mkuu jimena la muhimu ni kujipanga mimi nimejipanga xmass mwakani 2016 lazima nikasherehekee ZURICH, USWISI hapa nimeshafungua akaunti ya dola kila mwezi naweka 150 USD halafu viji-allowance mshenzi vya kushtukiza natumbukiza humo kwenye akaunti humo.
TANGAZO: Kwa wafanyakazi wa Umma unapaswa kukaa mita 200 toka airport ilipo yaani in short usikaribie uwanja wa ndege. Hapa MABASI tu
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.
Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.
Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.
Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.
Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
Hata kama ni rubani !! Masaa laki moja ni miaka 11!!!
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
Unawaonea sana Wanyakyusa!!Fastjet ndo ametutoa kimaso maso tulio wengi humu. Ila watu wa Mbeya wao washukuru zaidi FASTJET kwa kubakia ndege pekee inayotua SONGWE AIRPORT vinginevyo wangeishia kuiona Dar kwa usafiri wa FUSO (Samahani lakini).
Hahahaha tutake radhiFastjet ndo ametutoa kimaso maso tulio wengi humu. Ila watu wa Mbeya wao washukuru zaidi FASTJET kwa kubakia ndege pekee inayotua SONGWE AIRPORT vinginevyo wangeishia kuiona Dar kwa usafiri wa FUSO (Samahani lakini).
Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka mimi nikajipa kama dakika 20 hivi ndo niwe Airport duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichoka. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege.
**NEW DEVELOPMENT
Mwezi Juni 2015 nilipata safari ya kwenda CAMEROON (kwa hisani ya Watu wamarekani USAID) sasa tukiwa huko tukalipwa posho kwa hela ya huko Central African Franc sasa nikazibana nije kubadilishia Bongo nafika bongo Bureau De Change zote hawabadilishi hizi pesa yaani nmepagawa sijui nikazitupe Coco maana....
HAKIKA USHAMBA MZIGO!
Kuna dada nilikaa nae siti 1 ndani ya Qatar airways na ilikua mara yake ya kwanza kupanda ndege. Tupo anga za mbali huko mdada mashetani yaka mpanda yani ilikua balaa ,alipigiwa maombi na watu wa dini zote kuanzia waarabu, wahindi, wazungu mpaka blackys. Crazy