#COVID19 Visions & Trends Readings: Unaweza Usiamini Hili, "Namuona Baba Askofu Mpinga Chanjo, Ukichanjwa Chanjo ya Corona!"

#COVID19 Visions & Trends Readings: Unaweza Usiamini Hili, "Namuona Baba Askofu Mpinga Chanjo, Ukichanjwa Chanjo ya Corona!"

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Hili ni bandiko la Visions na Trends Readings, Visions za Trends Reading sio utabiri, ni maono ya mielekeo. Ni tofauti na maono ya utabiri.

Kwenye visions za trends readings zangu, zinanionyesha "Mbunge Wangu wa Kawe, Baba Askofu, Mheshimiwa sana, Dr. Josephat Gwajima" akichanjwa chanjo ya Corona!.

Baba Askofu Gwajima, licha ya kupinga chanjo ya Corona kwa mahubiri ya zaidi saa nzima., Trends Readings zangu, zinanionyesha, Baba Askofu Dr. Josephat Gwajima akichanjwa chanjo ya Corona!, na siku hiyo, atakapo chanjwa, atazungumza na ukimsikiliza atakakacho sema, unaweza usiamini kama mtu huyo anayezungumza siku hiyo, na aliyechanjwa, ndio, mtu yule yule aliyeongea maneno haya mimbarini kwake siku za nyuma!.

Trends na Visions ni Nini?
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa trends na visions. Trends ni kusoma mielekeo, na visions ni kuona mambo yajayo ya mbali, yatakayo tokeo kutokana na trends unanaziona sasa. Hivyo trends za Baba Akofu Gwajima anazokwenda nazo sasa za kupinga chanjo ya Corona, sii lolote, sii chochote, kwa sisi waona mbali, tuliojaaliwa kupata visions za yajayo, tunaona kabisa mambo mazuri huko tuendako, ikiwemo, licha ya Baba Askofu kupinga sana chanjo, trends na visions zinanionyesha Baba Askofu akipokea Chanjo ya Corona kwa kuchanjwa!.

Kutafsiri Trends & Visions, ni Psychoanalysis. Jee Hii Psychoanalysis ni Nini, na ya Kazi Gani?
Kuna msemo usemao, information is power, yaani ukiwa na taarifa sahihi, unakuwa na nguvu, hivyo hii psychoanalysis ni somo la kujifunza kwa nini watu wana behave kwa namna fulani kwenye situations fulani. Hivyo ukijua tabia za watu, kwa nini they behave the way they behave, wewe unakuwa na power ya kuwafahamu na sometimes bila wenyewe kujifahamu, hivyo kwa kuandika humu kuhusu their human behaviors, hii inaweza kuwasaidia watu hawa kujielewa na kubadilika, and changing for the better kwa kupunguza maneno na kuongeza vitendo. Waalimu wakuu wa hili somo la psychoanalysis, ni wawili, Carl Jung na Sigmund Freud.
Nimeifundisha sana Psychoanalysis, humu
Pascal Mayalla said:
Carl Jung na Sigmund Freud ni Nani na Walifundisha Nini kwenye Psychoanalysis?
Hawa ni mabingwa wa somo la saikojia ya watu na walijikita katika kufanya analysis za kubaini chanzo, the motive behind, tabia, maneno na matendo ya baadhi ya watu, huku Freud akijikita zaidi katika mahusiano ya kifamilia na Jung akijikita katika mahusiano ya kijamii, hivyo Freud kuheshimika kama mwanzilishi wa psychoanalysis na Jung akawa ni muasisi wa analytical psychology au Jung psychology, tena ingekuwa ni amri yangu, ningeamrisha viongozi wetu wote wapatiwe semina ya Jung Pschology inafundishwa katika kituo cha TAGLA pale IFM, kwa njia ya distance learning, kutawasaidia sana, maana kuna wengine wanadhani kuongea sana, kuhutubia sana, au kuongea kwa ukali na vitisho, ndiko kutalisaidia taifa hili kupata maendeleo!. No way, maendeleo ya kweli hayaletwa na maneno, na ukali au vitisho, bali yataletwa na matendo na mipango mkakati!, Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.
Hivyo ili kuwathibitishia Baba Askofu atapokea Chanjo ya Corona, Tembelea uzi huu, umsikilize kwa makini Baba Askofu, alisema nini hapa,
Baadaye aligeuka.

