Virusi vya ukimwi na ukimwi (insight) PART 1.

beric

Member
Joined
Feb 24, 2013
Posts
41
Reaction score
14
Ndugu,
Katika mfululizo wa elimu hii, nitakuwa nagusia Nyanja zote, na nitapitia kila kipande cha somo tofauti ili wasomaji mpate nafasi ya kuuliza maswali na maswali hayo yajibiwe.
KARIBU
PART 1: VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI
A. VIRUSI VYA UKIMWI
Virusi kwa ujumla
Virusi ni vijidudu vidogo Zaidi vinavyosababisha maambukizi, kuna aina tofauti za virusi kwa ujumla ila zote huwa na vinasaba vya RNA na DNA. Kirusi cha aina moja chaweza kuwa na RNA au DNA tuu na si vyote viwili. Ili nieleweke, nitaeleza kinagaubaga kuhusu RNA na DNA.
DNA (deoxyribonucleic acid) – asidi kiinideoksiribonukleik.
Hii ni molekuli inayobeba virithishi vya viumbe hai, ndivyo vinavyounda na kutunza habari muhimu za urithi wa kiumbe. Hizi ndizo taarifa za seli zinazoiwezesha kuzalisha protini muhimu za mwili au seli husika. Protini hizi hutunzwa kama (code) taarifa za siri zinazotambulika kwa kutafsiri (code) hizo wakati wa kutengeneza protini husika. Kila protini ina mfuatano wa (code) husika na code hiyo ikitafsiriwa hutoa protini iliyokusudiwa tuu. Hivyo virusi vyote huhitaji katika hatua Fulani kubadilika kuwa DNA ili iweze kutengeneza protini zake muhimu tutakazoziongelea baadae tutakapoanza kuongelea Virusi vya UKIMWI.
DNA huweza kujinakili na kutengeneza DNA nyingine inayofanana nayo. Hii hutokea pale seli inapozalisha seli nyingine. Hufanya hivyo kwa kujipasua kwa kutumia protini zilizotengenezwa na ni njia hii pia ambayo virusi hutumia kujizalisha. Inaitwa DNA kwa sababu huwa ni mbili zikiwa kwenye shapu ya ngazi iliyojifunga madhubuti. Ngazi hii hujifungua pale DNA inapojizalisha.

RNA (ribonucleic acid) – asidi ribonukleik
Hizi pia ni vinasaba muhimu vya kutengeneza protini. Kwa kawaida RNA hutengenezwa kutoka kwenye DNA. Mana yake ni kwamba RNA haziwezi kujizalisha kama inavyofanya DNA, hivyo, ili kirusi cha RNA kijizalishe, ni lazima kijiweke kwenye mfumo wa DNA ndipo izalishe copy zake. Hatua hiyo hufanyika ndani ya seli na hutumia seli husika kupata vitu muhimu vya kutengeneza DNA na kutengeneza copy zake.

