Visa vya wanandoa/wapenzi kuuana vinaongezeka kila kukicha

Visa vya wanandoa/wapenzi kuuana vinaongezeka kila kukicha

PromiseLand

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2021
Posts
298
Reaction score
413
Niende moja kwa moja kwenye mada, nipo mkoa wa Geita kikazi na leo nimefanikiwa kufika sehemu inayoitwa Nyarugusu visa nilivyovikuta vinashangaza na hizi hapa ni simulizi nilizozikuta kwenye msiba uliovuta hisia za watu wengi.

Ilikuwa ni msiba wa mama mmoja aliyeuawa na mme wake kwa kuchomwa kisu baada ya kukutwa na mwanaume huyo akiwa na picha za uchi alizopiga na mwanaume mwingine. Lakini tukiwa kwenye msiba huo nilitaarifiwa kuwa kuna misiba mingine tena miwili ya wanandoa mmoja akiwa ni mwanamke aliyepigwa kwa nondo na mme wake na kupelekea kupoteza maisha, lakini mwingine alikuwa ni mwanaume aliyepigwa mshale akiwa anatoka kuoga usiku saa mbili kwa sababu ya kwenda na wake za watu.

Matukio haya yametukia ndani ya wiki moja katika Kijiji kimoja ukiachia mbali wanandoa waliotoana manundu, sasa ukijumlisha na hilo la mapanga Musoma hali katika ndoa nyingi ni tete.

Enyi wanandoa kuuana na kuwaacha watoto wakiwa yatima ndio suluhisho? Viongozi wa dini wanajukumu kubwa la kuangalia upya hizi ndoa wanazofungisha maana Hawa wanaouana wengi wamefunga ndoa za kidini.

Ni vizuri kuwapima wandoa kama Wana ukichaa kabla hawajaoana.

Nawasilisha.

1635921687571.jpeg

 
Back
Top Bottom