sitasahau nilipopanda KLM hadi schipol/amsterdam uholanzi, nilikuwa naunganisha kwenda nchi nyingine ya ulaya. wiki hiyo kuna kijana gaidi wa nigeria alikamatwa anataka kulipua ndege ya delta ya wamarekani, hivyo mwafrica yeyote akionekana alikua akapekuliwa vilivyo.
huwezi amini, tulikuwa tumeongozana na wazungu wengi, lakini walipoona ngozi nyeusi tena inatoka africa, waliniweka pembeni wakaanza kukagua doc zangu zote polepole. they really humiliated me, askari mmoja akamwambie mwenzie "mwache uyo dogo hana tatizo", ndio nikaachiwa, lakini hata hivyo hawakuamini, mizigo yangu badala ya kupakiwa kwenye ndege yangu (kwasababu nilishachelewa ndege niliyotakiwa kuunganisha interval ya lisaa limoja) mizigo ilibaki, nilipata extension ya shirika lilelile la ndege bila malipo lakini kwa kupitia ufaransa na nikafika kwa kuchelewa masaa matano, ratiba yangu yote imevurugika.
nilipofika airport yangu yamwisho nilikuwa kuna kifurushi wameweka dawa za mswaki, tshirt ya shilika la ndege na kisuruari wakaniambia nitatumia kuvaa, ila niache address ya wapi nitakaa. drive from the airport hadi mtaa niliokuwa naenda kuishi ni nusu saa. nikaondoka. kesho yake, askari walileta mabegi yangu yote. kuangalia, kumbe waliyachelewesha ili wayakague.
HAPO NDIPO NILIPOONA UBAGUZI na ukatili wa wazungu. Mungu awasamehe......