Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Hasa ukute unakwea midege ya kwenda mbali New zealand huko
 
Duuu forum hii raha jamani ngoja nipumzike kidogo jukwaa la Nifah (sasa).
 
aisee mimi nimejaribu mara kadhaa kucheck-in kupitia zile AUTO TELLER MACHINE Za pale airport lakini zinazingua au zimewekwa pale mapambo tu
 
ndugu andreakalima zile mashine pale nadhan kuna wakati zinafanya kazi ingawa si muda wte na pia si ndege zote unaweza kutumia hizo mashine nafikiri ni zile za "MAANA" kama EMIRATES, QATAR, KLM, SWISSAIR n.k tu na sio FASTJET maana si unatujua sis abiria wa FASTJET tulivyo full watata
 
Clasi hizo pesa ziwekee albamu yake spesheli tu hakuna namna nyingine
 
Mie sikumbuki kioja cha ajabu, zaidi ya kusachiwa kwa masaa Rome na maaskari kisa mtz ameconnect toka dubai
 
dubai ni nafuu kwa nauli (flydubai & Ethiopian) na hoteli pia ni bei poa kuzid hata Nairobi, Cape Town, Kigali
 
Ahmadi! Hatudaiani tena na deni la ndege...nimefuta!! Kwa mara ya kwanza nimekata utepe leo.

Mwezi ujao KLM uelekeo Amsterdam.
 
gharama za usafir arusha to mosh sh ngapi na arusha to dar sh ngap kwa ndege
 

Loh siku ya kwanza itabidi nisafiri na mwenyeji nisije nikatia aibu kwa ushamba huu
 
Mimi siku ya kwanza kupanda ndege nilikuwa nasafiri Dar kwenda Moshi, Mojawapo ya huduma zilizokuwepo ilikuwa mgao wa bia mojamoja kwa anayehitaji!

Nikanywa kwa mapozi nilifikiri nipo kwenye bar! ghafla bia hata haijafika hata robo. Nikadikia tangazo "abiria wote fungeni mikanda ndege inatua"kumbe ilikuwa safari ya nusu saa -dk 45.

Niliaibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…