalalisha jukwa hili, kundi hili ovu likaja na hoja ya Dr. John Nkengasong wa (Africa CDC), wakishadadia maelezo yasio na “substance”kutoka kwa huyu mtalaam anaetumikia tumbo lake. Nikiri tena wazi, kama sio utumwa kwa mwajiri wake, basi mtalaam huyu atakuwa na shida mahali.

CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri - JamiiForums

Kwa heshima na taadhima, naleta kwenu maelezo ya kitaalam juu ya upimaji wa virusi vya corona kutoka kwa Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nikiri wazi kwamba simjui Dr. Ally wala sijawahi kumuona.

Hata wapotoshe, Kutakucha tu!

Tukiwa tupo kwenye taharuki juu ya kipimo cha corona (covid-19) hapa nchini, baada kutoa majibu ya positive kwa mbuzi na papai, naomba nitoe maoni yangu kama mdau katika tansia hii ya vitendanishi vya maabara (diagnostics).

Nianze kwa kutangaza maslahi yangu binafsi kwenye mada husika. Mimi ni mtafiti kwenye eneo hili la vitendanishi (Medical and clinical diagnostics). Tasnifu (thesis) yangu ya umahiri (MSc in Biotechnolgy) iljikita kwenye kutengeneza njia (method) ya kutambua kwa haraka na wepesi uwepo wa protini zinazoashiria uwepo wa saratani kwa binaadamu. Ama tasnifu yangu ya uzamivu (PhD in (Bio) Engineering) ilijikita kwenye kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajili ya kutendanisha vimelea vya maradhi (bacteria) kwa binaadamu. Tafiti zote zikiwa zimefanyika chuo kikuu cha Lund, Sweden. Kwa sasa tunaendelea na utafiti wa kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajilia ya kutendanisha kirusi kinacho shambulia simba na mbwa, kwa ufadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Pia kwa kutambua umuhimu wa kuwa na kitedanishi kinachoweza kutoa majibu haraka lakini pia kutumika nje ya maabara (rapid test strip) kwa ajili covid-19, tumetuma ‘concept note’ kwa mamlaka husika hapa Tanzania ili tuweze kuungwa mkono kwenye kutengeneza ‘rapid test’ itakayoweza kutendanisha mgonjwa covid-19 na asiye mgonjwa. Tungali tunasubiria mrejesho!

Tukirudi kwenye mada kuu, kwanza nitoe pongezi kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa uwamuzi wake wa kuamua kujiongeza ili kujiridhisha kama ni kweli Maabara yetu ya Taifa (NHL) inatoa majibu sahihi au la! Ni uamuzi sahihi na wakiuongozi!

Maswali tunayojiuliza: Jee njia zilizotumika (kupeleka sampuli (swab) za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu? Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini? Ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalam ndio tatizo? Au vyote? Kabla sijajibu maswali haya kwanza nianze kwa kuelezea jinsi covid-19 inavyopimwa:

Mpaka sasa kuna vipimo (vitendanishi) vya aina kuu mbili vinavyotumika kupima covid-19. Aina ya kwanza ni kile kinacho pima covid-19 kwa kuangalia uwepo wa kinasaba cha kirusi chenyewe (RNA). Kipimo hiki hujulikana kama ‘Real-time Reverse Transcription Polymerase Chain Reaction’ (RT-qPCR) au al-maarufu PCR! Hichi ndo kipimo mashuhuri na ‘standard’ kinachotumika ulimwenguni kwa sasa. Sampuli zake huchukuliwa kwa kurambisha (swab) kijiti cha pamba (cotton swab) ndani-nyuma ya pua (nasophyaryngeal swab) na/au ndani-nyuma ya mdomo (oropharyngeal swab).

Aina ya pili ni ile inayopima kwa kuangalia kinga (antibody) inayozalishwa na muathirika pindi anapopata maambukizi ya kirusi cha corona. Kipimo hichi hujulikana kama ‘Immune Rapid Test, na vipo vya aina tofauti. Aina maarufu kwa sasa ni ya ‘strip’, kama ile strip inayopima ujauzito kwenye mkojo (UPT strip) – aina hii hujulikana kama “Lateral flow immunochromatographic assays” au lateral flow test! Kipimo cha aina hii sampuli yake ni damu inayochukuliwa kwenye kidole (finger prick) au kwenye mkono (venepuncture). Kipimo hichi kwa sasa sio standard ila kuna kampuni mbali mbali duniania zinazalisha na zimepata vibali vya dharura kutoka FDA (USA) na mamlaka nyengine duniani kuingiza kwenye matumizi.

Kwa maelezo hayo bila shaka Maabara yetu ya Taifa huchakata sampuli za covid-19 kwa kutumia kitendanishi ambacho ni standard – PCR. Kitendanishi ambacho sampuli zake huchukuliwa ‘swab’ ya puani/ mdomoni! Sio mate, mkojo, damu wala kinyesi kama wengine wanavyo hoji!

Jee njia zilizotumiwa (kupeleka sampuli za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu?

Kuna wanaosema kitendanishi ukisha ki-calibrate kwa ajili ya sampuli flani ukipeleka sampuli tofauti majibu yanakuwa haya maana! Hivyo kwa sababu PCR hii ya covid-19 ilikuwa calibrated kwa ajili ya sampuli za swab ya pua na mdomo wa binaadamu kupeleka swab ya papai au mbuzi inafanya majibu ya kipimo yasiwe na maana! Kukubaliana au kupingana na hoja hii kwanza ni vyema kuelewa japo kwa muhtasari covid-19 ina pimwaje kwa PCR!

1.Sampuli ile, pamba (swab), hupokelewa maabara na kuandikishwa (registered) taarifa muhimu kama vile: taarifa za aliekusanya sampuli, taarifa za alieleta sampuli maabara, taafira za aina ya sampuli (swab ya pua au mdomo), taarifa za aliechukuliwa sampuli n.k.

2. Sampuli hiyo (pamba) hupitishwa hatua tofauti kwa kutumia kitenganishi maalum cha kinasaba cha RNA, kwa jina la kitaalamu ni ‘Viral RNA Extraction Kit’: kama vile, kuosha pamba hiyo (kuondoa kirusi kwenye pamba kiwe kwenye tube), kukipasua kirusi (lysis) ili kutoa kinasaba (RNA) ndani ya kirusi, na mwisho ni kusafisha (purification) ili kubaki na kinasaba cha kirusi tu. Kabla ya kupeleka kwenye PCR, kinasaba (RNA) hicho kilichosafishwa huangaliwa ubora wake (quality)! Ubora wake huhusisha wingi (concentration) na usafi (purity). Kuna kiasi na usafi maalumu ambao kama sampuli haijafikisha hutakiwi kuendelea nayo kwa hatua ya PCR, maana ni ubora usiofaa kwa kutoa majibu sahihi! Kifaa kinachotumika kupima ubora wa kinasaba (RNA) ni ‘spectrophotometer’ - modo maarufu ni ‘Nanodrop’. Sampuli (extracted RNA) ikikidhi vigezo (quality) ya kuendelea kwenye PCR, hupelekwa kwa ajili ya kusomwa ili ijulikane ni kinasaba cha kirusi kinachosababisha covid-19 au la!

3. PCR, hutendanisha kinasaba (RNA) kwanza kwa kukigeuza kutoka RNA kwenda DNA, kisha hutoa kopi nyingi (amplification) kwa kulenga maeneo mawili maalumu ya kinasaba, maeneo ambayo humtofautisha kinasaba cha corona anaesabisha covid-19 na kinasaba cha kirusi chengine chochote hata vile vya jamii moja na yeye, kama virusi vinavyoosababisha MERS na SARS. Kukopika kwa maeneo haya muhimu husomeka moja moja kwenye mashine hii ya PCR na ikifika kiwango kinachokubalika - mashine husoma-positive. Kama kopi itakuwa ni ya eneo moja tu kati ya hayo mawili mashine husoma – indeterminate (inconclusive), na kama hakuna kopi ya eneo hata moja- mashine husoma negative. Kwa majibu ya inconclusive maana yake kunahitajika sampuli nyengine kurudia kipimo.

