Visit Tanzania- Wanasimba hatutaki tena huo ujinga

Visit Tanzania- Wanasimba hatutaki tena huo ujinga

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Viongozi wa Simba kama mnakua na mambo yenu binafsi ya kujipendekeza, basi ingieni kwenye Siasa. Msilete Uchawa wa kijingajinga kwenye timu yetu.

Msimu uliopita mlijifanya Wazalendo sana mkaacha kumtafuta wadhamini kimataifa Bali mkataka kuonekana wazalendo uchwara.

Mkaandika Visit Tanzania
Yanga wenyewe Wakaamua kusaka pesa kutoka mdhamini Hier.

Sote tumeona Rais Samia anachofanya kwa timu yake Yanga.

Simba tumepambana na Wydad bingwa mtetezi mpaka Mwarabu analia lakini hatukuthaminika.

Leo hii waarabu ile Visit Tanzania wanayo kichwani mpaka kesho.

Yanga wao wameitangaza Hier lakini Rais ndio kafurahia kutangaza Hier kuliko Tanzania.

Sasa tunasema imetosha. Kama mkokosa wadhamini basi acheni plain.

Hakuna Cha uzalendo wana uzwazwa hapa ni kusaka Hela tu.

Ni wazi Wanasimba hatufurahishwi na mambo ya Siasa kuletwa kwenye michezo.
 
Labda umepata hasira na joto tu hiyo imeshavaliwa misimu yote ya mashindano ya kimataifa!
 
Usichokijua Sisi Ndiyo Wenye Nchi hii Tanzania. Ndiyo Maana Tunaitangaza Nchini Yetu.

Fedha tunaitaka lakini tunatanguliza Mbele Kuithaminisha nchi yetu ili Kwaro Dunia na Afrika Waelewe Kuna Nchi Inaitwa Tanzania na Waanze Kufuatilia Raha Zilizoko Tanzania na hatimaye Kujiongezea Utalii na Uwekezaji wa Kamataifa nchini kwenye Eneo la Viwanda vya Boashara, Viwanda vya Kukuza Mpira, Viwanda vya Utalii, Viwanda vya Upendo na Viwanda vya Kusambaza Upendo kwa Majirani.

NB: Sisi kama Wenye Nchi hatuna Hasara ya Kuitangaza nchi yetu na Sina Wasiwasi na Kila Mtanzania anaishi kwa Simba (Wenye Nchi). Simba Nguvu Moja Alunta Continua
 
Viongozi wa Simba kama mnakua na mambo yenu binafsi ya kujipendekeza, basi ingieni kwenye Siasa. Msilete Uchawa wa kijingajinga kwenye timu yetu.

Msimu uliopita mlijifanya wazalendo sana mkaacha kumtafuta wadhamini kimataifa Bali mkataka kuonekana wazalendo uvhwara. Mkaandika Visit Tanzania
Yanga wenyewe Wakaamua kusaka pesa kutoka mdhamini Hier.
Sote tumeona Rais Samia anachofanya kwa timu yake Yanga.
Simba tumepambana na Wydad bingwa mtetezi mpaka Mwarabu analia lakini hatukuthaminika. Leo hii waarabu ile Visit Tanzania wanayo kichwani mpaka kesho.
Yanga wao wameitangaza Hier lakini Rais ndio kafurahia kutangaza Hier kuliko Tanzania.

Sasa tunasema imetosha. Kama mkokosa wadhamini basi acheni plain.
Hakuna Cha uzalendo wana uzwazwa hapa ni kusaka Hela tu.
Ni wazi Wanasimba hatufurahishwi na mambo ya Siasa kuletwa kwenye michezo.
Siamini kama viongozi wangu wa Simba wenye uweledi Mkubwa watafuata ushauri wako huo wa kijinga eti kuacha plain kuliko kuweka "Visit Tanzania". Kwanza ujue tunatangazia jezi zetu kileleni mwa Mlima Kilimanjaro ambapo ni tayari tushaanza kuitangaza Tanzania!
 
Back
Top Bottom