Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo


Chuki binafsi

Mambo ni [emoji3533][emoji3533]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app


Mkuu una mawazo kama yangu

We boya jiheshim hata kama kumkosoa mtu sio unamkosoa kikuda hivyo....kama nawew unaumizwa na uzi huu tafuta namna nyingine sio kumshambulia mleta uzi kama hayawani

Kama vipi walete Hao walikuwa kukutukana si wasubirie ama hawana kazi za kufanya kazi yao ni kusoma nyuzi za kichawi tu. Kama wanataka kuburudika kuna viburudisho

Niweke siti kbs

Usitishike mkuu ..leta info hizo..

mkuu huyo hataki tu kukbali ukweli ujiji kupo kishamba kutokana na wafia dini na ushirikina, Mwanga kumeendelea zaidi

Kuna jamaa anatokea huko siku moja aliniambia ili ujiji kuendelee zinahitajika bar na guest zifunguliwe lakini wazee wa huko hawataki , si ruhusa kufungua biashara hizo.

true mkuu nilienda kikazi kule baa na gesti zipo mwanga kukle ujiji unafanya kazi kutwa kupumzika ni mwanga, mwenyeji mmoja alituambia kuna mtu alifungua baa akakomaliwa mpaka akaifunga

Part 4 bado?

Soma story uelewe usikurupuke kenge wewe ujue mnakela Sana na miswali ya kipumbavu

Wasikupotezee mda wako hapa twende Telegram ukaungane na Lwanda kule ni full raha

PART IV TAYARI.
 
Huenda ulichukua msukule ukaacha mtoto halisi ndio maana alikutimua.
 
Hapo ndio mpaka mwakani tena.....
 
PART V

Kurudi mwenge kwa jamaa akanambia nitafute maisha mengine yeye alishasaidia nimepata uzoefu.

Nikarudi Kariakoo kutafuta kazi.baada ya siku chache nikapata kwa mhindi mmoja.nlifanya naye kazi yule mama na mumewe. Nao walikuwa wakifungua duka asubuhi mimi natakiwa nisubiri nje.wakimaliza ndo wananiita.

Wale wahindi walikuwa watu wa ibada sana, ila cha kushangaza sasa asubuhi ilikuwa mteja yeyote akija wa kwanza kama anataka kitu lazima auziwe. Hata kwa bei nusu.hamna mteja wa kwanza kuondoka bila kununua kitu. Walifundisha hilo pia.kuwa ni vyema mteja wa kwanza aondoke amenunua kitu.

Siku moja yule mama akanambia pale nlipokaa nivute draw nimpatie kitabu cha mahesabu.kumbe nlivuta nyingine ya juu kimakosa. Ile kuvuta hivi nikakuta kuna paka mkubwa sana yule mle ndani. Yule mama kuona nimevuta ile draw alinifuata kwa hasira akataka kunipiga kibao nlimtizama akasita.akatukana sana.

Akanambia nibebe kila changu mle ndani akanipa tsh 50,000 nisikanyage tena dukani kwake.na asije akasikia lolote lile maana atasema nimemwibia.nliondoka nikiwa na maswali mengi. Nakumbuka yule mama na mumewe kuna rangi walinikataza nisivae mle dukani. Wao walipendelea rangi ya kijani.wakiwa wanajifunga tukamba twa kijani pia.mikononi. lakini pia hata kwenye gari pale kwenye steering na gear walifunga vitambaa vya kijani. Mle ndani hawakuacha kuchoma ubani hasa asub,mchana na jion saa 10.

Kijani Ilikuwa ndiyo rangi yao pendwa pale dukani.nlitoka na maswali mengi sana.sikuwa na hamu tena ya kuuza duka kariakoo.

Miaka yangu yote nlikuwa napenda sana magari. Hivyo nliona ni wakati mzuri wa mimi kwenda jifunza ufundi makenika.

Nlitembea mpaka kijitonyama huko nikakuta kuna garage moja hivi maeneo ya karibu na sayansi kama.unataka kwenda kilipo kituo cha daladala kwa sasa.nliomba kujifunza ufundi.

Jamaa walishauriana sana kuhusu kunichukua. wakaamua niwe nafika asubuhi kujifunza mpaka jioni.