Muhimu: Sampuli ya mgonjwa mara zote husomwa pamoja na sampuli za kukontroli (control samples) kwa ajili ya kuhakikisha kama PCR (mashine) inafanyakazi sawa sawa. Sampuli za kontroli hizi ni sehemu ya kinasaba cha kirusi cha covid-19 ambacho hutumika kama positive kontrol na maji maalum (buffer) yenye kila kilichowekwa kwenye sampuli halisi isipokuwa kinasaba (RNA) ambayo hutumika kama negative kontrol. Hivyo majibu hayo hapo juu hukubalika tu endapo postivive control itasoma positive na negative control ikisoma negative.

Kwa kuangalia hatua hizo, utaona kwamba kinachokwenda kwenye mashine ya PCR si mate wala makamasi, ni kinasaba (RNA) safi (purified RNA), haijalishi kimetolewa wapi! Lakini pia ile ‘Viral RNA Extraction Kit’ imetengenezwa kutenganisha na kusafisha kinasaba (RNA) cha kirusi kutoka specimen yoyote, iwe binaadamu, papai, mbuzi, bata, udongo n.k, kama swab ya hiyo specimen (mfano mbuzi) ina kirusi cha RNA basi RNA ya hicho kirusi itapatikana tu. Hivyo basi sampuli zilizopelekwa zilikuwa sahihi na hazileti mkanganyiko wowote kwenye mashine ya PCR wala kwenye extraction kit.

Lakini, jee kulikuwa na njia nyengine ya kujua ubora wa kifaa na wataalam husika?

Ndio! Kwenye utendaji kazi wa maabara, ili maabra kujiridhisha na majibu inayotoa, huwa inashirikisha maabara nyengine kupata majibu ya sampuli hiyo hiyo kulinganisha majibu yake, kitaalam inaitwa Inter-Laboratory Comparisons (ILC). Hivyo badala ya kupeleka sampuli ya papai au mbuzi kwenye maabara yetu ya taifa, tungetuma sampuli za baadhi ya waloambiwa positive na wale waloambiwa negative (na maabara yetu) kwenye maabara za nchi jirani kisha tukalinganisha majibu yao na ya kwetu!

Kwanini PCR kiwe kitendanishi standard cha covid-19?

PCR ina sifa mbili bora na muhimu za kipimo cha kimaabara zinazofanya kitendanishi hiki kiwe ndio standard:

1.‘High Sensitivity’: (a) ‘High analytical sensitivity’ (uwezo kusoma hata kiwango kidogo cha virusi) kwa maana hata kukiwepo na uzi mmoja tu wa kinasaba (single RNA strand) basi PCR inaweza kutendanisha! (b) ‘High clinical sensitivity’ (>95%), kwamaana kama kuna watu 100 wenye covid-19 (positive), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya positive kwa watu wasiopungua 95 miongoni mwa hao 100! Ijulikane, mpaka sasa hakuna kitendanishi chenye clinical sensitivity ya 100%!

2. ‘High Specificity/Selectivity’: (a) ‘High analytical specificity’ kwa maana ina kopi maeneo mawili ya kinasaba, maeneo ambayo ni maalumu kwa nCov tu, hivyo hata kirusi cha familia moja na nCov hakiwezi kusomwa (haichanganyi), achilia mbali wale wa mbali kama HIV na wengine. (b) High clinical Specificity (99%), kwa maana kama watakuja watu 100 ambao hawana covid-19 (negative), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya negative kwa watu 99 miongoni mwa hao 100! Hivyo PCR ikisoma positive ujuwe ni positive kweli!

Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini (ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalamu ndio tatizo au vyote?

Kwanza kabisa niseme kwamba kirusi hichi, SARS-CoV-2 au nCov, kinachosababisha ugonjwa wa corona (Covid-19), bado ni kipya, wanasayansi ndo kwanza wanajaribu kukielewa! Bado kila kukicha wanagundua kitu kipya juu ya kirusi hiki, kuanzia uwepo wake kwenye viumbe mbali mbali, uwepo wake sehemu mbali mbali za miili yetu, anavyojibadilisha (mutation), ushambuliaji wake, na hata hatari yake yakusababisha vifo. Ila kwa maarifa yaliyopo mpaka naandika makala hii kirusi hichi hakijaonekana kwenye sampuli zote zote katika hizi zilizopelekwa kwenye maabara yetu ya taifa (papai, mbuzi, n.k). Hivyo basi tulitegemea majibu yawe negative! Kuna sababu nyingi, moja au mchanganyiko zinazoweka kuwa zimepelekea majibu ya covid-19 positive kwa mbuzi na papai! Lakini katika sababu zote hizi, iwayo yoyote huwezi kuwaondoa kwenye mashaka wataalamu walopima sampuli hizi.

1. Inaweza kuwa ni ‘contamination’ wakati wa kuchukuwa sampuli, huenda mchukuaji hakuwa na ujuzi wa kuchukuwa sampuli, kupelekea ku-contaminate sampuli kwa namna moja au nyengine yoyote ile! Hivyo kimsingi alieonekana kuwa na covid-19 positive si mbuzi au papai bali ni mchukuwaji wa sampuli.

2. Au ‘contamination’ wakati wa kusafirisha na ku-process sampuli (extraction and purification) pale maabara kabla ya kupeleka kwenye PCR mashine! Hivyo sample ika pass kwenye Nanodrop na PCR ikasoma positive! Kimsingi positive sio papai wala mbuzi bali alie process sampuli maabara au msafirishaji wa sampuli!

3. Au ‘contamination’ wakati wa kuandaa sampuli kwa ajili ya PCR, huenda kwa bahati mbaya sampuli ya positive Kontrol iliingia bila kujua kwenye sampuli ya papai au mbuzi! Hivyo majibu yakasoma positive!

Kama ni moja katika hayo au yote basi kunatatizo la kiujuzi (lack of competence) katika kuchukuwa, ku-handle na ku-process sampuli. Hata kama aliechukuwa sampuli sio sehemu ya wataalamu wa maabara ya taifa, basi kuna tatizo katika kupokea sampuli (ambayo ni sehemu ya handling ya sampuli). Sampuli lazima zipokelewe kutoka kwa watu maalumu walopewa kazi hiyo wakiwa na ujuzi uliothibitishwa wa kufanya kazi hiyo! Sio kila mtu tu.

4. Jee vipi kama kitendanishi (PCR) ndio bomu? Ni kweli mashine inaweza kuwa imeharibika au ni kimeo kimeletwa kwa makusudi na "mabeberu", na wala hakukuwa na ‘contamination’ popote ila tu mashine inasema uwongo.

Kama ni hivyo, basi walitakiwa wao wataalamu wa maabara waling’amuwe hilo kabla ya mkuu wanchi kutilia mashaka na kuamua kuhakiki kwa njia zake. Utaratibu wa upimaji wa covid-19 kwa PCR (Standard Operating Procedure (SOP)) na utendaji kazi nzuri wa maabara (Good Laboratory Practice (GLP)) kama vitafuatwa ipasavyo vinawapa nafasi kwa wataalamu wa maabara kujua makosa/ubovu wa kifaa kabla yakukitumia na hata ubora wa sampuli kabla ya kuipima. Na hata baada ya kupelekewa sampuli za papai au mbuzi (sampuli ambao hazina nCov), utaratibu hapo juu unawawezesha kujua kwamba hii sampuli haifai hata kwenda kwenye PCR kwa kuangalia tu quality ya RNA (kinasaba) kwenye Nanodrop! Ila haiyondoi uwezekano kwamba kwenye papai au mbuzi kunaweza kuwa na kirusi chengine (RNA virus) na hivyo ukapata quality RNA kwenye Nanodrop! Lakini bado wangeweza kujua kwa kulinganisha majibu ya PCR ya sampuli ya negative kontrol na sampuli husika! Kama sampuli ya negative kontrol nayo inasoma positive, basi mashine ina matatizo!

5.Au jee wataalam wetu walizidiwa na wingi wa sampuli, wakachoka, ikawa badala ya kupima sampuli zote, wakaamua kucheza mchezo wa ‘ana- ana-do”, hii positive, hii negative, hii positive, hii negative…Sidhani, wala sifikirii kwamba wataalamu wetu walojitolea mstari wa mbele kupigana vita kwa ajili yetu dhidi ya corona eti wafanye hivyo! La hasha! Na kama itakuwa hivyo basi tatizo ni kubwa sana!

