Virusi vya Corona: Hatua za udhibiti zalegezwa Afrika Kusini, huku maambukizi yakipungua

Virusi vya Corona: Hatua za udhibiti zalegezwa Afrika Kusini, huku maambukizi yakipungua

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Afrika Kusini ilitekeleza amri ya kutotoka nje tarehe tarehe 27 MachiImage caption: Afrika Kusini ilitekeleza amri ya kutotoka nje tarehe tarehe 27 Machi

Afrika Kusini, ambayo ilikuwa ni moja ya nchi zilizochukua hatua kali mapema zaidi duniani za kukabiliana na kusambaa ka virusi vya corona, imetangaza kulegeza zaidi hatua hizo dhidi ya viusi hivyo.

Kuanzia tarehe 20 Septemba amri ya kutotembea nje usiku itapunguzwa, mikusanyiko itaruhusiwa kwa 50% ya uwezo wa maeneo ya mikusanyiko , na pombe zitauzwa tena.

"Tumevuka dhoruba la virusi vya corona," alisema Rais Cyril Ramaphosa katika hotuba yake ya televisheni.

Lakini sheria za kukaa mbali na uvaaji wa barakoa zitaendelea.

Afrika Kusini ambayo iliingia katika kipindi cha sheria ya kukaa nyumbani tarehe 27 Machi – hadi sasa imeripoti zaidi ya maambukizi 650,000, ikiwa na vifo zaidi ya 15,000.

Hatahivyo, idadi ya maambukizi mapya imepungua hadi 12,000 kwa siku katika mwezi wa Julai walikuwa chini ya 2,000.
 

Attachments

  • 1600346828475.gif
    1600346828475.gif
    42 bytes · Views: 2
Back
Top Bottom