Vipimo vya DNA vyaleta kilio kwa 'Wabeba boksi' wanaotaka kuleta familia zao ulaya

Vipimo vya DNA vyaleta kilio kwa 'Wabeba boksi' wanaotaka kuleta familia zao ulaya

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
8,082
Reaction score
17,838
Mzuka wanajamvi

Katika sheria ya haki za binadamu zinaruhusu muamiaji katika nchi zingine uwe mkimbizi wa kisiasa ama unafanya kazi ama kuishi kiuhalali katika nchi nyingine kupeleka familia yake ambao uliiiaacha kwenye nchi yako.

Unaruhusiwa kumleta mke na watoto chini ya mia 16 wako wa damu. Pia nchi nyingi ulaya kama una uraia wao zinaruhusu kuwaleta wazazi wako kama wana miaka zaidi ya 65.

Sasa kwenye watoto kuwaleta lazima wapime DNA kama ni damu yako halali. Na hizi DNA lazima zifanyike na majibu kupatikana kwenye balozi husika.

Vilio na huzuni vimetawala sana kwa wanaume kugundua wamekuwa wakilea na kutunza watoto siyo wao pale wameshafanyya process zote za kuleta familia zao ikibakia tu matokeo ya DNA katika balozi wanaambiwa mtoto ama watoto si wako na balozi kusitisha mara moja visa.

Hii imetokea sana kwa Raia wa Iraq, Syria, Somalia na Ethiopia.

Nchini Ethiopia ambapo kuna balozi nyingi za ulaya na Marekani na Canada zinazoshughulikia raia wa Somalia kwenda nchini mwao kuna Vilio sana na sintofahamu ikifika kupima DNA watoto.

Source rafiki wa karibu sana anayehusika na mambo haya
 
Kama mtu una BP au hasira za haraka usipime DNA, maana unaweza kufa au kuua mtu, ukute umelea mtoto na kusomesha shule za gharama huku ukijinyima mpaka unachekwa na wenzako alafu uje uambiwe si damu yako.
 
Hao wamefanya kama biashara sana kubeba watoto ambao sio wao
Zamani ilikuwa hakuna DNA [emoji3459] na kufanya watu wengi kukubaliwa kuleta watu wao
Wapo walioleta mpaka watoto kumi na zaidi
Ila mambo yamebadilika na magumashi yameisha ni mwendo wa [emoji3459]
Lakini sio kama unavyofikiria
 
Watu wanaogopa kumezwa na wageni wanakutafutia pakukatalia tu
 
Mtu ynakiaje baada ya kupunguziwa majikumu. Yani ito nauli uliyokuwa umeandaa hata mwanamke unamterekeza unatafta mke wa kizungu uko uko maisha yanaendelea na kufa tunakufa mara moja.
 
Kama mtu una BP au hasira za haraka usipime DNA, maana unaweza kufa au kuua mtu, ukute umelea mtoto na kusomesha shule za gharama huku ukijinyima mpaka unachekwa na wenzako alafu uje uambiwe si damu yako.
Kawaida tunapima watoto wakiwa chini ya mwaka mmoja. Wangu pamoja na resistance za mama niliwapima
 
Kama mtu una BP au hasira za haraka usipime DNA, maana unaweza kufa au kuua mtu, ukute umelea mtoto na kusomesha shule za gharama huku ukijinyima mpaka unachekwa na wenzako alafu uje uambiwe si damu yako.
Si unakua umemsaidia binaadam mwenzako? Mungu ndiye atakayekulipa so hata ukimrithisha mali zako inaweza kuwa poa au unaonaje jamani!
 
Back
Top Bottom