Mimi siku ya kwanza kupanda ndege nilikuwa nasafiri Dar kwenda Moshi,Mojawapo ya huduma zilizokuwepo ilikuwa mgao wa bia mojamoja kwa anayehitaji!Nikanywa kwa mapozi nilifikiri nipo kwenye bar! ghafla bia hata haijafika hata robo. Nikadikia tangazo "abiria wote fungeni mikanda ndege inatua"kumbe ilikuwa safari ya nusu saa -dk 45.Niliaibika.
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
Niko Primary dadangu akapata safari ya uingereza.(Kipindi hicho tunasema ulaya v haijalishi hata kama umeenda Marekani). Hakuna yeyote alowah kusafir na ndege kwetu mpk muda huo achilia mbali kwenda nje ya nchi tu. Bana weh,
1.Alishonesha suti kwa fundi kama ya sarafina pale wakati movie inaisha.
2. Tulikodi tax tatu kumsindkiza airport.
3. Mzee alituma nauli kwa shangazi na bibi wiki moja kabla ili watoke Mbeya kuja kumsindikiza dada airport.
4. Pale airport tukajipanga warefu nyuma, wafupi wachuchumae, tukapga picha. Ni moja kati ya picha dada hazipendi sana leo akikumbuka tulivokuwa washamba.
Hahahahaaaa Hihihihiiiii Huhuhuhuhuhuuuh atiii nini? Ndege hahaha nimecheka sn
Stak ata kukumbuka maana nusu nijikojolee.... Hahaaahaa 2010 mweeh
teh teh teh uwiiiii mbavu zangu mie mtoto wa marehemu!!!!
Mie nilikusanya vitambulisho vyote mpk vya drs la saba, birth certificate mpk death certificate za wazazi wng nikidhania ukifika kwenye mlango wa ndege unakaguliwa!!
Nikajisemea moyoni wakikataa hiki natoa hiki!!! mweeee ama kweli ushamba mzigo...
Mie mbona sitasahau,,,,,,,,,,
cku iyo nilijipodoa kama naenda harusini kufika airport parfume yng ikawekwa kwny dustibini niliumia sana.............
nilipoingia ndani sijui ni uoga nikaita air host aje kunifunga mkanda kasheshe wkt wa kushuka mkanda ukanishinda kufungua ikabidi jirani yng kk mmoja anisaidie..
tinna cute pole sana. mimi perfume na dawa za mswaki zilitupwa kwenye waste bin ile kufika kwa jamaa wa uhamiaji wananiuliza vipi mkuu unaenda kufundisha KISWAHILI ughaibuni? sijui nnimekaa kama mwalimu. Mwishoni akamalizia kwa kuomba hela ya Chai UHAMIAJI AIRPORT punguzen njaaa.
hahhhhhahhahahahahahahaah!!!!!!!!!!!!!!!! bujibuji umefunika mwanangu!
Mimi niling'ang'ania kuingilia pale inapoingia mizigo sikupenda kabisa kutenganishwa na mizigo yangu.Halafu nilikosea mlango wa chooni nikaingia kwa rubani dah!
aisee mimi nimejaribu mara kadhaa kucheck-in kupitia zile AUTO TELLER MACHINE Za pale airport lakini zinazingua au zimewekwa pale mapambo tu
Mm kiukweli Swissair ndo naizimikia haswaaa