VIRUSI VYA UKIMWI
Ni aina ya virusi vinavyopatikana katika kundi la RETROVIRUS. Virusi hivi ni RNA, hivyo kama nilivyosema, ili vizalishane, ni lazima kwanza vijitengeneze kuwa DNA kwa kutumia kiwezeshi kinachoitwa Reverse transcriptase. Hii ni protein wezeshi zinazoitwa enzyme ambazo huiwezesha hii RNA ya virusi vya ukimwi kubadilika na kuwa DNA kwa kutumia na kufaikia kutitia seli ambayo hiki kirusi kimevamia. Sitaingia kwa undani kwa sababu ya ugumu wa somo lenyewe kwa hadhira ambayo nategemea mpaka hapa nimeshasema vitu vivyoeleweka kwao. Kwa wenye nia tafadhali some vitabu.
Virusi vya ukimwi hukaa katika majimaji yote ya mwili, hivyo hata maambukizi yake hutegemea hili. Huzaliana pale tuu vinapoingia kwenye seli. Kwa kei hii, ni seli za kinga ya mwili zinazoitwa CD4. Hizi ni celi za kinga za mwili aina ya Helper T cells na huzaliana ndani ya seli.
NJIA ZA MAAMBUKIZI
Virusi vya ukimwi huambukizwa kwa njia zifuatazo:
1. Njia ya ngono;
Hii ni njia inayoongoza kwa maambukizi, kwanza ieleweke virusi hupatikana kwenye majimaji yote ya mwili. Kwa upande wa seli ni seli aina ya Helper T cell pekee. Sababu ni kwamba VVU vinahitaji kipokeaji (receiptor) maalum inayoiwezesha kuingia kwenye seli. Hivyo maambukizi kwa njia ya ngono ni kutokana na majimaji yenye virusi kupata sehemu yenye kidonda kiasi cha majimaji hayo kugusana na majimaji/damu ya mwili wa mtu asiye na virusi.
Zifuatazo ni hali ambazo lazima ziwepo ili maambukizi kwa njia na ngono itokee.
• Lazima asiye na maambukizi awe amechubuka hivyo kuruhusu majimaji yenye virusi kugusana na damu ya asiye na maambukizi.
• Si lazima kwa mwenye maambukizi apate mchubuko, maana manii au majimaji ya uke huwa na virusi.
• Ikiwa asiye na maambukizi hana mchubuko wa aina yoyote ule, haiwezekani kuambukizwa virusi. Lakini kwa kuwa ngono ni kitendo cha msuguano, ni gumu kusema hukupata mchubuko.
Zifuatazo ni ukweli kuhusu maambukizi kwa njia ya ngono;
• Mbegu za kiume hazina virusi, ila manii ( semen) ndiyo huwa na virusi, majimaji mengine yenye virusi ni kama mate, damu n.k.
• Huwezi kw kumshikshika mtu aliye na maambukizi bila majimaji yake kugusana na damu au kidonda chako.
• Ngono inayohusisha mkundu (anal sex) huongeza uwezekano wa maambukizi kwa kiasi kikubwa kwani kwa asilia hakuna ulowanisho unaokuwepo kama kwenye uke, hivyo huongeza uwezekano wa mchubuko kutokana na ngozi ya uume na mkundu ni laini sana.
• Inawezekana kabisa kufanya ngono na mtu mwenye maambukizi na usipate maambukizi kama hakutakuwepo kwa michubuko. (ila jua penye msuguano mchubuko ni rahisi sana kutokea).

2. Njia ya mama kwenda kwa mtoto.
Kwanza kwa kuwa nimesema hata kama mama ana maambukizi, yai la uzazi la kike haliwezi kubeba maambukizi kama nilivyosema hapo juu kwa kuwa halina (receiptors). Vivyo hivyo kwa mbegu ya kiume. Lakini pia mzunguko wa damu wa mama na wa mtoto zimetofautishwa na havigusani kwa namna yoyote isipokuwa ikitokea tatizo.
Njia za maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hutokea:
i. Wakati wa ujauzito;, ikitokea mama mjamzito amepata tatizo linalopelekea damu ya mtoto kugusana na damu ya mama mtoto akiwa tumboni, mfano, abrutio placenta, etc,
ii. Wakati wa kujifungua;, kwa kuwa kuzaa ni kitendo kinachohusisha mtoto kupita kwenye kiungo cha mama, na pia kondo ya nyuma kuachana na mama, yawezekana mtoto akachubuka, au wakati wa kukata kondo la nyuma damu ya mama na ya mtoto ikagusana hivyo kupelekea maambukizi.
iii. Wakati wa kunyonyesha;, nilisema maji yote ya mwilini hubeba virusi, hivyo maziwa ya mama huwa yana virusi pia ikiwa mama ana maambukizi. Lakini kwa kuwa njia ya chakula ya mtoto inakuwa haina mchubuko, mtoto hupata maambukizi ikiwa njia yake ya chakula itapata mchubuko mfano, kutumia vyakula vya ziada kabla njia ya chakula haijawa tayari, i.e kabla ya miezi sita (6).
3. Kujichoma sindano au kujikata na kitu cha ncha kali alichotumia mtu mwenye virusi vya ukimwi.
Hii hutokea sana kwa hatoa huduma wanapojichoma kwa bahati mbaya wakati wa kutoa huduma, hii ni kwa sababu ile sindano kwa mfano au wembe utakuwa na mabaki ya damu ya mgonjwa mwenye maambukizi, hivyo kwa kuwa kajichom, atakuwa amepeleka damu hiyo mwilini mwake.
Wengine wenye hatari ya maambukizi kwa njia hii, ni wale wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujichoma na kushirikishana sindano hizo.
4. Kung’atwa na mtu mwenye maambukizi, mara chache sana,
5. Ngono ya mdomoni, oral sex, pia mara chache,
6. Kugusana kidonda na mtu mwenye maambukizi
7. Kula chakula kilichotafunwa na mtu mwenye maambukizi, mfano watoto wachanga wanapolishwa kwa njia hii, na mtoto ana vidonda mtomoni.
Kwa leo tuishie hapa, itakayofuata ni UPIMAJI WA VIRUSI VYA UKIMWI NA MAJIBU, NA MAJIBU KWA MASWALI.
 
