#COVID19 Vita dhidi ya Corona: Kunawa mikono sawa lakini vipi kutumia media kuhimiza watu kuacha kupiga chafya na kukohoa kwa kutumia viganja vya mkono?

#COVID19 Vita dhidi ya Corona: Kunawa mikono sawa lakini vipi kutumia media kuhimiza watu kuacha kupiga chafya na kukohoa kwa kutumia viganja vya mkono?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Unajua wakati mwingine wanadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa tena sometimes kwa kukosa maarifa madogo tu.

Mfano halisi wa hiki ninachosema ni sisi wanadamu kutumia nguvu kubwa kuhimiza watu kunawa mikono/kutakasa mikono katika kudhibiti maambukizi ya corona na kutumia nguvu kidogo kuhimiza watu kuacha kupiga chafya au kukohoa kwa kutumia kiganja/viganja vya mkono.

Yaani tunatumia nguvu kubwa na muda mwingi kupambana na matokeo(vimelea kwenye mikono) badala ya kuelekeza nguvu hiyo kupambana na chanzo cha hayo matokeo(kukohoa au kupiga chafya huku umeziba mdomo kwa kiganja/viganja) na huku ndio kuangamia kwa kukosa maarifa ninakokusema.

Ukweli ni kwamba, hata ukinawa, bado utalazimika kufunga bomba kwa kutumia mikono hiyo hiyo ulionawa wakati bomba hilo teyari lko contaminated baada ya wewe kulifungua ili unawe(umesambaza virusi kwenye bomba wakati unalifungu).

Mfano mwingine ni jinsi wahudumu kwenye mabaa na sehemu za kulia chakula wanavyoshiriki kusambaza huu ugonjwa pale wanapokufungulia kinywaji kwa kutumia mikono ambayo baadhi yao wana vikohozi na wanatumia mikono hiyo kuziba midomo yao pale wanapokohoa au kupiga chafya na kisha baadae wanakuja kukufungulia kinywaji(via, soda, n.k).

Kwahiyo, ukichunguza, utagundua ndio maana huu ugonjwa unakuwa mgumu kudhibiti kwani tumepuuza chanzo kikuu kinachosambaza huu ugonjwa huku wengi hutavai barakoa.

Kwa kutumia vyombo vya habari na kampeni zingine, ni rahisi kuhimiza watu kuacha kukohoa na kupiga chafya kwa kutumia viganja vya mikono na tukapata matokeo mazuri kuliko ilivyo vigumu kuhimiza watu kuvaa barakoa na wakavaa kwani mpaka sasa uvaaji wa barakoa bado uko chini sana.

Hivyo, nashauri sehemu ya fedha zinazotolewa kupambana na corona, zitumike kugharamia matangazo ya kuhamasisha wananchi waache tabia ya kupiga chafya au kukohoa huku wameziba midomo yao kwa kutumia viganja vya mkono na badala yake wahimizwe kutumia viwiko vya mikono kuziba midomo yao wanapokohoa, kupiga chafya na hata wanapopiga mihayo.

Wizara ya Afya tumieni wasanii na watu wengine maarufu kuhimiza na kushawishi watu kuacha kukohoa, kupiga chafya na hata kupiga mihayo kwa kutumia viganja vya mikono vinginevyo huu ugonjwa kamwe hatutoushinda.

Mfano ni Raisi kila anaposimama kuhutubia, ahimize watu kuacha kukohoa na kupiga chafya kwa kutumia viganya vya mikono na clip zake ziwe zinarudiwa katika vyombo vya habari(Radio, television, n.k).

Pia,wasanii wakubwa kama kina Diamond, Ally Kiba na wengineo, watumike kuelimisha umma juu ya jambo hili na ninahakika tutapata matokeo chanya baada ya muda mfupi tu.

Matangazo au ujumbe wa aina hiyo pia utumike wakati wa matangazo ya mechi za ligi kuu na matukio mengine yanayovuta hisia za watu wengi.

Bila kulinda mkono yetu, hakuna kujilinda na corona.
 
Kwani kukohoa ni tabia au ugonjwa! Unataka watu waache tabia ya kukohoa? Hivi una akili wewe?
Wenzako sasa hivi wana promote chanjo, wewe unataka watu wafundishwe namna ya kukohoa.
Usifikiri watu hawapo Conscious kuhusu Covid19, watanzania wengi wasio vaa barakoa wameng'amua tayari kuwa huu " ugonjwa" ni scum! Hakuna lolote...ninyi mnaolishwa taarifa na Television kuhusu Corona ndo mtabakia kuogopa na kujiziba msipumue vizuri matokeo yake mnaharibu mapafu yenu, afu mnakuja kutuambia kafa kwa corona!!pymbavu.
Sisi tunaona game lote kwenye Tv kama movie za holywood tu.
Ndo maana serikali itapata tabu sana kwa vile hakuna anayeunga mkono, sio wanajeshi wetu wala polisi. Juzi nilikuwa polisi hakuna hata anayejali, mwendo mdundo.
Wewe kama unaogopa vaa barakoa usitushawishi sisi.
Hata hizo dozi za chanjo zitaisha kwa tabu sana, hizo hizo 1.2Mln.
 
Kwenye msafara wa mamba, hata kenge wamo.
 
Back
Top Bottom