Visima 10 vya Maji Kuchimbwa Wilaya ya Kaliua

Visima 10 vya Maji Kuchimbwa Wilaya ya Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

VISIMA 10 VYA MAJI KUCHIMBWA WILAYA YA KALIUA, KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI

Taarifa kutoka Ofisi ya Meneja RUWASA Wilaya ya Kaliua imethibitisha kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora Imepokea Mitambo ya kuchimba Visima Kumi (10) ambavyo vitasaidia kumshusha Mama Ndoo kichwani

Visima kumi vya Maji kuchimbwa Wilaya ya Kaliua, ambapo Jimbo la Ulyankulu kutachimbwa visima vitano na Jimbo la Kaliua vitachimbwa visima vitano katika katika Kata za Mwongozo, Makingi, Ilege, Silambo, Uyowa, Usinge, Kamsekwa, Ufukutwa, Zugimlole na Igwisi.

Mtambo huu wa kuchimba visima ni wa Mkoani Tabora ambapo ukimaliza kuchimba visima hivi kumi utahamia katika Wilaya nyingine ya Mkoa wa Tabora ambapo ikifikia tena awamu ya Kaliua watakuja kuchimba visima vingine tena hivyo mtambo ni wetu unafanya mzunguko lengo ni kuendelea kupunguza changamoto za maji ndani ya Mkoa wa Tabora.

Tukumbuke pia Kaliua inatarajia mradi mkubwa wa Maji toka Ziwa Victoria.
Kama unaona Kijiji chako hakijatajwa basi subiria mzunguko wa pili mtambo ni wetu.

Lengo ni kumtua Mama ndoo ya Maji 💦
#TwendeZetuKaliua
#KaliuaImefunguka
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 13.41.03(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 13.41.03(1).jpeg
    65 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 13.41.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 13.41.03.jpeg
    56.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 13.41.02(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 13.41.02(2).jpeg
    67.2 KB · Views: 2
Back
Top Bottom