Mwisho siku haya yoote ni nadharia kwenye kitendawili cha kipimo cha covid-19 hapa nchini, kitendawili ambacho TUME iliyoundwa na waziri wa afya tutegemee italeta majibu sahihi ili waTanzania turudishe imani kwa majibu tunayopata! Kwa hakika jua litachomoza tena, kutakucha!

Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, UDSM

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Niwaombe viongozi wa Jamii Forum kupunguza mada zinazookana wazi kupotosha ukweli wa kisayansi ili kuwaokoa hawa wasaka tonge.

Ahsantenii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usisahau hao hao wakenya waliwapima madereva wao na kupelekwa karantini, alipimwa mara ya pili ikaonekana hana corona. Aibu!!
haaaaaaaaaaaa, Mr. researcher, Covid-19, unaweza kupima leo ukawa huna, lakini baada ya muda ukapima ukawa unayo, na kuna ambao hawana sympoms zozote zile. Kuna sehemu watu wameshakaa siku 14 wakapimwa hawana, baada siku ya 28 wamekutwa nayo, unataka kusema nini? what about those asymptomatic.
======================
President John Magufuli of Tanzania – which has not enacted any strict measures to curb the coronavirus, skipped the meeting, though Tanzania currently has 509 confirmed cases, with 21 deaths. After neighbouring Zambia recorded its biggest daily jump in cases – most at a town along the Tanzanian border – Zambia closed its border with Tanzania.
On Saturday, Zambia recorded 85 new confirmed cases, 76 in Nakonde, the border town with Tunduma, Tanzania. As of Tuesday, Zambia had a total of 441 Covid-19 cases and seven deaths
.
 
Ahsante sana kwa maswali mazuri, hapo ndipo JPM anapopata shida dhidi ya wazungu na mawakala wao. Anapojaribu kusimama mwenyewe anaonekana anatenda kinyume na matakwa ya wenye nguvu (World Order). By the way, aliyeleta ugonjwa kaleta na vifaa vya kupimia na analazimisha kutumia hivyo vifaa hata kama ni vibovu.
Mkuu unaweza kutafiti report ya evaluation ya hiyo machine hapa Tanzania ilifanywa na nani na majibu yalikuwaje mpaka kuihalalisha itumike?
 
Ahsante pia kwa swali, kwa kufipi, kwenye analytical chemistry, kipima ubora wa kifaa unachokitumia na kazi ya operator. hii ni pamoja na kuona kama majibu yanayotoka in authentic au sio. Kupeleka sample kwingineko ni last resort kama unahitaji kujiridhisha zaidi. Lakini kwa majibu haya ni wazi kun tatitzo, kama si ya kibinadamu basi ni machine. Tume itatusaidia kujibu

Ngoja tusubirie jibu la Tume kama litakuja kisayansi
 
Kwanza kabisa naomba nianze kwa kudeclare “interest" kwenye suala ya Covid-19. Mimi ni mtafiti kwenye utengenezaji wa madawa haswa kwa kutumia "Computer Aided Drug Design (CADD)". Tangu janga hili la Covid-19 lianze, tumejikita kwenye kutafuta dawa itakayoweza kutibu Covid-19 kama ilivyo kwa wenzutu walioko maabara kote duniani.

Tukirudi kwenye mada; tokoa Mh. Rais John Pombe Magufuli alivyotoa matokeo ya unchunguzi dhidi ya ubora wa vifaa vinavyotumika kupima sampuli za corona, kumekwepo upotoshwaji wa makusudi dhidi ya hatua aliyochukua Mh. Rais. Kundi kubwa la watu wanadangwa mchana kweupe na watu wenye nia ovu dhidi ya usalama wa nchi, na taifa kwa ujumla.

Imekuwa kawaida ya kujkwa hili kushiriki upotoshwaji huu kwa kuleta makala ya watu wanaotumikia matumbo kupotosha ukweli na kuteka mjadala wa Covid-19.. Hivi karibuni, katika kupambana na ukweli Mh. Rais tumemsikia Dr. Mwele kupitia mtandao wa twitter akidhihaki hatua aliochukua Mh. Rais. Kama ni kweli twitter ile ilikuwa ya kwake basi nikiri wazi anauwezo mdogo sana kwenye sayansi ya upimaji.

Dkt. Mwele: Kipimo ulichokicalibrate kwa ajili ya COVID kitapima COVID ukiingiza sampuli ambazo siyo umeivuruga! Majibu yatakuwa hayana mantiki! - JamiiForums

Baada ya hapo kundi hilo likaja na hoja ya nyota ya Dr. Nyambura wakijaribu kuonyesha kwamba kasimamishwa kimakosa.

Nyota ya Dr Nyambura Moremi itang'aa Kimataifa - JamiiForums

Khali khadhalika, kwa kudhalalisha jukwa hili, kundi hili ovu likaja na hoja ya Dr. John Nkengasong wa (Africa CDC), wakishadadia maelezo yasio na “substance”kutoka kwa huyu mtalaam anaetumikia tumbo lake. Nikiri tena wazi, kama sio utumwa kwa mwajiri wake, basi mtalaam huyu atakuwa na shida mahali.

CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri - JamiiForums

Kwa heshima na taadhima, naleta kwenu maelezo ya kitaalam juu ya upimaji wa virusi vya corona kutoka kwa Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nikiri wazi kwamba simjui Dr. Ally wala sijawahi kumuona.

Hata wapotoshe, Kutakucha tu!

Tukiwa tupo kwenye taharuki juu ya kipimo cha corona (covid-19) hapa nchini, baada kutoa majibu ya positive kwa mbuzi na papai, naomba nitoe maoni yangu kama mdau katika tansia hii ya vitendanishi vya maabara (diagnostics).

Nianze kwa kutangaza maslahi yangu binafsi kwenye mada husika. Mimi ni mtafiti kwenye eneo hili la vitendanishi (Medical and clinical diagnostics). Tasnifu (thesis) yangu ya umahiri (MSc in Biotechnolgy) iljikita kwenye kutengeneza njia (method) ya kutambua kwa haraka na wepesi uwepo wa protini zinazoashiria uwepo wa saratani kwa binaadamu. Ama tasnifu yangu ya uzamivu (PhD in (Bio) Engineering) ilijikita kwenye kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajili ya kutendanisha vimelea vya maradhi (bacteria) kwa binaadamu. Tafiti zote zikiwa zimefanyika chuo kikuu cha Lund, Sweden. Kwa sasa tunaendelea na utafiti wa kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajilia ya kutendanisha kirusi kinacho shambulia simba na mbwa, kwa ufadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Pia kwa kutambua umuhimu wa kuwa na kitedanishi kinachoweza kutoa majibu haraka lakini pia kutumika nje ya maabara (rapid test strip) kwa ajili covid-19, tumetuma ‘concept note’ kwa mamlaka husika hapa Tanzania ili tuweze kuungwa mkono kwenye kutengeneza ‘rapid test’ itakayoweza kutendanisha mgonjwa covid-19 na asiye mgonjwa. Tungali tunasubiria mrejesho!

Tukirudi kwenye mada kuu, kwanza nitoe pongezi kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa uwamuzi wake wa kuamua kujiongeza ili kujiridhisha kama ni kweli Maabara yetu ya Taifa (NHL) inatoa majibu sahihi au la! Ni uamuzi sahihi na wakiuongozi!

Maswali tunayojiuliza: Jee njia zilizotumika (kupeleka sampuli (swab) za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu? Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini? Ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalam ndio tatizo? Au vyote? Kabla sijajibu maswali haya kwanza nianze kwa kuelezea jinsi covid-19 inavyopimwa:

Mpaka sasa kuna vipimo (vitendanishi) vya aina kuu mbili vinavyotumika kupima covid-19. Aina ya kwanza ni kile kinacho pima covid-19 kwa kuangalia uwepo wa kinasaba cha kirusi chenyewe (RNA). Kipimo hiki hujulikana kama ‘Real-time Reverse Transcription Polymerase Chain Reaction’ (RT-qPCR) au al-maarufu PCR! Hichi ndo kipimo mashuhuri na ‘standard’ kinachotumika ulimwenguni kwa sasa. Sampuli zake huchukuliwa kwa kurambisha (swab) kijiti cha pamba (cotton swab) ndani-nyuma ya pua (nasophyaryngeal swab) na/au ndani-nyuma ya mdomo (oropharyngeal swab).

