SoC02 Visa vya watu kujiua: Sababu kuu na ushauri wa nini kifanyike

SoC02 Visa vya watu kujiua: Sababu kuu na ushauri wa nini kifanyike

Stories of Change - 2022 Competition

Amani Ne

Member
Joined
Dec 15, 2018
Posts
11
Reaction score
10
Utangulizi
Kwa mujibu wa taarifa ya WHO (2019) ni kwamba kila baada ya sekunde 40 kuna mtu anajiua kwa sababu kadha wa kadha. Tatizo la watu kujiua limekua kwa kasi na linaongezeka kila kukicha na sababu zinazokusanywa za waliojiua hutofautiana kati ya mtu mmoja na mtu mwingine. Nina rafiki yangu anafanya kazi kama mchunguzi wa maiti amenieleza kuwa kwa week amekua akipokea miili zaidinya saba ya kesi za watu waliokwisha kujiua.

Kwa mujibu wa WHO (2019) ni kuwa kuna wastani wa 10.5 katika watu 100,000 ambao walijua kwa mwaka 2016 pekee. Na idadi ya watu kujiua huongezeka kila mwaka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Wanaume hujiua zaidi kuliko wanwake, katika watu 100 waliojiua nasi wanaume ni 75 na wanawake ni 25 (WHO, 2019). Na sababu za kujiua hufanana kwa jinsi zote mbili ila uwezo wa kujieleza upo kwa wanawake zaidi kuliko kwa wanaume, ndio maana idadi ya wanaume wanaojiua ni kunwa kuliko wanawake.

Tatizo hili si tu lipo Tanzania bali duniani kwa ujumla. Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaoongoza kujiua ni wale walio kati ya umri wa miaka 19 hadi 30. Kundi hili ni la vijana wa umri wa chini ambao kwa umri wao wako shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu na au kwa umri wao wamemaliza elimu ya sekondari na elimu ya vyuo na vyuo vikuu. Kundi hili kwa namna moja au nyingine ni kundi ambalo linakua na matamanio na matarajio makubwa ya kimaisha, kimahusiano na kiimani. Inapotokea kuyumba kwa moja ya matarajio tajwa wengi huathirika na ugonjwa wa afya ya akili na wanaposhindwa kujizuia hujikuta wamechukua maamuzi ya kujiua. Sababu nyingi ukizisikiliza hazileti mantiki lakini ndio watu hujua kwa sababu hizo Mfano kufokewa, kufumaniwa, kuhisi n.k hizi ni kipimo cha uwepo wa tatizo la akili nchini.

Afya ya akili ni muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kudhorota kwa afya ya akili hupelekea mtu kufanya maamuzi yasio na busara katika jamii ikiwemo kuzuru watu wa karibu, au kujizuru mtu mwenyewe. Matatizo yote ya ukatili iwe ukatili wa kijinsia, ukatili kwa watoto na au ukatili binafsi ikiwemo kujizuru na kujiua hutokana na madhara anayo yapata mtu katika mfumo wake wa akili. Kila binadamu kwa wakati tofauti anapitia mazingira yanayoweza kumletea athari katika afya ya akili. Mfano, kufukuzwa kazi, kupata hasara katika biashara, magonjwa, kufeli mitihani, matatizo ya kimahusiano (kuachana, kufamaniana), miito ya kiimani (kusikia sauti za watu walio kufa, kuwaona mizimu, misukule). Haya na mengine mengi hupelekea watu kupata shida katika afya zao za akili. Matatizo mengi ya afya ya akili yanapona kwa huduma za ushauri na nasaha.

