Vipindi vichache,wanafunzi wachache,mazingira majanga.

Parata

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
3,090
Reaction score
680
nimepangiwa shule moja huku serengeti near MUGUMU,kiukweli darasa nililopewa lina wanafunzi 17 na ni kidato cha 4.Sehemu hii mazingira yake ya shule ni mazuri kwakua kuna sola ila umeme wa TANESCO hamna,mtaani ndio pabovu na hapaeleweki.Ilikua ni changamoto kubwa sana katika maisha yangu kukutana nayo ila nashukuru Mungu nimepazoea.Katika kuuliza uliza kwangu nikaambiwa mashamba yapo tena bure kwa walimu na viwanja vinauzwa kuanzia elfu hamsini hadi laki 2.Kilichonitia moyo ni usafiri wa uhakika wa kwenda mjini MUGUMU ila gharama ni elfu tatu,tulipokelewa vizuri na tukapewa nyumba ya kuishi,kitanda na godoro.
 
ujue sijaelewa lengo la post yako mwalimu au ulitaka upangiwe kibaha high au azania high?ujue maisha ni popote nzuri zaidi unapopelekwa sehemu cheap kama hizo ukiwa mjanja utatoka kimaisha hivi punde..
 
ujue sijaelewa lengo la post yako mwalimu au ulitaka upangiwe kibaha high au azania high?ujue maisha ni popote nzuri zaidi unapopelekwa sehemu cheap kama hizo ukiwa mjanja utatoka kimaisha hivi punde..

lengo langu ni kutoa taarifa kama nimekosea samahani
 
Wanafunzi 17?
Unafundisha sayansi?

Da!wanafunzi 17 Mbona raha!hakuna kazi hapo Mkuu jamaa apange mishe zake vizuri aone anavyotoka kimaisha.Mwenzio nilikuwa na vipindi A,B,C na D,shule ya kata nilikuwa nawaweka Darasa moja walikuwa wanafika kama 250,sina hata pa kusimama nasimama mlangoni au dirishani kwa nje mwendo wa Lecture nawaswaga kama ng'ombe.
 
lengo langu ni kutoa taarifa kama nimekosea samahani

pouwah kila la kheri kaka jitahidi uweke miradi yakutosha ujue walimu wengi walio mjini wanaish substandard life simply because life expenses in town areas are extremely high to purchase/afford.,you may findout that most teachers in town areas spend almost quarter of their salaries for daily routes..jipange bhana tena ikibidi lima na mpunga afu pia usisahau kuwa phD bongo bado ni wachache
 
miye shule nzima wanafunzima kidato cha kwanza mpaka cha 4 wapo wanafunzi 100 walimu tupo 18 yani full burudani tumepewa nyumba ya kisasa ina solar chakula cha kutosha net work mitandao yote inapatikana nauri toka hapa kijijin mpaka mjini wilayani buku 2 mwendo wa nusu saa kwa kupanda baiskeli kwa piki piki dakika 15 tu so tupige kazi wadau siku tukirudi mijin yello afungue geti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…