Aina ya pili ni ile inayopima kwa kuangalia kinga (antibody) inayozalishwa na muathirika pindi anapopata maambukizi ya kirusi cha corona. Kipimo hichi hujulikana kama ‘Immune Rapid Test, na vipo vya aina tofauti. Aina maarufu kwa sasa ni ya ‘strip’, kama ile strip inayopima ujauzito kwenye mkojo (UPT strip) – aina hii hujulikana kama “Lateral flow immunochromatographic assays” au lateral flow test! Kipimo cha aina hii sampuli yake ni damu inayochukuliwa kwenye kidole (finger prick) au kwenye mkono (venepuncture). Kipimo hichi kwa sasa sio standard ila kuna kampuni mbali mbali duniania zinazalisha na zimepata vibali vya dharura kutoka FDA (USA) na mamlaka nyengine duniani kuingiza kwenye matumizi.

Kwa maelezo hayo bila shaka Maabara yetu ya Taifa huchakata sampuli za covid-19 kwa kutumia kitendanishi ambacho ni standard – PCR. Kitendanishi ambacho sampuli zake huchukuliwa ‘swab’ ya puani/ mdomoni! Sio mate, mkojo, damu wala kinyesi kama wengine wanavyo hoji!

Jee njia zilizotumiwa (kupeleka sampuli za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu?

Kuna wanaosema kitendanishi ukisha ki-calibrate kwa ajili ya sampuli flani ukipeleka sampuli tofauti majibu yanakuwa haya maana! Hivyo kwa sababu PCR hii ya covid-19 ilikuwa calibrated kwa ajili ya sampuli za swab ya pua na mdomo wa binaadamu kupeleka swab ya papai au mbuzi inafanya majibu ya kipimo yasiwe na maana! Kukubaliana au kupingana na hoja hii kwanza ni vyema kuelewa japo kwa muhtasari covid-19 ina pimwaje kwa PCR!

1.Sampuli ile, pamba (swab), hupokelewa maabara na kuandikishwa (registered) taarifa muhimu kama vile: taarifa za aliekusanya sampuli, taarifa za alieleta sampuli maabara, taafira za aina ya sampuli (swab ya pua au mdomo), taarifa za aliechukuliwa sampuli n.k.

2. Sampuli hiyo (pamba) hupitishwa hatua tofauti kwa kutumia kitenganishi maalum cha kinasaba cha RNA, kwa jina la kitaalamu ni ‘Viral RNA Extraction Kit’: kama vile, kuosha pamba hiyo (kuondoa kirusi kwenye pamba kiwe kwenye tube), kukipasua kirusi (lysis) ili kutoa kinasaba (RNA) ndani ya kirusi, na mwisho ni kusafisha (purification) ili kubaki na kinasaba cha kirusi tu. Kabla ya kupeleka kwenye PCR, kinasaba (RNA) hicho kilichosafishwa huangaliwa ubora wake (quality)! Ubora wake huhusisha wingi (concentration) na usafi (purity). Kuna kiasi na usafi maalumu ambao kama sampuli haijafikisha hutakiwi kuendelea nayo kwa hatua ya PCR, maana ni ubora usiofaa kwa kutoa majibu sahihi! Kifaa kinachotumika kupima ubora wa kinasaba (RNA) ni ‘spectrophotometer’ - modo maarufu ni ‘Nanodrop’. Sampuli (extracted RNA) ikikidhi vigezo (quality) ya kuendelea kwenye PCR, hupelekwa kwa ajili ya kusomwa ili ijulikane ni kinasaba cha kirusi kinachosababisha covid-19 au la!

3. PCR, hutendanisha kinasaba (RNA) kwanza kwa kukigeuza kutoka RNA kwenda DNA, kisha hutoa kopi nyingi (amplification) kwa kulenga maeneo mawili maalumu ya kinasaba, maeneo ambayo humtofautisha kinasaba cha corona anaesabisha covid-19 na kinasaba cha kirusi chengine chochote hata vile vya jamii moja na yeye, kama virusi vinavyoosababisha MERS na SARS. Kukopika kwa maeneo haya muhimu husomeka moja moja kwenye mashine hii ya PCR na ikifika kiwango kinachokubalika - mashine husoma-positive. Kama kopi itakuwa ni ya eneo moja tu kati ya hayo mawili mashine husoma – indeterminate (inconclusive), na kama hakuna kopi ya eneo hata moja- mashine husoma negative. Kwa majibu ya inconclusive maana yake kunahitajika sampuli nyengine kurudia kipimo.

Muhimu: Sampuli ya mgonjwa mara zote husomwa pamoja na sampuli za kukontroli (control samples) kwa ajili ya kuhakikisha kama PCR (mashine) inafanyakazi sawa sawa. Sampuli za kontroli hizi ni sehemu ya kinasaba cha kirusi cha covid-19 ambacho hutumika kama positive kontrol na maji maalum (buffer) yenye kila kilichowekwa kwenye sampuli halisi isipokuwa kinasaba (RNA) ambayo hutumika kama negative kontrol. Hivyo majibu hayo hapo juu hukubalika tu endapo postivive control itasoma positive na negative control ikisoma negative.

Kwa kuangalia hatua hizo, utaona kwamba kinachokwenda kwenye mashine ya PCR si mate wala makamasi, ni kinasaba (RNA) safi (purified RNA), haijalishi kimetolewa wapi! Lakini pia ile ‘Viral RNA Extraction Kit’ imetengenezwa kutenganisha na kusafisha kinasaba (RNA) cha kirusi kutoka specimen yoyote, iwe binaadamu, papai, mbuzi, bata, udongo n.k, kama swab ya hiyo specimen (mfano mbuzi) ina kirusi cha RNA basi RNA ya hicho kirusi itapatikana tu. Hivyo basi sampuli zilizopelekwa zilikuwa sahihi na hazileti mkanganyiko wowote kwenye mashine ya PCR wala kwenye extraction kit.

Lakini, jee kulikuwa na njia nyengine ya kujua ubora wa kifaa na wataalam husika?

Ndio! Kwenye utendaji kazi wa maabara, ili maabra kujiridhisha na majibu inayotoa, huwa inashirikisha maabara nyengine kupata majibu ya sampuli hiyo hiyo kulinganisha majibu yake, kitaalam inaitwa Inter-Laboratory Comparisons (ILC). Hivyo badala ya kupeleka sampuli ya papai au mbuzi kwenye maabara yetu ya taifa, tungetuma sampuli za baadhi ya waloambiwa positive na wale waloambiwa negative (na maabara yetu) kwenye maabara za nchi jirani kisha tukalinganisha majibu yao na ya kwetu!

Kwanini PCR kiwe kitendanishi standard cha covid-19?

PCR ina sifa mbili bora na muhimu za kipimo cha kimaabara zinazofanya kitendanishi hiki kiwe ndio standard:

1.‘High Sensitivity’: (a) ‘High analytical sensitivity’ (uwezo kusoma hata kiwango kidogo cha virusi) kwa maana hata kukiwepo na uzi mmoja tu wa kinasaba (single RNA strand) basi PCR inaweza kutendanisha! (b) ‘High clinical sensitivity’ (>95%), kwamaana kama kuna watu 100 wenye covid-19 (positive), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya positive kwa watu wasiopungua 95 miongoni mwa hao 100! Ijulikane, mpaka sasa hakuna kitendanishi chenye clinical sensitivity ya 100%!

2. ‘High Specificity/Selectivity’: (a) ‘High analytical specificity’ kwa maana ina kopi maeneo mawili ya kinasaba, maeneo ambayo ni maalumu kwa nCov tu, hivyo hata kirusi cha familia moja na nCov hakiwezi kusomwa (haichanganyi), achilia mbali wale wa mbali kama HIV na wengine. (b) High clinical Specificity (99%), kwa maana kama watakuja watu 100 ambao hawana covid-19 (negative), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya negative kwa watu 99 miongoni mwa hao 100! Hivyo PCR ikisoma positive ujuwe ni positive kweli!

Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini (ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalamu ndio tatizo au vyote?

