Parata
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 3,090
- 680
nimepangiwa shule moja huku serengeti near MUGUMU,kiukweli darasa nililopewa lina wanafunzi 17 na ni kidato cha 4.Sehemu hii mazingira yake ya shule ni mazuri kwakua kuna sola ila umeme wa TANESCO hamna,mtaani ndio pabovu na hapaeleweki.Ilikua ni changamoto kubwa sana katika maisha yangu kukutana nayo ila nashukuru Mungu nimepazoea.Katika kuuliza uliza kwangu nikaambiwa mashamba yapo tena bure kwa walimu na viwanja vinauzwa kuanzia elfu hamsini hadi laki 2.Kilichonitia moyo ni usafiri wa uhakika wa kwenda mjini MUGUMU ila gharama ni elfu tatu,tulipokelewa vizuri na tukapewa nyumba ya kuishi,kitanda na godoro.