Sababu kuu za watu kujiua
Kujiua kuna leta simanzi katika familia na jamii inayozunguka. Kupoteza nguvu kazi nyingi na rasilimali watu ambazo zingetumika katika uzalishaji wa shughuli za kiuchumi. Inasemekana kua 90% ya watu wanaojiua ni watu wenye uwezo mkubwa kiakili. Mara nyingi watu wenye uwezo mkubwa kiakili wanaposhindwa katika jambo fulani huamini kwamba hakuna mtu mwingine anaye weza kulitatua😅. Njia kubwa ya kupona kwa mtu ambae anachangamoto ya kutaka kujiua ni kueleza matatizo yake kwa watu sahihi waliomzunguka na kupatiwa msaada anaohitaji jambo hili linawezwa kufanywa na watu wenye uwezo wa kawaida na uwezo mdogo wa kiakili. Watu wenye uwezo mkubwa kiakili wanajiamini sana na kujikubali katika maamuzi yao, nashauri watu hawa wapewe elimu ya kuishi kwa kushirikiana itawasaidia kuwa huru kujieleza oale wanapokumbwa na matatizo.

Baada ya kusoma visa zaidi ya 50 vya watu waliojiua nimeweza kubaini kua zipo sababu kubwa tatu zinaoweza kutusaidia kujua kwanini watu wengi hujiua:

1. Uchumi
Watu wengi duniani hujiua kwa sababu hii. Wengi wa wafanya biashara na wafanya kazi wanaposhindwa kumudu hasara au kuyumba kwa uchumi hujikuta katika msongo wa mawazo na kupelekea kujiua. Mikopo ya kifedha inaposhindwa kuleta tija, usimamizi mbovu na ushauri usioridhisha wa kibiashara ni miongoni mwa sababu za kushuka kiuchumi.

Vijana wengi wana matarajio makubwa ya kimaisha, wengi wanapoajiriwa hujikuta wanaingia mikopo mikubwa, hufanya mambo kwa kushindana, kujiingiza katika biashara za mitandaoni bila kuwa na uelewa wa kutosha, matokeo yake wengi hushindwa kujizuia mambo hanapoenda ndivyo sivyo.

Suala la ajira, ukosefu wa ajira ni sababu pia inayopelekea kupoteza baadhi ya watu. Vijana wengi wanakata tamaa ya maisha pindi wanapomaliza vyuo na kukuta mtaaani mambo hayaendi kama walivyotarajia. Wengi bado wanaamini katika ajira rasmi, inapotokea tofauti na matarajio vijana wengi hukosa furaha, amani, mwishowe kuwa na msongo wa mawazo.

Vijana tupunguze matarajio makubwa, hakuna mafanikio yanayopatikana kwa usiku mmoja. Tujifunze kukusanya kidogo kidogo kwa muda mrefu tutafanikiwa. Maisha ya mitandaoni, kushindana mwisho wake huzaa tamaa na baadae mauti.

Migogoro ya kifamilia, kupigania mali na mirathi ni sababu inayoweza leta mauaji na watu kujiua. Kunyimwa fungu katika mirathi au kuzulumiana ni moja ya sababu za kujiua.

2: Mahusiano
Mahusiano ya kimapenzi na ndoa ni moja ya sababu inayopelekea watu wengi kujiua.
Nadhani unaweza kunielewa zaidi kama umewahi kumfumania mpenzi wako au mke wako wa ndoa au mme wako na mtu mwingine, wote tunajua namna ambavyo mioyo yetu huwa inalipuka. Tumeona wengi wakiua na kujiua inapotokea kesi ya kufumaniana. Kuachana na kutelekezwa katika mahusiano ni sababu nyingine inayopelekea ongezeko la watu kujiua. Tumeona watu wakinywa sumu na au kujivika vitanzi kisa kutokubaliwa au kuachwa. Kila baada ya kesi nne za kujinyonga moja inahusu mapenzi na mbili zinahusu uchumi na mwisho inahusu sababu zingine

3: imani
Hapa ninazungumzia imani za kidini na imani za kishirikina. Uwezo wa mtu kusikia na kuwasiliana na viumbe visivyo onekana kwa macho. Tumeshuhudia visa vingi vya watu kuua na kujiua ili wafike mahali ambako wao wanaamini ni pa starehe (tukumbuke habari za mfalme Juha😀). Kuna watu pia wanajiua wanapofiwa na wapendwa wao, wengi husimulia kabla ya kujiua kuwa wamesikia wakiitwa etc.

