mimi nina MASTER CARD,niko nje ya nchi.Ninapokua bongo huwa natumia ATM ya Barclays pale OHIO STREET.Kila unapoweka card yako ndani ya ATM in one turn unaweza kuchukua 400,000shs.Lakini unaweza kuweka card yako as many times as you can on the same day,ikitegemea benki yako inakuruhusu uchukue pesa ngapi kwa siku.Mfano,benki yangu hapa Ugaibuni inaniruhusu kwa siku kutoa kwenye ATM nikitumia card yangu amount ambayo ni equivalent na kama milion tano za kitanzania.Kwa hiyo,siku moja nikiwa Tanzania,nililiweza kutumia MASTER CARD yangu pale Barclays,nkachukua milioni tatu na laki mbili kwa siku moja maana Bank yangu ya ughaibuni inaniruhusu hadi equivalent ya kama milion 5 per day kwa ATM.Nilichokua nafanya,nilikua naweka jadi ndani ya ATM nachukua laki 4,then nangoja kama dakika moja naingiza tena card nachuku a tena laki 4.Niliingiza kadi mara nane ,nkachukua a total of 3,200,000tshs.
Na hii nimefanya si mara moja kuna siku nilichukua kama milion2 per day.
Kuna siku nilichukua milion 1 per day.
sasa kwa kua kadi yako ni VISA CARD,na nina uhakikia ATM za Barclays zinakubali VISA CARD,basi hiki nilichofanya mimi,pia kwako nina hakika kinawezekana kwa asilimia mia.
Sasa pale Barclays OHIO STREET,OPPOSITE NA MOVENPICK HOTEL,wana ATM tatu.
ATM mbili ziko nje,ATM moja iko ndani.ATM za nje wameandika zinapokea VISA na MASTER CARD,lakini kwa sasa wameziblock,hazipokei VISA au MASTER CARD inayotolewa na BENKI isio bongo,ukiweka kadi yako,ATM itasema imeshindwa kuisoma.Kwa hiyo tumia ATM ya ndani ya BENK.Hiyo itakupa pesa bila wasiwasi kabisa.Utakachofanya,ni kuingia ndani ya BENK,kuwaambia wafanyakazi kuwa unataka kutumia ATM ya ndani mana ya nje imekataa,Watakuruhusu.
Kumbuka pia kwamba,inaweza benk yako ya ughaibuni ikawa inakuruhsu kuchukua kwa ATM mfano pesa ambayo ni sawa na milion tano za bongo kwa siku.Lakini unaweza kwenda Barclays,ukachukua mfano laki nane[yaani laki nne in two turns},then ukataka kuchukua tena laki nne mashine ikashindwa kukupa pesa,Hii hutokea ikiwa ATM inakuwa imeishiwa pesa.Hivyo,kama unataka pesa nyingi kwa siku moja,mimi huwa naenda asubuhi sana bado ATM ikiwa bado inapesa ya kutosha.
Pia ATM ya BARCLAYS inakundikia kuwa in one turn unaweza toka laki 4,Lakini usishangae siku moja unaweka kadi yako,unacommand ATM ikupe laki nne,then ATM ikasshindwa.Hii hutokea kama ndani ya ATM kwa siku hiyo wameweka pesa in terms of noti za elfu tano [badala ya noti za elfu kumi},hivyo laki nne kwa noti za elfu tano,unakuwa mzigo mkubwa kiasi kwamba hauwezi kupita kwenye eneo la ku release pesa la ATM,ukiona hivyo,basi komandi ATM ikupe laki mbili,na mambo yatakua ok.
Lakini ninakushauri,ikiwa ATM itakubali kukupa laki nne kila unapoweka kadi,basi tumia option hii ya laki nne .Kwa maana ukitumia option ya laki 2,utalazimika kuweka kadi mara nyingi kama unahitaji pesa nyingi{mfano kama unataka 3,200,000 utaweka kadi mara nane} na in every turn unapoweka kadi na kuchukua pesa,unalipia hiyo gharama [mfano kwa benki yangu,ikiwa nachukua pesa ATM nje ya nchi niliyopo kwa sasa,basi in every time ninapoweka kadi na kuchukua pesa wanani charge pesa ambayo ni sawa na kama shs 7,000 za TANZANIA]/
natumai umenipata vema sana.Haya maelezo nina hakika nayo kwa asilimia mia,,maana mimi nimekuwa nikifanya hivyo mara nyingi as lately as November 2009.
Kama kuna kitu hujanipata vema,usiwe na tatizo kuniuliza mkuu.
Mungu akubariki.
THE SON OF AFRICA a.k.a KIJANA WA KIJIJINI