Vipimo vya UTI

Vipimo vya UTI

Meridah Tough

Senior Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
136
Reaction score
365
Habarini?

Naomba kufahamu, je vipimo vya UTI vinaweza kuonyesha ujauzito? Na kama vinaweza je hata ujauzito wa siku tano unaweza kuonekana?

Ahsanteni.
 
wajuzi watanisahihisha,

navofahamu Mimi ni kwamba UTI ni maambukizi katika njia ya mkojo na hupimwa Kwa kutumia mkojo na ujauzito hupimwa Kwa kutumia mkojo pia.

ila kipimo cha ujauzito huwezi kutumia kupima UTI na hivyo hivyo cha UTI huwezi kutumia kupima ujauzito.

Maambukizi katika njia ya mkojo hupimwa Kwa kuangalia uwepo wa leukocytes and nitrites kwenye mkojo Kwa kutumia strip maalumu Kwa sehemu zenye uhaba wa vifaa.

Inashauriwa kufanya kuotesha wadudu katika vifaa maalumu (culture) ili kupata majibu yenye uhakika zaidi.

kipimo cha ujauzito hupima uwepo wa hormone iitwayo Human chorionic gonadotropin hormone(HCG -hormone ) ambayo huzalishwa na kuongezeka katika mkojo kipindi mtu akiwa ni mjamzito.

Navofahamu Mimi ni kuanzia wiki mbili na kuendelea lakini unaweza kupima hii hormone kuanzia siku 7 kwenye damu kuweza kufahamu Kwa sababu ...HCG -hormone Una kawaida ya kuongezeka taratibu Kwanza kwenye damu na ikizidi ndo huanza kutoka kwenye mkojo pindi mimba inapozidi kuongezeka.

ko Kwa hapo unaweza pima kufahamu lakini si kwenye mkojo, ni mpaka upime level yake kwenye damu.(serum or plasma)

Nafikiri wajuzi watanisahihisha na kuweka vizuri pasipo Sawa.
 
Back
Top Bottom