Waganga wa jadi nao huchangia sana katika kufanya hili tatizo kuwa kubwa zaidi. Waganga wa jadi ni watu wanaoaminika na wateja wao, inapotokea mtu anapopata tatizo na mganga anapotaja watu wengine kuwa chanzo cha matatizo hupelekea mgogoro baina ya pande mbili ambapo moja ya athari ni mauaji ya watu wasio na hatia.

Ukatili wa kijinsia unaosababishwa na imani potofu husababisha watu wasio na hatia kujiua. Baba kumbaka bintiye ili apate utajiri, kulawiti watoto wakiume kwa masharti ya kupata mali huacha makovu kwa wanajamii ambao wanaposhindwa kukubaliana na matokeo wengi hujiua. Imani potofu ni mwiba katika makuzi ya jamii.

Nini kifanyike
Ninashauri, sisi taasisi zinazosaidia kuboresha afya ya akili tuwe sauti na sikio kwa watu wanaopitia matatizo yanayosababisha mtu aweze kujiua

Elimu itolewe kwa wanajamii, watu wafundishwe kuchangamana na watu katika burudani na kuwa huru kueleza matatizo yao wanapokua na matatizo.

Uwepo urahisi wa watu ambao wanamsongo wa mawazo kutokana na hasara za kibiashara kusamehewa mikopo yao na au uwekwe utaratibu wa ofisi za ustawi kuwatambua watu ambao mali zao zinapigwa mnada kutokana na mikopo kuweza kusaidiwa kwa kupatiwa ushauri na maeneo ya wao kuishi na kujipanga upya.

Uwepo uwezekano wa kila ofisi ya Ustawi kuwa na budget kusaidia watu ambao wameporomoka kiuchumi, watu wasio jiweza, etc

Mikopo kutoka board ya mikopo itolewe kwa wanafunzi wote wanao maliza vyuo vikuu na vyuo vya kati na ijumuishwe katika madeni yao ya mikopo. Ikatumike kama mitaji, na ofisi za NEEC (Uwezeshaji wananchi kiucbumi) za kila halmashauri ziwe na programu za kuwafanyia mentorshirship vijana wote waliopatiwa mikopo ili mikopo wanayopatiwa itumike kama ilivyokusudiwa.

Kama ilivyoundwa tume ya kupambana na madawa ya kulevya, pia nashauri tuwe na tume ya kupambana na vitendo vya kujiua. Tume hii iwe na ofisi kila kijiji na kila mtaa na kila kata, wajumbe wake wawe wana jamii ambao wanafikika na kila raia, viongozi wake wasiwe viongozi wa serikali.

Tupinge kwa nguvu zetu zote mila na imani potofu katika jamii. Waganga wajadi wasio na wito na wasio na nidhamu wazuiwe kutoa huduma za matibabu. Wengi walio matapeli hutumia mbinu ovu kuleta taharuki katika jamii kwa kuwatendesha wana jamii matendo ya kiovu. Ikumbukwe waganga wa jadi wana aminika sana hivyo wanaposema jambo basi wateja wao wanaliamini.

Makanisa na misikiti waanzishe mpango wa kusaidia waumini wao kukua kiuchumi. Ikiwezekana kupitoa sadaka na dhaka asilimia fulani itengwe kwa ajili ya kuwasaidia waumini wasio na mitaji kukua kiuchumi, iwasaidie lia wale waliokosa au kupata hasara kurudi upya. Makanisa mengi na misikiti mingi haina utaratibu wa kusaidia watu wao kiuchumi. Ukifuatilia watu wengi wanaojiua wengi wao ni wakristo wazuri na waislamu wazuri. Huduma za kusaidiana katika makanisa zinajikita katika kufiwa na magonjwa tu na sio kuinuana kiuchumi. Wachunangaji na Mashekhe tuchukue somo hapa.

Rejea
1. BBC - Homepage › swahili
Ni kwanini idadi ya vijana wanaojiua Tanzania imeongezeka kwa kasi?

2. Kila sekunde 40 mtu mmoja anakufa kwa kujiua-WHO
 
Upvote 2
Back
Top Bottom