Vipodozi Bidhaa Inayopendwa Na Watu, Tushughulike Na Wanunuaji

Sozo_

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2022
Posts
776
Reaction score
1,132
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV vipondozi vinatekezwa na mamlaka husika.

Ninavyojua mtu hawezi kuweka bidhaa kwenye duka lake ikiwa haina soko, tena bidhaa ambayo ni hatari kwake akikutwa na serikali.

Vipodozi hivi vinanunuliwa sana na watu ndio maana vinajazwa kwenye maduka.

Leo tumevitekeza ila kesho mtu anaenda dukani kuulizia, na atahakikisha anavipata.

Tunaweza kudili na wauzaji tukasahau wanunuaji ambao wanaifanya biashara ya vipodozi iendelee kukua.

Wananchi wanapaswa kupewa elimu, mtu akishajua madhara ya vipodozi ataacha kununua. Akiacha kununua muuzaji hataleta bidhaa hatarishi kwenye duka lake.

Tusipotoa elimu tutaendelea kupambana na tatizo juu juu, lakini wananchi wataendelea kuathirika.

Elimu itolewe kwa kina kupitia vyombo vya habari kama yalivyo matangazo mengine.
 
Wewe unadhani hawana elimu au hawajui madhara yake.

Watu wanatafuta kupendeza hayo ya madhara utajua wewe na familia yako.

Ukitaka hili liishe wanaume waache kupenda wanawake warembo na wenye makalio makubwa...hapo ndio soko la hivyo vipodozi litakoma.

#MaendeleoHayanaChama
 
Jua linawaunguza ila hawaachi kutumia, unafikiri hawajui madhara yake, ni sawa na sigara imeandikwa kabisa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako lakini mtu bado ananunua na anatumia
 
Elimu itolewe bila kuchoka, watu wafundishwe uzuri wa ngozi zao.
 
Jua linawaunguza ila hawaachi kutumia, unafikiri hawajui madhara yake, ni sawa na sigara imeandikwa kabisa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako lakini mtu bado ananunua na anatumia
Ujinga ni kitu kibaya sana, wanahitaji elimu
 
Mambo ya cocopulp , citrolight , extraclair , Diana , watakataza sana na mikoa yote itakubali kuacha ila mbeya kwa akina mwafyale itachukua muda kuwaaminisha kuwa weupe sio uzuri hata mweusi ni mzuri pia
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV vipondozi vinatekezwa na mamlaka husika.

Ninavyojua mtu hawezi kuweka bidhaa kwenye duka lake ikiwa haina soko, tena bidhaa ambayo ni hatari kwake akikutwa na serikali.

Vipodozi hivi vinanunuliwa sana na watu ndio maana vinajazwa kwenye maduka.

Leo tumevitekeza ila kesho mtu anaenda dukani kuulizia, na atahakikisha anavipata.

Tunaweza kudili na wauzaji tukasahau wanunuaji ambao wanaifanya biashara ya vipodozi iendelee kukua.

Wananchi wanapaswa kupewa elimu, mtu akishajua madhara ya vipodozi ataacha kununua. Akiacha kununua muuzaji hataleta bidhaa hatarishi kwenye duka lake.

Tusipotoa elimu tutaendelea kupambana na tatizo juu juu, lakini wananchi wataendelea kuathirika.

Elimu itolewe kwa kina kupitia vyombo vya habari kama yalivyo matangazo mengine.
Hivi kweli ni elimu gani ambayo haijatolewa hadi leo hii, haijawaingia watu!!??Huo UKIMWI, tu sasa ni zaidi ya miaka 30, elimu imetolewa mno, lakini kuna baadhi ya maeneo ukienda ni kama hawajawahi kupata elimu ya ukimwi.Waafrika tuna matatizo tu.
 
Itabidi tubadilishe namna ya kutoa elimu, elimu ihamie kwenye nyumba za ibada.
 
Daaa kwa akili zetu nadhani bado kuna kazi tu!!mfano kwenye hizi energy drinks, wameandika kabisa usinywe zaidi ya mbili, lakini sasa vimekuwa kama ndio maji ya kunywa!!watu wanaitaka serikali eti kuingilia kati kuwa vipigwe marufuku!!mbona Redbull imekuwepo miaka na miaka , ila hivi vingine tatizo ni bei yake kuwa ndogo!!!
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari ITV vipondozi vinatekezwa na mamlaka husika.

Ninavyojua mtu hawezi kuweka bidhaa kwenye duka lake ikiwa haina soko, tena bidhaa ambayo ni hatari kwake akikutwa na serikali.

Vipodozi hivi vinanunuliwa sana na watu ndio maana vinajazwa kwenye maduka.

Leo tumevitekeza ila kesho mtu anaenda dukani kuulizia, na atahakikisha anavipata.

Tunaweza kudili na wauzaji tukasahau wanunuaji ambao wanaifanya biashara ya vipodozi iendelee kukua.

Wananchi wanapaswa kupewa elimu, mtu akishajua madhara ya vipodozi ataacha kununua. Akiacha kununua muuzaji hataleta bidhaa hatarishi kwenye duka lake.

Tusipotoa elimu tutaendelea kupambana na tatizo juu juu, lakini wananchi wataendelea kuathirika.

Elimu itolewe kwa kina kupitia vyombo vya habari kama yalivyo matangazo mengine.
Sawa,lakini wadhibitiwe watengenezaji na waingizaji.Ikiwa hivyo hata mhitaji akitaka hawezi kupata.
 
Daaa kwa akili zetu nadhani bado kuna kazi tu!!mfano kwenye hizi energy drinks, wameandika kabisa usinywe zaidi ya mbili, lakini sasa vimekuwa kama ndio maji ya kunywa!!watu wanaitaka serikali eti kuingilia kati kuwa vipigwe marufuku!!mbona Redbull imekuwepo miaka na miaka , ila hivi vingine tatizo ni bei yake kuwa ndogo!!!
Serikali inapaswa kujua necha ya wananchi wake walivyo, wanapaswa kutumia njia ya kuwafikia watu wawape elimu, huenda njia wanayotumia inaonekana haizai matunda.
 
Sawa,lakini wadhibitiwe watengenezaji na waingizaji.Ikiwa hivyo hata mhitaji akitaka hawezi kupata.
Bidhaa yeyote ikiwa na soko wauzaji watatafuta kila njia kuiingiza, dawa ni kukosa wanunuaji.
 
Back
Top Bottom