Wanabodi
Hili ni bandiko la Visions na Trends Readings, Visions za Trends Reading sio utabiri, ni maono ya mielekeo. Ni tofauti na maono ya utabiri.
Kwenye visions za trends readings zangu, zinanionyesha "Mbunge Wangu wa Kawe, Baba Askofu, Mheshimiwa sana, Dr. Josephat Gwajima" akichanjwa chanjo ya Corona!.
Baba Askofu Gwajima, licha ya kupinga chanjo ya Corona kwa mahubiri ya zaidi saa nzima., Trends Readings zangu, zinanionyesha, Baba Askofu Dr. Josephat Gwajima akichanjwa chanjo ya Corona!, na siku hiyo, atakapo chanjwa, atazungumza na ukimsikiliza atakakacho sema, unaweza usiamini kama mtu huyo anayezungumza siku hiyo, na aliyechanjwa, ndio, mtu yule yule aliyeongea maneno haya mimbarini kwake siku za nyuma!.
Trends na Visions ni Nini?
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa trends na visions. Trends ni kusoma mielekeo, na visions ni kuona mambo yajayo ya mbali, yatakayo tokeo kutokana na trends unanaziona sasa. Hivyo trends za Baba Akofu Gwajima anazokwenda nazo sasa za kupinga chanjo ya Corona, sii lolote, sii chochote, kwa sisi waona mbali, tuliojaaliwa kupata visions za yajayo, tunaona kabisa mambo mazuri huko tuendako, ikiwemo, licha ya Baba Askofu kupinga sana chanjo, trends na visions zinanionyesha Baba Askofu akipokea Chanjo ya Corona kwa kuchanjwa!.
Kutafsiri Trends & Visions, ni Psychoanalysis. Jee Hii Psychoanalysis ni Nini, na ya Kazi Gani?
Kuna msemo usemao, information is power, yaani ukiwa na taarifa sahihi, unakuwa na nguvu, hivyo hii psychoanalysis ni somo la kujifunza kwa nini watu wana behave kwa namna fulani kwenye situations fulani. Hivyo ukijua tabia za watu, kwa nini they behave the way they behave, wewe unakuwa na power ya kuwafahamu na sometimes bila wenyewe kujifahamu, hivyo kwa kuandika humu kuhusu their human behaviors, hii inaweza kuwasaidia watu hawa kujielewa na kubadilika, and changing for the better kwa kupunguza maneno na kuongeza vitendo. Waalimu wakuu wa hili somo la psychoanalysis, ni wawili, Carl Jung na Sigmund Freud.
Nimeifundisha sana
Psychoanalysis, humu
Pascal Mayalla said:
Hivyo ili kuwathibitishia Baba Askofu atapokea Chanjo ya Corona, Tembelea uzi huu, umsikilize kwa makini Baba Askofu, alisema nini hapa,
Wanabodi, Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje? Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza...
Baadaye aligeuka.
Hata siku alipozungumza haya kumhusu Muadhama Polycarp, Carninali Pengo,
, baadaye alifuta kauli na alimtembelea na kuomba msamaha.
Alipomzungumzia Bashite,
, pia baadaye alifuta kauli na wakapatana.
Hivyo hata kauli yake hii ya sasa ya kupinga chanjo ya Corona, ni kauli tuu, isiwatatize, Baba Askofu, atafuta kauli na atachanjwa Corona.
Kwa wale wageni na mabandiko ya Trends zangu, mnaweza kusisoma baadhi ya trends na zilikuja kutokea hivyo hivyo...
Wanabodi, Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha...
Wanabodi, Hili ni bandiko kuhusu kitu kinachoitwa trends na visions. Trends ni kusoma mielekeo, na visions ni kuona mambo yajayo ya mbali, hivyo trends za rais Magufuli anazokwenda nazo, kwa sisi waona mbali, tuliojaaliwa kupata visions za yajayo, tunaona kabisa mambo mazuri huko tuendako...
Wanabodi. Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja? Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu hilo...
Trends na Visions, Zina Uzuri na Ubaya, Uzuri wa Trends ni zinapotokea kweli kama ulivyosema, ubaya wa trends, ni zisipotokea, utaonekana muongo, hivyo hata mimi, sio trends zangu zote hutokea, kuna nyingine hazitokei, hivyo kuonekana muongo,
Hizi ni baadhi ya trends ambazo hazikutokea,
Wanabodi, Hili ni bandiko kuhusu kitu kinachoitwa "voices from within" ni kama "trends reading of some sort. 'Voices from Within" ni kuisikia sauti kutoka ndani yako!. Sasa baada ya Naibu Waziri wa Madini kushindwa kuapa, na Rais Magufuli kumtumbua pale pale, au papo kwa papo kwa kudhania...
Wanabodi, Hili ni bandiko kuhusu kitu kinachoitwa "voices from within" ni kama "trends reading of some sort. 'Voices from Within" ni kuisikia sauti kutoka ndani yako!. Sasa baada ya Naibu Waziri wa Madini kushindwa kuapa, na Rais Magufuli kumtumbua pale pale, au papo kwa papo kwa kudhania...
Wanabodi, Declaration of Interest Naomba nianze kwanza kwa kudeclare interest, kuwa mimi Pascal Mayalla ni mkaazi wa Wilaya wa Kinondoni, kama mwananchi wa kawaida, ila pia ni mwanachama, wa chama cha siasa, na sio Chadema, mimi ni mfuasi wa falsafa ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage...
Paskali