Visa vya chips funga kwenye sehemu za starehe (Bar)

Street Hustler

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
2,175
Reaction score
4,299
Mie Hawa watu huwa najiuliza akili zao huwa wanaziweka wapi, yaani huwa ni zero kabisa.

Mfano

1. Kuna mdada mmoja alikuwa kukaa meza ya jirani na jamaa yake sasa wakaagiza supu ya utumbo si unajua Arusha hii supu kila kona ipo basi yule dada aliinywa Ile supu kwa muda zaidi ya nusu saa, sasa nikajiuliza hapo anakula mafuta au anakunywa.

2. Leo wakati nacheki game ya Arsenal na Chelsea basi kaja jamaa mmoja big na mwanamke wake. Basi jamaa anagonga makali mwanamke chupa ya St. Anna na kiglass chake basi nyama ikaja yaani mwanamke anakula huku akichezea ki Itel cha tochi kuanzia dakika 36 ya mchezo wa Arsenal mpaka kipindi cha pili dakika ya 59 na baridi ya Arusha ile nyama sijui ilikuwaje.

Hawa ndugu imenitokea kuwatupia mijicho kila ninapokutana nao sehemu za moja mbili tatu.

Tupe na wewe huko huwa wanafanyaje hawa dada zetu.
 
We was friends = we were friends
 
we was friends!

kuna ulazima gani wa kutumia kiingereza hali ya kuwa hukifahamu vizuri.

Ila story yako imenivutia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi za ujana bana Kuna siku weekend Moja muda ya saa nne usiku hv nikiwa napiga vitu vyangu pale Calabash Basi nikapavibe ya kumpigia mdada mmoja hv alikuwa hostel pale UDSM Basi nikamwambia aje duh siakaja na wenzake wawili jumla watatu picha linaanza wanasema hawajala eti saa tano usiku! Nikawaambie agizen mzee kila mtu nipe supu ya kuku haya kinywaji savanna nikamwambia msela angu nlikuwa nae nikamwambia huu ujinga Sasa haya kwenda mziki wanataka billicanas na hapo sie hatuna ndinga tunawaambia Bora ambiance au kilitime pale shekilango eti billicanas ndo kunaamshaamsha.

Ile siku nakumbuka ndo ilkua siku ya mwisho kutumia pesa yangu hovyo kwa hiz chips funga mpaka leo huo ujinga sifanyagi
 
Jinsia ke ndo zao kujishongondoa wakiwa wanakula public..

Uwakute maghetoni kwao sasa... Anakula kama mwehu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…