Kwanza kabisa niseme kwamba kirusi hichi, SARS-CoV-2 au nCov, kinachosababisha ugonjwa wa corona (Covid-19), bado ni kipya, wanasayansi ndo kwanza wanajaribu kukielewa! Bado kila kukicha wanagundua kitu kipya juu ya kirusi hiki, kuanzia uwepo wake kwenye viumbe mbali mbali, uwepo wake sehemu mbali mbali za miili yetu, anavyojibadilisha (mutation), ushambuliaji wake, na hata hatari yake yakusababisha vifo. Ila kwa maarifa yaliyopo mpaka naandika makala hii kirusi hichi hakijaonekana kwenye sampuli zote zote katika hizi zilizopelekwa kwenye maabara yetu ya taifa (papai, mbuzi, n.k). Hivyo basi tulitegemea majibu yawe negative! Kuna sababu nyingi, moja au mchanganyiko zinazoweka kuwa zimepelekea majibu ya covid-19 positive kwa mbuzi na papai! Lakini katika sababu zote hizi, iwayo yoyote huwezi kuwaondoa kwenye mashaka wataalamu walopima sampuli hizi.

1. Inaweza kuwa ni ‘contamination’ wakati wa kuchukuwa sampuli, huenda mchukuaji hakuwa na ujuzi wa kuchukuwa sampuli, kupelekea ku-contaminate sampuli kwa namna moja au nyengine yoyote ile! Hivyo kimsingi alieonekana kuwa na covid-19 positive si mbuzi au papai bali ni mchukuwaji wa sampuli.

2. Au ‘contamination’ wakati wa kusafirisha na ku-process sampuli (extraction and purification) pale maabara kabla ya kupeleka kwenye PCR mashine! Hivyo sample ika pass kwenye Nanodrop na PCR ikasoma positive! Kimsingi positive sio papai wala mbuzi bali alie process sampuli maabara au msafirishaji wa sampuli!

3. Au ‘contamination’ wakati wa kuandaa sampuli kwa ajili ya PCR, huenda kwa bahati mbaya sampuli ya positive Kontrol iliingia bila kujua kwenye sampuli ya papai au mbuzi! Hivyo majibu yakasoma positive!

Kama ni moja katika hayo au yote basi kunatatizo la kiujuzi (lack of competence) katika kuchukuwa, ku-handle na ku-process sampuli. Hata kama aliechukuwa sampuli sio sehemu ya wataalamu wa maabara ya taifa, basi kuna tatizo katika kupokea sampuli (ambayo ni sehemu ya handling ya sampuli). Sampuli lazima zipokelewe kutoka kwa watu maalumu walopewa kazi hiyo wakiwa na ujuzi uliothibitishwa wa kufanya kazi hiyo! Sio kila mtu tu.

4. Jee vipi kama kitendanishi (PCR) ndio bomu? Ni kweli mashine inaweza kuwa imeharibika au ni kimeo kimeletwa kwa makusudi na "mabeberu", na wala hakukuwa na ‘contamination’ popote ila tu mashine inasema uwongo.

Kama ni hivyo, basi walitakiwa wao wataalamu wa maabara waling’amuwe hilo kabla ya mkuu wanchi kutilia mashaka na kuamua kuhakiki kwa njia zake. Utaratibu wa upimaji wa covid-19 kwa PCR (Standard Operating Procedure (SOP)) na utendaji kazi nzuri wa maabara (Good Laboratory Practice (GLP)) kama vitafuatwa ipasavyo vinawapa nafasi kwa wataalamu wa maabara kujua makosa/ubovu wa kifaa kabla yakukitumia na hata ubora wa sampuli kabla ya kuipima. Na hata baada ya kupelekewa sampuli za papai au mbuzi (sampuli ambao hazina nCov), utaratibu hapo juu unawawezesha kujua kwamba hii sampuli haifai hata kwenda kwenye PCR kwa kuangalia tu quality ya RNA (kinasaba) kwenye Nanodrop! Ila haiyondoi uwezekano kwamba kwenye papai au mbuzi kunaweza kuwa na kirusi chengine (RNA virus) na hivyo ukapata quality RNA kwenye Nanodrop! Lakini bado wangeweza kujua kwa kulinganisha majibu ya PCR ya sampuli ya negative kontrol na sampuli husika! Kama sampuli ya negative kontrol nayo inasoma positive, basi mashine ina matatizo!

5.Au jee wataalam wetu walizidiwa na wingi wa sampuli, wakachoka, ikawa badala ya kupima sampuli zote, wakaamua kucheza mchezo wa ‘ana- ana-do”, hii positive, hii negative, hii positive, hii negative…Sidhani, wala sifikirii kwamba wataalamu wetu walojitolea mstari wa mbele kupigana vita kwa ajili yetu dhidi ya corona eti wafanye hivyo! La hasha! Na kama itakuwa hivyo basi tatizo ni kubwa sana!

Mwisho siku haya yoote ni nadharia kwenye kitendawili cha kipimo cha covid-19 hapa nchini, kitendawili ambacho TUME iliyoundwa na waziri wa afya tutegemee italeta majibu sahihi ili waTanzania turudishe imani kwa majibu tunayopata! Kwa hakika jua litachomoza tena, kutakucha!

Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, UDSM

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Niwaombe viongozi wa Jamii Forum kupunguza mada zinazookana wazi kupotosha ukweli wa kisayansi ili kuwaokoa hawa wasaka tonge.

Ahsantenii
Ulipomtaja Mwele nikajua umemmisquote. Huyu si ndo alikuwa Mkurugenzi wa NIMR?
Bado nadhani hiyo account iliyotumika kutoa comment itakuwa sio yake.
Maana imetolewa kama vile Mwele hata hajui chochote kuhusu PCR
No it cant be Mwele - Yule Biologist mwenye PhD tuliyemtetea alipotumbuliwa
 
Sijawahi kuteuliwa wala sitegemei uteuzi. Kazi yangu ni kukusaidia wewe dhidi ya wasaka tonge
Mkuu nashukru sana kwa makala yako, bahati mbaya ni makala iliyo deep sana kwenye molecular biology na humu wengi si wataalam, so utaambulia kejeli matusi na kuitwa Lumumba.

Hii ni sababu watu wamejeruhiwa kihisia na majibu yanatoka kihisia bila facts za kisayansi.

Uliyoandika ni kweli na mojawapo yanaweza yakawa sababu.

Ilishawahi kunitokea wakati nafanya tasnifu ya shahada ya umahiri ambapo nilikua na sample 28 lakini zilizokua na ubora baada ha kufanya DNA extraction zilikua sample 7 tu.
Nilifanya PCR na zile sample bora na safi (pure) nilizipelekea kwenye DNA sequencer.

Baada ya kufanya protocal zote na kuweka sample nilishangaa baada ya ku-run 24hrs, kesho yake sample yangu moja ilionesha ilikua ni nyani tena wanapatikana Congo, nilipaniki sababu mimi sample zangu zilikua ni fangasi kutoka kwenye matunda. Lakini tulivyofanya uchunguzi, tulikuja kujua kumbe technician alikosea kuweka template so kukawa na mislabelling.
 
Nimesoma makala yako kituo kwa kituo, sina tatizo na ulipojibu hoja za Mwele na mkuu wa CDC Africa

Hoja hujibiwa kwa hoja hilo halina ubishi

Shida yangu ipo kwenye namna ulivyofanya conclusions zako, moja umeacha sayansi ukakimbilia kwenye siasa "Mabeberu" Hivyo vipimo havikuwepo kabla ya ujio wa Covid-19
Kipindi hicho mnatumia hivyo vipimo kwa ajili ya mambo mengine mabeberu hawakuwepo?

La pili umetumia nguvu nyingi sana kutuaminisha wewe ni mtaalam, kwa nadharia za kawaida tu anayepiga kelele nyingi kwenye chumba ndiye mdhaifu.

Tatu Watanzania tunajijua wenyewe, kwa mdomo tu tuna tatizo kwa haya yote unayoyajua vipi unafanya kazi kwenye maabara ya taifa sasa hivi?
Kama haufanyi tunaambiwa wapimaji ni wachache kwanini hukuomba nafasi uonyeshe ujuzi wako pale kuwasaidia Watanzania.

Tanzania yetu hii mwenye degree anatafuta kazi na mwenye kazi anatafuta degree hivyo wacha mimi nisiburie Mtaalam atakaye jibu hoja zako niendelee kujifunza.