Ok. Inamaana ukimwandaa mwenza (ambaye ameathirika) vizuri kabla ya kupiga mechi bado kupo uwezekano mkubwa wa kuukwaa?
 
Uwezekano upo bado

Sababu ni Kwamba uwezekano wa mchubuko bado upo. Kwani hata mchubuko ukiwa mdogo kiasi gani, bado kutakuwa na uwezekano wa majimaji kugusana
 
Kwakifupi, wengi tumepotoka juu ya hilo.

Ni kweli maandalizi mazuri hupunguza chance ya maambukizi. But haiondoi kabisa uwezekano. Ndio maana tunashauriwa kuendelea kutumia condoms kwa usahihi
 
Always HIV is contradicting and its difficult to defend this kind of conspiracies & fallacies to individual with higher level of thinking.....
I don't need any kind of question unless is common phenomenon to this platform.
 
Always HIV is contradicting and its difficult to defend this kind of conspiracies & fallacies to individual with higher level of thinking.....
I don't need any kind of question unless is common phenomenon to this platform.
Always sounds like a ballad passed through generations. Very contradicting to people with hyper reasoning capabilities. I've decided to hit the exit button whenever i meet with such kind of stories, decided to stick to my instincts.
 
Ebu tutolee upuuZ wako ulokaririshwa na wakoloni!huna aibu?
 
 
Ndiyo reality. Huwezi kuondoa uwezekano wa mchubuko kwa asilimia 100
Mkuu asante kwa kutupatia elimu hii, Mungu akubariki sana, naomba kuelimishwa kidogo, hivi ukiachana na mchubuko, ulishasema majimaji ya ukeni yanakuwa na virusi, je maambukizi hayawezi kupitia kwenye mrija wa uume ukiachana na mchubuko???
Kwani umetuambia kuwa manii yanabeba virusi sasa manii yakikutana na manii ya mwanamke aliye athirika wakati wa tendo hapo inakuwaje?
 
Mkuu asante kwa kutupatia elimu hii, Mungu akubariki sana, naomba kuelimishwa kidogo, hivi ukiachana na mchubuko, ulishasema majimaji ya ukeni yanakuwa na virusi, je maambukizi hayawezi kupitia kwenye mrija wa uume ukiachana na mchubuko???

Hapana haiwezi
 
Hapana haiwezi

Kama nilivyosema, lazima kuwepo na mgusano kati ya majimaji ya mwenye virusi na damu ya asiye na virusi. Miirija hiyo ina layer inayouitwa epithelium. Hii layer in seli maalum ambazo hazina kipokezi(receiptor) inayoweza kupokea virusi. Hivyo ni lazima iwepo mgusano na seli zenye uwezo huo. Seli hizo zipo kwenye damu na huitwa CD4 au helper T cell
 
Aisee asante kwa darasa hili zuri sana
 

Mkuu zamani miaka ya mwishoni ya 80 kuna ndugu yangu ilisemekena alifariki kwa huu ugonjwa lakini ktk cheti chake cha kifo sababu ya kifo chake imeandikwa ARDS,nikagoogle nikaona wameandika Aids Related Disease,sasa naomba niulize inawezekana kweli atakuwa alifariki kwa ugonjwa huo?,manake nakumbuka hardly aligua kwa wiki 3 tu,baada ya hapo akafariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…