Masi Lambo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 532
- 360
Haki miliki ya pichaUNIVERSITY OF PITTSBURGH
Bing Liu, profesa msaidizi mwenye miaka 37 katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Pittsburgh, Marekani alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake siku ya Jumamosi.
Wenzake walisema alikuwa karibu kupata "matokeo muhimu" ya tafiti kuhusu Covid-19, tukio lililosababisha kuwepo kwa maoni mitandaoni yanayoeleza kuwa yawezekana bwana Liu aliuawa lakini polisi wanasema ni tukio la kujiua.
Kwanini Liu aliuawa?
Alikutwa akiwa na majeraha mengi ya risasi kichwani, shingoni katika eneo la Pittsburgh yalipo makazi yake kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo.
Mtu aliyekuwa na silaha alitambulika kuwa na miaka 46, mhandisi wa programu ya kompyuta, Hao Gu. Mamlaka zinasema muuaji naye alijiua baada ya kurudi kwenye gari lake.
Liu na Gu walikuwa wanafahamiana, maafisa wapelelezi wa mauaji walieleza.
Uchunguzi umebaini kuwa lilikuwa tukio la kuua na kujiua lililotokana na ''mgogoro wa muda mrefu wa masuala ya kimapenzi''.
Wamesema ''hakuna ushahidi'' wa kuhusisha tukio hilo na utafiti wa Liu na mazingira ya sasa ya changamoto za kiafya.
Liu ni nani?
Katika taarifa yao , wenzake wamemwelezea kama mtafiti wa kipekee ambaye ''alikuwa ukingoni kufanikisha kupata matokeo muhimu '' ya kuelewa maambukizi ya Covid-19.
Waliomboleza kifo cha Liu na kuahidi kumalizia utafiti wake ''zikiwa ni juhudi za kuenzi ubora wake katika uwanja wa kisanyansi''.
Liu, raia wa China alipata shahada yake ya kwanza na shahada ya uzamivu katika masomo ya sayansi ya kompyuta nchini Singapore kabla ya kufanya utafiti nchini Marekani.
Aliwahi kuungana na wanabaiolojia wengine kufanya utafiti kuhusu kinga ya binaadamu, kwa mujibu wa wasifu wake mtandaoni.
Yanayozungumzwa mitandaoni
''Mungu wangu'' mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijamii wa Weibo aliandika. '' Labda alibaini kuwa virusi vilitengenezwa kwenye maabara nchini Marekani.''
Maoni kama hayo yalieleza kuwa Liu aliuawa kwa sababu pengine aligundua chanzo cha virusi vya corona.
Maafisa wa China na vyombo vya habari vya habari vya serikali vilisema kuwa madai yakuwa virusi vilitengenezwa Marekani na kupelekwa Wuhan na wanajeshi wa Marekani hayana msigi.
Wengine walisema ni tukio ambalo lina sababu iliyojificha.
''Inawezekana kuwa kuna siri iliyojificha gizani''. Alieleza mtu mmoja kwenye mtandao huo.