Mwisho kabisa CV yako nadhani itapokelewa Chato ukawe katibu Mkuu wizara ya Afya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma makala yako kituo kwa kituo, sina tatizo na ulipojibu hoja za Mwele na mkuu wa CDC Africa

Hoja hujibiwa kwa hoja hilo halina ubishi

Shida yangu ipo kwenye namna ulivyofanya conclusions zako, moja umeacha sayansi ukakimbilia kwenye siasa "Mabeberu" Hivyo vipomo havikuwepo kabla ya ujio wa Covid-19
Kipindi hicho mnatumia hivyo vipimo kwa ajili ya mambo mengine mabeberu hawakuwepo?

La pili umetumia nguvu nyingi sana kutuaminisha wewe ni mtaalam, kwa nadharia za kawaida tu anayepiga kelele nyingi kwenye chumba ndiye mdhaifu.

Tatu Watanzania tunajijua wenyewe, kwa mdomo tu tuna tatizo kwa haya yote unayoyajua vipi unafanya kazi kwenye maabara ya taifa sasa hivi?
Kama haufanyi tunaambiwa wapimaji ni wachache kwanini hukuomba nafasi uonyeshe ujuzi wako pale kuwasaidia Watanzania.

Tanzania yetu hii mwenye degree anatafuta kazi na mwenye kazi anatafuta degree hivyo wacha mimi nisiburie Mtaalam atakaye jibu hoja zako niendelee kujifunza.

Mwisho kabisa CV yako nadhani itapokelewa Chato ukawe katibu Mkuu wizara ya Afya

Sent using Jamii Forums mobile app
UncleBen kwanza ahsante sana kwa maoni yako. Pili, naomba uelewe kwamba nia na madhumuni yangu haikuwa kutafuta kazi bali kuonyesha ukweli halisi. Walioitwa wasaka tonge kwenye uzi huu mara nyingi hawapendi mtu ajitokeze kuelezea ukweli ili waendelee kuwadanganya watu wengi. Mwaka 2015, niliwahi kufutwa inbox na kupigwa biti kali sana na kundi hilo.
Tushirikiane kunyoosha panapindishwa kwa lazima kama ipo ndani ya uwezo wetu.

Nimemalizia kwa kutoka kidogo nje ya sayansi kwa sababu mada za huko nyuma zililetwa kisiasa zaidi. Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe lakini kuruhusu jina lako litumike kisiasa inamaana unakubaliana na yanayosemwa. Napata shida sana kuamini kwamba account husika ni ya Dr.Mwele.
Ulipomtaja Mwele nikajua umemmisquote. Huyu si ndo alikuwa Mkurugenzi wa NIMR?
Bado nadhani hiyo account iliyotumika kutoa comment itakuwa sio yake.
Maana imetolewa kama vile Mwele hata hajui chochote kuhusu PCR
No it cant be Mwele - Yule Biologist mwenye PhD tuliyemtetea alipotumbuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa naomba nianze kwa kudeclare “interest" kwenye suala ya Covid-19. Mimi ni mtafiti kwenye utengenezaji wa madawa haswa kwa kutumia "Computer Aided Drug Design (CADD)". Tangu janga hili la Covid-19 lianze, tumejikita kwenye kutafuta dawa itakayoweza kutibu Covid-19 kama ilivyo kwa wenzutu walioko maabara kote duniani.

Tukirudi kwenye mada; tokoa Mh. Rais John Pombe Magufuli alivyotoa matokeo ya unchunguzi dhidi ya ubora wa vifaa vinavyotumika kupima sampuli za corona, kumekwepo upotoshwaji wa makusudi dhidi ya hatua aliyochukua Mh. Rais. Kundi kubwa la watu wanadangwa mchana kweupe na watu wenye nia ovu dhidi ya usalama wa nchi, na taifa kwa ujumla.

Imekuwa kawaida ya kujkwa hili kushiriki upotoshwaji huu kwa kuleta makala ya watu wanaotumikia matumbo kupotosha ukweli na kuteka mjadala wa Covid-19.. Hivi karibuni, katika kupambana na ukweli Mh. Rais tumemsikia Dr. Mwele kupitia mtandao wa twitter akidhihaki hatua aliochukua Mh. Rais. Kama ni kweli twitter ile ilikuwa ya kwake basi nikiri wazi anauwezo mdogo sana kwenye sayansi ya upimaji.

Dkt. Mwele: Kipimo ulichokicalibrate kwa ajili ya COVID kitapima COVID ukiingiza sampuli ambazo siyo umeivuruga! Majibu yatakuwa hayana mantiki! - JamiiForums

Baada ya hapo kundi hilo likaja na hoja ya nyota ya Dr. Nyambura wakijaribu kuonyesha kwamba kasimamishwa kimakosa.

Nyota ya Dr Nyambura Moremi itang'aa Kimataifa - JamiiForums

Khali khadhalika, kwa kudhalalisha jukwa hili, kundi hili ovu likaja na hoja ya Dr. John Nkengasong wa (Africa CDC), wakishadadia maelezo yasio na “substance”kutoka kwa huyu mtalaam anaetumikia tumbo lake. Nikiri tena wazi, kama sio utumwa kwa mwajiri wake, basi mtalaam huyu atakuwa na shida mahali.

CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri - JamiiForums

Kwa heshima na taadhima, naleta kwenu maelezo ya kitaalam juu ya upimaji wa virusi vya corona kutoka kwa Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nikiri wazi kwamba simjui Dr. Ally wala sijawahi kumuona.

Hata wapotoshe, Kutakucha tu!

Tukiwa tupo kwenye taharuki juu ya kipimo cha corona (covid-19) hapa nchini, baada kutoa majibu ya positive kwa mbuzi na papai, naomba nitoe maoni yangu kama mdau katika tansia hii ya vitendanishi vya maabara (diagnostics).

Nianze kwa kutangaza maslahi yangu binafsi kwenye mada husika. Mimi ni mtafiti kwenye eneo hili la vitendanishi (Medical and clinical diagnostics). Tasnifu (thesis) yangu ya umahiri (MSc in Biotechnolgy) iljikita kwenye kutengeneza njia (method) ya kutambua kwa haraka na wepesi uwepo wa protini zinazoashiria uwepo wa saratani kwa binaadamu. Ama tasnifu yangu ya uzamivu (PhD in (Bio) Engineering) ilijikita kwenye kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajili ya kutendanisha vimelea vya maradhi (bacteria) kwa binaadamu. Tafiti zote zikiwa zimefanyika chuo kikuu cha Lund, Sweden. Kwa sasa tunaendelea na utafiti wa kutengeneza kitendanishi cha kihisio cha kibayolojia (Biosensor) kwa ajilia ya kutendanisha kirusi kinacho shambulia simba na mbwa, kwa ufadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Pia kwa kutambua umuhimu wa kuwa na kitedanishi kinachoweza kutoa majibu haraka lakini pia kutumika nje ya maabara (rapid test strip) kwa ajili covid-19, tumetuma ‘concept note’ kwa mamlaka husika hapa Tanzania ili tuweze kuungwa mkono kwenye kutengeneza ‘rapid test’ itakayoweza kutendanisha mgonjwa covid-19 na asiye mgonjwa. Tungali tunasubiria mrejesho!

Tukirudi kwenye mada kuu, kwanza nitoe pongezi kwa Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa uwamuzi wake wa kuamua kujiongeza ili kujiridhisha kama ni kweli Maabara yetu ya Taifa (NHL) inatoa majibu sahihi au la! Ni uamuzi sahihi na wakiuongozi!

Maswali tunayojiuliza: Jee njia zilizotumika (kupeleka sampuli (swab) za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu? Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini? Ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalam ndio tatizo? Au vyote? Kabla sijajibu maswali haya kwanza nianze kwa kuelezea jinsi covid-19 inavyopimwa:

Mpaka sasa kuna vipimo (vitendanishi) vya aina kuu mbili vinavyotumika kupima covid-19. Aina ya kwanza ni kile kinacho pima covid-19 kwa kuangalia uwepo wa kinasaba cha kirusi chenyewe (RNA). Kipimo hiki hujulikana kama ‘Real-time Reverse Transcription Polymerase Chain Reaction’ (RT-qPCR) au al-maarufu PCR! Hichi ndo kipimo mashuhuri na ‘standard’ kinachotumika ulimwenguni kwa sasa. Sampuli zake huchukuliwa kwa kurambisha (swab) kijiti cha pamba (cotton swab) ndani-nyuma ya pua (nasophyaryngeal swab) na/au ndani-nyuma ya mdomo (oropharyngeal swab).

