Virusi vya Corona: WHO yasitisha majaribio ya dawa ya Hydroxychloroquine na kutoa onyo

Virusi vya Corona: WHO yasitisha majaribio ya dawa ya Hydroxychloroquine na kutoa onyo

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Majaribio yanayofanyiwa dawa ya ugonjwa wa malaria Hydroxychloroquine ili kuona iwapo inaweza kutibu virusi vya corona yamesitishwa kutokana na hofu ya usalama wake, shirika la afya duniani WHO limesema.

Vipimo vilivyokuwa vikifanywa katika mataifa kadhaa vimesitishwa kwa muda kama hatua ya kuchukua tahadhari, lilisema shirika hilo siku ya Jumatatu.

Hatua hiyo inajiri baada ya utafiti wa tiba uliofanyika hivi karibuni kusema kwamba dawa hiyo inaweza kuongeza hatari ya mgonjwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

Rais Donald Trump amesema kuwa anatumia dawa hiyo kuzuia virusi hivyo.

Rais huyo wa Marekani ameikuza dawa hiyo ya malaria, kinyume na ushauri wa kimatibabu na onyo kutoka kwa maafisa wa Afya kwamba inaweza kusababisha tatizo la moyo.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins vifo vilivyotokana na corona vimefikia 98,218.

Wiki iliopita, utafiti uliofanywa na jarida la tiba duniani Lancet ulibaini kwamba hakuna faida yoyote kwa kutumia dawa ya Hydroxychloroquine na kwamba utumizi wake unaweza kuongeza idadi ya vifo miongoni mwa wagonjwa hospitalini walio na maambukizi ya corona.

Hydrochloroquine ni dawa salama ya kutibu ugonjwa wa malaria, baridi yabisi na Lupus, lakini hakuna majaribio yoyote ambayo yamependekeza matumizi yake kutibu Covid-19.

Watafiti wanasemaa kwamba wagonjwa wa Covid-19 hawafai kutumia hydroxychloroquine.

Shirika la Afya duniani linafanyia majaribio dawa kadhaa kuona iwapo zinaweza kutibu ugonjwa huo mbali na kuripoti kwamba baadhi ya watu binafsi wamekuwa wakitumia dawa hiyo na hivyobasi kujisababishia madhara makubwa.

Siku ya Jumatatu, maafisa katika shirika hilo la Umoja wa Mataifa walisema kwamba hydroxychloroquine itaondolewa katika majaribio hayo kwa muda ili kuruhusu uchunguzi wa usalama wake.

Utafiti huo wa Lancet ulihusisha wagonjwa 96,000 wa virusi vya corona ambapo kati yao 15,000 walipatiwa dawa ya Hydroxychloroquine ama ile inayohusishwa na Chloroquine , pekee ama na dawa ya antibiotic.

Utafiti huo ulibaini kwamba wagonjwa hao walikuwa na hatari kubwa ya kufariki hospitalini na kupatwa na tatizo la moyo ikilinganishwa na wagonjwa wengine wa Covid-19.

Hatari ya mgonjwa anayetumia hydroxychloroquine kufariki ilikuwa asilimia 18, asilimia 16.4 kwa waliotumia Chloroquine na asilimia 9 kwa kundi jingine.

Wale waliotibiwa na hydroxychloroquine au chloroquine kwa mchanganyiko na dawa ya antibiotic walikuwa na hatari ya juu zaidi kufariki.

Watafiti hao walionya kwamba Hydroxychloroquine haifai kutumiwa kando na majaribio hayo.
 
Naona jinsi Dr. Tedros na WHO yake wanazidisha mgogoro na Trump na Marekani. Maana Rais Trump alitangazia dunia kwamba yeye binafsi amekuwa anaitumia hiyo dawa na kusisitiza wataalamu wake waendelee kuitumia. Sasa kwa taarifa hii ya WHO maana yake mgogoro huu ndio unaanza upyaaaa...
 
VP walisemaga ile Madagascar iwekwe sumu Kwa kuahidiwa dola mil. 20. Nani anawaamini hao WHO
 
1590480371147.png

Shirika la Afya ulimwenguni WHO, limesema linaahirisha majaribio ya dawa ya hydroxychloroquine kama tiba ya ugonjwa wa COVID-19.
Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema wanachunguza usalama wa dawa hiyo.

Uamuzi huo wa WHO umefikiwa baada ya ripoti ya wanasayansi iliyochapishwa katika jarida maarufu la kitabibu la The Lancet wiki iliyopita, ikisema matumizi wa hydroxychloroquine yalikuwa yakizidisha hatari ya kufa miongoni mwa wagonjwa wa COVID-19, amesema mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya video jana jioni.

Tedros alisema kile kinachofahamika kama 'mshikamano wa majaribio' kinachohusisha mamia ya hospitali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikiijaribu dawa hiyo kwa wagonjwa wa virusi vya corona kimeacha majaribio hayo kama hatua ya tahadhari tu. Mkuu wa huduma za dharura katika shirika la WHO Mike Ryan amesisitiza kuwa hakuna matatizo mengine yaliyojitokeza.

Ingawa dawa hiyo awali ilitumiwa kutibu malaumivu ya misuli, baadhi ya watu, rais Donald Trump wa Marekani miongoni mwao, wamekuwa wakiipigia debe kama tiba kwa virusi vya corona, na nchi kadhaa zimekuwa zikiiagiza kwa wingi.

Wiki iliyopita, waziri wa afya wa Brazil alishauri matumizi ya dawa hiyo, pamoja na nyingine ya Chloroquine inayotibu malaria, kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19.
 
Kwanini wasimuulize Magufuli amefanyaje kushusha idadi ya wagonjwa na hatimaye anamshukuru Mungu?
 
Baada ya Professor Kabudi kupeleka muongozo wetu wa kukabiliana na corona Tanzania, mbona WHO hawaja sufu jitihada zetu? Mawazo na elimu ya juu ya jembe let’s Rais Dr JPM.
 
Back
Top Bottom