Nikawa sina pa kulala.nikawa natoka jioni naenda lala Mwenge.ikaenda hivi kama mwezi mzima.jamaa walinipenda sababu nlikuwa mpole na pia najituma sana.pia nlikuwa mwaminifu sana.so jioni natembea taratibu hadi mwenge najizungusha zungusha mpaka night ndo nalala.

Siku moja nikamwambia mlinzi issue yangu.akanielewa ila alishangaa sana kuwa kipindi chote hicho kumbe nlikuwa sina pa kulala. Wakaniruhusu niwe nalala mle ndani ya garage. Ikawa ndo maisha yangu.

Nlijifunza ufundi kwa bidii sana.nikaja fundishwa udereva na fundi mkuu. Nikawa angalau napata pesa kidogo natunza kwa mmiliki wa gereji ambaye alinipenda kama mdogo wake.

Ikawa kila mara napopata nafasi naenda Mwenge kuwasalimia jamaa wa pale.

Baadaye nikawa fundi mzuri wa body (panel beating )na mechanics kidogo.nliipenda kazi ndani ya miaka miwili nlikuwa napata kazi sehemu mbalimbali.

Pale garage nikawa sikai mara nyingi naitwa kwenda fanya kazi nje.mwenye gereji akaamua kuwa aniajiri.nikakubali.nlifanya kazi miezi 3 ananipa posho tu. Mshahara hanipi.kila nikimwambia maneno yanakuwa mengi.na kipindi hiki nimeshapanga nina maisha yangu.

Nikahamia garage nyingine.niliendelea kujijenga vizuri tu nikafahamika sana.baadaye yakaanza majungu kazini.mwenye gereji alikuwa anapenda sana majungu. Anapenda apewe hbr za watu wote pale gereji.mimi nlichukiwa sababu sikuwa napenda maneno na pia tabia ya wizi sikuwa nayo.hivyo ikawa matajiri wanapenda gari zao wanikabidhi mimi.

Sometimes wanaleta gari wanataka mimi ndo nikanunue spares wakati kazi inafanywa na mtu mwingine. Siwezi sahau siku ambayo walinizushia nimeiba spare ya gari Prado ambayo ilishushwa engine.

Nlifadhaishwa sana.nikaambiwa nisikanyage tena pale gereji.nikarudi mtaani.nikahangaika sana kupata kazi. Mara nyngi ilikuwa ni day worker tu. Nikaenda Pugu Road kuna tajiri mmoja ana magari makubwa pale.

Nlienda omba kazi kwa wahindi.walinambia hamna kazi.nikarudi mnyonge sana. Kule home miaka ilikuwa imeshapita na mama alisha fariki. Nikawa nawasiliana na mzee.

Nikamweleza suala la kazi. Akanambia atanisaidia kwenda kwa mzee wetu flani kule kijijini. Kweli baba alienda akanambia nimtumie kiasi flani cha pesa.nikatuma. zilitumwa dawa za kuoga na kutafuna. Niliambiwa nioge usiku ambao kesho yake naenda tafuta kazi. Then nilale chini, nisi sex ,nisinywe pombe.nlioga nikalala chini.

Kesho yake nikarudi Pugu Road( Nyerere Road) kule kule kwa wahindi. Nikasema nataka onana na manager.kweli nikapelekwa kwake.nikaonana naye nikamwambia nahitaji kazi.

Akanambia kama nipo tayari nianze muda huo anipeleke kwa supervisor.kweli akanipeleka kwa supervisor na kunambia nianze kazi ni deal na yale magari ambayo yalikuwa na shida kwenye body(panel beating)

Nikaanza kazi.

Itaendelea....
 
Chizi maarifa shusha nondo
 
Baaba. Watu wa Kigoma Ni bad news. Hata ukipakana nae shamba au kiwanja ujipange. Bora hata upakane na mchagga
Bora upakane na shetani tu, Mchagga kwa ulozi, wale jamaa hatari aisee. Ulozi wao wananunua popote pale hapa Tanzania ili mradi tu afanikiwe.
 
Mmmh, kwa hiyo sister angezubaa mtoto ndo ilikuwa kwa heri. Binadamu tunaabudu utajiri kuliko utu

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…