Aina ya pili ni ile inayopima kwa kuangalia kinga (antibody) inayozalishwa na muathirika pindi anapopata maambukizi ya kirusi cha corona. Kipimo hichi hujulikana kama ‘Immune Rapid Test, na vipo vya aina tofauti. Aina maarufu kwa sasa ni ya ‘strip’, kama ile strip inayopima ujauzito kwenye mkojo (UPT strip) – aina hii hujulikana kama “Lateral flow immunochromatographic assays” au lateral flow test! Kipimo cha aina hii sampuli yake ni damu inayochukuliwa kwenye kidole (finger prick) au kwenye mkono (venepuncture). Kipimo hichi kwa sasa sio standard ila kuna kampuni mbali mbali duniania zinazalisha na zimepata vibali vya dharura kutoka FDA (USA) na mamlaka nyengine duniani kuingiza kwenye matumizi.

Kwa maelezo hayo bila shaka Maabara yetu ya Taifa huchakata sampuli za covid-19 kwa kutumia kitendanishi ambacho ni standard – PCR. Kitendanishi ambacho sampuli zake huchukuliwa ‘swab’ ya puani/ mdomoni! Sio mate, mkojo, damu wala kinyesi kama wengine wanavyo hoji!

Jee njia zilizotumiwa (kupeleka sampuli za papai, fenesi, oil na mbuzi) kujua usahihi wa majibu ni sahihi kitaalamu?

Kuna wanaosema kitendanishi ukisha ki-calibrate kwa ajili ya sampuli flani ukipeleka sampuli tofauti majibu yanakuwa haya maana! Hivyo kwa sababu PCR hii ya covid-19 ilikuwa calibrated kwa ajili ya sampuli za swab ya pua na mdomo wa binaadamu kupeleka swab ya papai au mbuzi inafanya majibu ya kipimo yasiwe na maana! Kukubaliana au kupingana na hoja hii kwanza ni vyema kuelewa japo kwa muhtasari covid-19 ina pimwaje kwa PCR!

1.Sampuli ile, pamba (swab), hupokelewa maabara na kuandikishwa (registered) taarifa muhimu kama vile: taarifa za aliekusanya sampuli, taarifa za alieleta sampuli maabara, taafira za aina ya sampuli (swab ya pua au mdomo), taarifa za aliechukuliwa sampuli n.k.

2. Sampuli hiyo (pamba) hupitishwa hatua tofauti kwa kutumia kitenganishi maalum cha kinasaba cha RNA, kwa jina la kitaalamu ni ‘Viral RNA Extraction Kit’: kama vile, kuosha pamba hiyo (kuondoa kirusi kwenye pamba kiwe kwenye tube), kukipasua kirusi (lysis) ili kutoa kinasaba (RNA) ndani ya kirusi, na mwisho ni kusafisha (purification) ili kubaki na kinasaba cha kirusi tu. Kabla ya kupeleka kwenye PCR, kinasaba (RNA) hicho kilichosafishwa huangaliwa ubora wake (quality)! Ubora wake huhusisha wingi (concentration) na usafi (purity). Kuna kiasi na usafi maalumu ambao kama sampuli haijafikisha hutakiwi kuendelea nayo kwa hatua ya PCR, maana ni ubora usiofaa kwa kutoa majibu sahihi! Kifaa kinachotumika kupima ubora wa kinasaba (RNA) ni ‘spectrophotometer’ - modo maarufu ni ‘Nanodrop’. Sampuli (extracted RNA) ikikidhi vigezo (quality) ya kuendelea kwenye PCR, hupelekwa kwa ajili ya kusomwa ili ijulikane ni kinasaba cha kirusi kinachosababisha covid-19 au la!

3. PCR, hutendanisha kinasaba (RNA) kwanza kwa kukigeuza kutoka RNA kwenda DNA, kisha hutoa kopi nyingi (amplification) kwa kulenga maeneo mawili maalumu ya kinasaba, maeneo ambayo humtofautisha kinasaba cha corona anaesabisha covid-19 na kinasaba cha kirusi chengine chochote hata vile vya jamii moja na yeye, kama virusi vinavyoosababisha MERS na SARS. Kukopika kwa maeneo haya muhimu husomeka moja moja kwenye mashine hii ya PCR na ikifika kiwango kinachokubalika - mashine husoma-positive. Kama kopi itakuwa ni ya eneo moja tu kati ya hayo mawili mashine husoma – indeterminate (inconclusive), na kama hakuna kopi ya eneo hata moja- mashine husoma negative. Kwa majibu ya inconclusive maana yake kunahitajika sampuli nyengine kurudia kipimo.

Muhimu: Sampuli ya mgonjwa mara zote husomwa pamoja na sampuli za kukontroli (control samples) kwa ajili ya kuhakikisha kama PCR (mashine) inafanyakazi sawa sawa. Sampuli za kontroli hizi ni sehemu ya kinasaba cha kirusi cha covid-19 ambacho hutumika kama positive kontrol na maji maalum (buffer) yenye kila kilichowekwa kwenye sampuli halisi isipokuwa kinasaba (RNA) ambayo hutumika kama negative kontrol. Hivyo majibu hayo hapo juu hukubalika tu endapo postivive control itasoma positive na negative control ikisoma negative.

Kwa kuangalia hatua hizo, utaona kwamba kinachokwenda kwenye mashine ya PCR si mate wala makamasi, ni kinasaba (RNA) safi (purified RNA), haijalishi kimetolewa wapi! Lakini pia ile ‘Viral RNA Extraction Kit’ imetengenezwa kutenganisha na kusafisha kinasaba (RNA) cha kirusi kutoka specimen yoyote, iwe binaadamu, papai, mbuzi, bata, udongo n.k, kama swab ya hiyo specimen (mfano mbuzi) ina kirusi cha RNA basi RNA ya hicho kirusi itapatikana tu. Hivyo basi sampuli zilizopelekwa zilikuwa sahihi na hazileti mkanganyiko wowote kwenye mashine ya PCR wala kwenye extraction kit.

Lakini, jee kulikuwa na njia nyengine ya kujua ubora wa kifaa na wataalam husika?

Ndio! Kwenye utendaji kazi wa maabara, ili maabra kujiridhisha na majibu inayotoa, huwa inashirikisha maabara nyengine kupata majibu ya sampuli hiyo hiyo kulinganisha majibu yake, kitaalam inaitwa Inter-Laboratory Comparisons (ILC). Hivyo badala ya kupeleka sampuli ya papai au mbuzi kwenye maabara yetu ya taifa, tungetuma sampuli za baadhi ya waloambiwa positive na wale waloambiwa negative (na maabara yetu) kwenye maabara za nchi jirani kisha tukalinganisha majibu yao na ya kwetu!

Kwanini PCR kiwe kitendanishi standard cha covid-19?

PCR ina sifa mbili bora na muhimu za kipimo cha kimaabara zinazofanya kitendanishi hiki kiwe ndio standard:

1.‘High Sensitivity’: (a) ‘High analytical sensitivity’ (uwezo kusoma hata kiwango kidogo cha virusi) kwa maana hata kukiwepo na uzi mmoja tu wa kinasaba (single RNA strand) basi PCR inaweza kutendanisha! (b) ‘High clinical sensitivity’ (>95%), kwamaana kama kuna watu 100 wenye covid-19 (positive), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya positive kwa watu wasiopungua 95 miongoni mwa hao 100! Ijulikane, mpaka sasa hakuna kitendanishi chenye clinical sensitivity ya 100%!

2. ‘High Specificity/Selectivity’: (a) ‘High analytical specificity’ kwa maana ina kopi maeneo mawili ya kinasaba, maeneo ambayo ni maalumu kwa nCov tu, hivyo hata kirusi cha familia moja na nCov hakiwezi kusomwa (haichanganyi), achilia mbali wale wa mbali kama HIV na wengine. (b) High clinical Specificity (99%), kwa maana kama watakuja watu 100 ambao hawana covid-19 (negative), basi pasi na shaka PCR mashine itakupa majibu ya negative kwa watu 99 miongoni mwa hao 100! Hivyo PCR ikisoma positive ujuwe ni positive kweli!