Hata siku alipozungumza haya kumhusu Muadhama Polycarp, Carninali Pengo, , baadaye alifuta kauli na alimtembelea na kuomba msamaha.

Alipomzungumzia Bashite, , pia baadaye alifuta kauli na wakapatana.

Hivyo hata kauli yake hii ya sasa ya kupinga chanjo ya Corona, ni kauli tuu, isiwatatize, Baba Askofu, atafuta kauli na atachanjwa Corona.

Kwa wale wageni na mabandiko ya Trends zangu, mnaweza kusisoma baadhi ya trends na zilikuja kutokea hivyo hivyo...

Trends na Visions, Zina Uzuri na Ubaya, Uzuri wa Trends ni zinapotokea kweli kama ulivyosema, ubaya wa trends, ni zisipotokea, utaonekana muongo, hivyo hata mimi, sio trends zangu zote hutokea, kuna nyingine hazitokei, hivyo kuonekana muongo,
Hizi ni baadhi ya trends ambazo hazikutokea,

Paskali
 
Si mchanjwe hiyo graphene oxide nano particles mtulie, msubiri wazungu wawaletee 5G waanze kuwaondoa mmoja mmoja? Mnataka kila mtu aingie kwenye hilo janga ? Sio kila mtu ni mjinga. Wewe kachanje..hata achanje gwajima wengine hatutachanja na watu wetu.

Mshasema ni choice, promo hizi zote za nini? Sio kila mtu akili zake zimeshikiliwa na mawazo au maoni ya watu. Hata gwaji achomwe hatutachoma...it's that simple. Eti kama mzungu angetaka kutuuwa angetuuwa tu..Mzungu sio Mungu, sio kwamba anaweza fanya lolote lile kama akili za baadhi ya watu wanavyotaka tuaminj ili tuchanje.

Kwann tuchanje kama watu wajinga vile? Yani kila mtu achanje tu. Ni hivi watz wamekataa watachanjwa hao mnaowajua nyinyi.
Tansa.jpg
 
Ngoja akuangushie kitu kizito ukasimulie kizazi chako chote,naona unazidi kumchokonoa.

Kwani wewe unaweza kuthibitisha hayo kuwa chanjo Haina madhara ya muda mfupi au mrefu?.

Au hujui maandamano yanayofanyika Ulaya kupinga chanjo? Kwa Nini wanapinga.

Ungekuwa wa maana ungetumia ujuzi wako wa kuandika habari kujibu kisayansi hoja za Gwajima
na Magufuli na nabii Loringa juu ya mashaka waliyonayo juu ya chanjo.

Yeye alishasema hana shida ya chanjo,ila hii ya Mwendokasi.

Hebu wewe tueleze faida ya chanjo hizi Kama bado aliyechomwa anaweza kuambukizwa na kuambukiza au kufa kabisa.

Rais akitaka kukuteua atakuteua tu si lazima ung'ang'ane kumzodoa Gwajima ili ukumbukwe.

Msalimie Bashite.
 
Si mchanjwe hiyo graphene oxide nano particles mtulie, msubiri wazungu wawaletee 5G waanze kuwaondoa mmoja mmoja? Mnataka kila mtu aingie kwenye hilo janga ? Sio kila mtu ni mjinga. Wewe kachanje..hata achanje gwajima wengine hatutachanja na watu wetu...
Kule FB, Twitani, Insta na Youtube watu wanasema wameamini kweli JPM hajafa! Na kwamba ile kauli yake ya ^Nileteeni Gwajima! Nileteeeni Gwajima!! Nileteeni Gwajimaaaaaa!!!^ ilikuwa so prophetic & timely. Huyu Askofu Mbunge amemhisibu JPM & legacy yake hadi raha sana!!! 🙂 🙂 🙂
 
Si mchanjwe hiyo graphene oxide nano particles mtulie, msubiri wazungu wawaletee 5G waanze kuwaondoa mmoja mmoja? Mnataka kila mtu aingie kwenye hilo janga ? Sio kila mtu ni mjinga. Wewe kachanje..hata achanje gwajima wengine hatutachanja na watu wetu..
Typical stupidity in live action and brain malfunctions in display!!
 
