Kaka mimi kwa mtizamo wangu nadhani pia ni nchi zote kama sio dunia nzima, ustaarabu unaendana na kipato huwezi kuishi uswahilini ukataka ustaarabu ukaeleweka
Kama una kipato cha ustaarabu usirudie tena kwenda huko karume kwenye makekele, nenda maduka makubwa makubwa
Huko Karume waichie hao ambao sio wastaarabu
Tunaweza kuweka mifumo ya kujiendesha kistaarabu sehemu nyingi.
Tunaweza ku plan mambo yawe ya kistaarabu hata sehemu za watu wa hali ya chini.
Kwa kweli, huko ndiko tulikotokea.
Dar es salaam ulikuwa ni mji wa kistaarabu. Kuna vijana tukiwahadithia kuwa mji ulikuwa na umeme, maji, mabasi ya usafiri wa umma mpaka ya Icarus Kumbakumba, huduma za kuzoa takataka angalau mara moja za Halmashauri ya Jiji, mpaka miaka ya mwanzo ya 1980s, watu wanaona kama hadithi za kubuni.
Ni vigumu sana kuwa na ustaarabu kama kuna mfumuko mkubwa wa idadi ya watu, watu hawana kazi, wenye kazi kazi nyingi ni za "disguised unemployment" kama hizo za umachinga.
Ni vigumu sana kuwa nanustaarabu katika jamii yenye watu wenye njaa, njaa inaondoa ustaarabu. Hapo Karume hata kama mtu kalelewa kwa misingi ya heshima na kutoshikashika watu huko kijijini kwao, akija mjini na kuona ushindaninwa kibiashara ndiyo unamtaka afanye hivyo ili kufanikiwa, atafanya hivyo tu.
Njaa haina ustaarabu.
Ukitaka ustaarabu, tengeneza uchumi vizuri uondoe njaa kwanza.
Sisi tulijitahidi kuendeleza ustaarabu hata kwenye njaa ya miaka ya 1980- 1985, tukapanga foleni kwenye maduka ya kaya kununua chakula, tukisaidiwa sana na idadi ya watu kuwa ndogo. Ni vigumu sana kukosa ustaarabu kama ukiangalia kushoto unamuona mtu mnayesoma naye, ukiangalia kulia unamuona mtu mnayesali naye.
Sasa hivi, kuna njaa halafu kuna massive rural urban migration, vijana wanatoka vijijini mwao, wanakuja mijini hawamjui yeyote, wana njaa katika mji mkubwa ambao hawamjui mtu, hapo ustaarabu ni kitu cha mwisho kabisa katika mawazo yao.