Jee Majibu yaliyopatikana (mbuzi na papai kuwa positive kwa covid-19) yanaashiria nini (ni mashine (kitendanishi) au ni wataaalamu ndio tatizo au vyote?

Kwanza kabisa niseme kwamba kirusi hichi, SARS-CoV-2 au nCov, kinachosababisha ugonjwa wa corona (Covid-19), bado ni kipya, wanasayansi ndo kwanza wanajaribu kukielewa! Bado kila kukicha wanagundua kitu kipya juu ya kirusi hiki, kuanzia uwepo wake kwenye viumbe mbali mbali, uwepo wake sehemu mbali mbali za miili yetu, anavyojibadilisha (mutation), ushambuliaji wake, na hata hatari yake yakusababisha vifo. Ila kwa maarifa yaliyopo mpaka naandika makala hii kirusi hichi hakijaonekana kwenye sampuli zote zote katika hizi zilizopelekwa kwenye maabara yetu ya taifa (papai, mbuzi, n.k). Hivyo basi tulitegemea majibu yawe negative! Kuna sababu nyingi, moja au mchanganyiko zinazoweka kuwa zimepelekea majibu ya covid-19 positive kwa mbuzi na papai! Lakini katika sababu zote hizi, iwayo yoyote huwezi kuwaondoa kwenye mashaka wataalamu walopima sampuli hizi.

1. Inaweza kuwa ni ‘contamination’ wakati wa kuchukuwa sampuli, huenda mchukuaji hakuwa na ujuzi wa kuchukuwa sampuli, kupelekea ku-contaminate sampuli kwa namna moja au nyengine yoyote ile! Hivyo kimsingi alieonekana kuwa na covid-19 positive si mbuzi au papai bali ni mchukuwaji wa sampuli.

2. Au ‘contamination’ wakati wa kusafirisha na ku-process sampuli (extraction and purification) pale maabara kabla ya kupeleka kwenye PCR mashine! Hivyo sample ika pass kwenye Nanodrop na PCR ikasoma positive! Kimsingi positive sio papai wala mbuzi bali alie process sampuli maabara au msafirishaji wa sampuli!

3. Au ‘contamination’ wakati wa kuandaa sampuli kwa ajili ya PCR, huenda kwa bahati mbaya sampuli ya positive Kontrol iliingia bila kujua kwenye sampuli ya papai au mbuzi! Hivyo majibu yakasoma positive!

Kama ni moja katika hayo au yote basi kunatatizo la kiujuzi (lack of competence) katika kuchukuwa, ku-handle na ku-process sampuli. Hata kama aliechukuwa sampuli sio sehemu ya wataalamu wa maabara ya taifa, basi kuna tatizo katika kupokea sampuli (ambayo ni sehemu ya handling ya sampuli). Sampuli lazima zipokelewe kutoka kwa watu maalumu walopewa kazi hiyo wakiwa na ujuzi uliothibitishwa wa kufanya kazi hiyo! Sio kila mtu tu.

4. Jee vipi kama kitendanishi (PCR) ndio bomu? Ni kweli mashine inaweza kuwa imeharibika au ni kimeo kimeletwa kwa makusudi na "mabeberu", na wala hakukuwa na ‘contamination’ popote ila tu mashine inasema uwongo.

Kama ni hivyo, basi walitakiwa wao wataalamu wa maabara waling’amuwe hilo kabla ya mkuu wanchi kutilia mashaka na kuamua kuhakiki kwa njia zake. Utaratibu wa upimaji wa covid-19 kwa PCR (Standard Operating Procedure (SOP)) na utendaji kazi nzuri wa maabara (Good Laboratory Practice (GLP)) kama vitafuatwa ipasavyo vinawapa nafasi kwa wataalamu wa maabara kujua makosa/ubovu wa kifaa kabla yakukitumia na hata ubora wa sampuli kabla ya kuipima. Na hata baada ya kupelekewa sampuli za papai au mbuzi (sampuli ambao hazina nCov), utaratibu hapo juu unawawezesha kujua kwamba hii sampuli haifai hata kwenda kwenye PCR kwa kuangalia tu quality ya RNA (kinasaba) kwenye Nanodrop! Ila haiyondoi uwezekano kwamba kwenye papai au mbuzi kunaweza kuwa na kirusi chengine (RNA virus) na hivyo ukapata quality RNA kwenye Nanodrop! Lakini bado wangeweza kujua kwa kulinganisha majibu ya PCR ya sampuli ya negative kontrol na sampuli husika! Kama sampuli ya negative kontrol nayo inasoma positive, basi mashine ina matatizo!

5.Au jee wataalam wetu walizidiwa na wingi wa sampuli, wakachoka, ikawa badala ya kupima sampuli zote, wakaamua kucheza mchezo wa ‘ana- ana-do”, hii positive, hii negative, hii positive, hii negative…Sidhani, wala sifikirii kwamba wataalamu wetu walojitolea mstari wa mbele kupigana vita kwa ajili yetu dhidi ya corona eti wafanye hivyo! La hasha! Na kama itakuwa hivyo basi tatizo ni kubwa sana!

Mwisho siku haya yoote ni nadharia kwenye kitendawili cha kipimo cha covid-19 hapa nchini, kitendawili ambacho TUME iliyoundwa na waziri wa afya tutegemee italeta majibu sahihi ili waTanzania turudishe imani kwa majibu tunayopata! Kwa hakika jua litachomoza tena, kutakucha!

Dr. Ally Mahadhy, Department of Molecular Biology and Biotechnology, UDSM

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Niwaombe viongozi wa Jamii Forum kupunguza mada zinazookana wazi kupotosha ukweli wa kisayansi ili kuwaokoa hawa wasaka tonge.

Ahsantenii
Hii taarifa yako ni nzuri sana lakini, nzuri kwa mtu mzuri. Au ni nzuri Kwa JF ya miaka ile. JF ya sasa haina control. Kila kitu kinaamuliwa kwa mtindo wa CCM vs CHADEMA. Hakuna ufahamu na hakuna uelewa. Hata asiyejua RNA na DNA atasema analolijua kuhusu CCM au CHADEMA. Angalia michango ya watu hapa, wengine hata hiyo PCR hawajawahi kuiona lakini hawaulizi. Badala yake wanazomea! Najua wataota sharubu wakiwa JF bila kuongeza uelewa.

Mwishoni umetoa ombi kwa viongozi wa JF. Hawa ndo tatizo kwa sasa. Nionavyo hawako apolitical. Wanajilazimisha kuwa neutral lakini wako na msimamo wa aina fulani. JF ya mwanzo iliondoa au kufuta thd zisizoleta tija na zisizo na ushahidi. Leo hii tunaletewa tetesi, hata kijana wa kindergarten analeta thrd na inachangiwa na wenzake.
 
1589472742312.png

1589472956038.png

Dr. David Nabarro​

THE Special Envoy to World Health Organisation (WHO) and Director-General on Convid-19, Dr. David Nabarro has recommended a COVID-Ready society in which people will learn to live with the virus instead of unending lockdown as a preventive measure having produced no vaccines or cure for the virus.

Nabarro made the statement through his Twitter account stating that unending lockdown may do more harm than good as a result of its effects to people and economies of nations at large.

“This virus is going to be with us for the foreseeable future and nobody wants to go having lockdowns as we have at the moment”

“Covid-19 tracing, containment and neighbourhood health watch will be necessary even once the present wave of outbreaks is gone.

“We have all got to learn to live with this virus, to do our business with this virus in our presence, to have social relations with this virus in our presence and not to be continuously having to be in lockdown because of the widespread infections that can occur”, Nabarro stated.

According to him, establishing a COVIDready state requires the full and willing participation of people, a high level of organization within communities, public health services as well as COVID-Ready hospitals and other health care units.

https://www.carlumegboro.com/2020/0...earn-to-live-with-the-virus-who-boss-nabarro/

Aibu kubwa kwa wengi.
 
Tunasubiri majibu yenye ufafanuzi angalau wa kitaalamu kidogo,lakini siyo yale majibu ya ukipima maji utaonekana mkojo.
 
Back
Top Bottom