Anaweza fanya hivyo ili kumfurahisha mwenyekiti wake kama bado ana ndoto za ubunge, na kwa tabia zake za kisanii alizonazo sitamshangaa akigeuka.
 
Si mchanjwe hiyo graphene oxide nano particles mtulie, msubiri wazungu wawaletee 5G waanze kuwaondoa mmoja mmoja? Mnataka kila mtu aingie kwenye hilo janga ? Sio kila mtu ni mjinga. Wewe kachanje..hata achanje gwajima wengine hatutachanja na watu wetu...
Kweli kabisa prom.za Nini? Au walipopewa pesa waliwekewa target ya idadi Fulani ya watu,wanaona haitatimia?
 
Ngoja akuangushie kitu kizito ukasimulie kizazi chako chote,naona unazidi kumchokonoa.

Kwani wewe unaweza kuthibitisha hayo kuwa chanjo Haina madhara ya muda mfupi au mrefu?...
This comment deserves countless likes!!! 🙂 ^Chanjo ya Mwendokasi^
 
Uthibitisho wa Bi Mkubwa kwamba chanjo ni salama, na haina madhara:

1. Mimi ni Mama
2. Mimi ni Mke
3. Nina Watoto
4. Nina Wajukuu
5. Mimi ni Rais
6. Mimi ni Mkuu wa Nchi & Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Yote
7. Nishawahi kupewa chanjo ya magonjwa mengine zamani
8. Kama ugonjwa wa korona umemkumba ndugu au jamaa yako wa karibu, lazima utakuwa na mtazamo tofauti kuhusu chanjo
9. Niko tayari kuchanjwa
10. Siwadanganyi Watanzania

^Brigedia, hapa tumepigwa!!!^ ~ JPM 🙂
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la Visions na Trends Readings, Visions za Trends Reading sio utabiri, ni maono ya mielekeo. Ni tofauti na maono ya utabiri.

Kwenye visions za trends readings zangu, zinanionyesha "Mbunge Wangu wa Kawe, Baba Askofu, Mheshimiwa sana, Dr. Josephat Gwajima" akichanjwa chanjo ya Corona!.
Bandiko Suri sana Mkuu Pascal..

Huyu MUNGU angetufanyia wepesi tu kwa huyu Mchungaji feki maana anayofanya is like 'sabotage'.. na uzuri wa covid19 wale wote wanaoidharau ndio inawafyeka mfano Nkuruzinza na Meko..

Wee ngoja tutarudi kati sasa hivi kwa huyu Mchungaji wa uongo.

Wanabodi

Hili ni bandiko la Visions na Trends Readings, Visions za Trends Reading sio utabiri, ni maono ya mielekeo. Ni tofauti na maono ya utabiri.
 
Si mchanjwe hiyo graphene oxide nano particles mtulie, msubiri wazungu wawaletee 5G waanze kuwaondoa mmoja mmoja? Mnataka kila mtu aingie kwenye hilo janga ? Sio kila mtu ni mjinga. Wewe kachanje..hata achanje gwajima wengine hatutachanja na watu wetu.

Mshasema ni choice, promo hizi zote za nini? Sio kila mtu akili zake zimeshikiliwa na mawazo au maoni ya watu. Hata gwaji achomwe hatutachoma...it's that simple. Eti kama mzungu angetaka kutuuwa angetuuwa tu..Mzungu sio Mungu, sio kwamba anaweza fanya lolote lile kama akili za baadhi ya watu wanavyotaka tuaminj ili tuchanje.

Kwann tuchanje kama watu wajinga vile? Yani kila mtu achanje tu. Ni hivi watz wamekataa watachanjwa hao mnaowajua nyinyi. View attachment 1873722
Graphene Oxide? Hivi huwa mnapotosha kwa faida ya nani?? Kma ni kuwaua hapo ulipo 90% ya vitu kuanzia huo mtumba uliovaa mpka simu unayotumia imetoka kwa beberu eti asikumalize kutumia hivyo mpaka akupe chanjo???

Tuache inferiority complex.... Kwani kuna nchi imekataza usitengeneze chanjo zako?? Eti Graphene Oxide!!
 
Back
Top Bottom