..hakuna anayepinga Tz kuunganisha nguvu na kuwa na mahusiano ya kiuchumi na nchi majirani na za Afrika kwa ujumla.
..particularly naunga mkono Ethiopian Airline kufungua HUB hapa Dsm.
..tena ningependa waweke hub (abiria na mizigo) nyingine kanda ya kaskazini ili kusaidia sekta ya utalii na sekta ya kilimo cha maua.
..zaidi naunga mkono mashirikiano ktk sekta ya nishati. Mpango wa kuwa na grid ya pamoja kuanzia Ethiopia, Kenya, Tz ni mzuri.
..nisichokubaliana nacho ni madai yaliyotolewa kuwa mizigo ya Ethiopia itakuwa ikiletwa bandarini Dsm na baadaye kupakiwa ktk ndege kwenda Addis Ababa.
..lingine nisilokubaliana nalo ni hoja ya kufundishwa na Waethiopia jinsi ya kuzalisha umeme wa maji. Naamini utaalamu huo waTz tunao. Tumekuwa na miradi ya Kidatu, Mtera, Pangani, ..miongo kadhaa kabla Ethiopia hawaanza mradi.
..lakini vilevile kwa mazingira yetu, umeme wa maji siyo wa uhakika. Tulishaamua kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme wa gesi.
..Idea ya kushirikiana na Ethiopia ni nzuri. Tatizo nimeliona ktk hoja za JPM ambaye alijikita zaidi kuomba-omba hata mambo ambayo yako ndani ya uwezo wetu.
..
Mkuu hapo kwenye Hub naomba unieleweshe kidogo. Ina maana watakuwa na hub ya ndege zao kuanzia DSM kwenda mataifa mengine bila kupitia Adis?
Au ina maana itakuwa hub ya kuunganisha mataifa mengine kabla ya kupitia Adis Ababa?
Ninavyoelewa kila shirika la ndege huweka hub katika nchi husika kwasababu za kiuchumi
Kwa upande wa Ethiopian airline, nini hasa kinalengwa? Na je wapo tayari na kwa faida zipi?
Kuhusu umeme, katika mambo yalinisikitisha sana hili ni mojawapo.
Nyerere alijenga mabwawa yote licha ya uchanga wa Taifa na matatizo mengine.
Mradi uliobaki ulikuwa wa Stiegler ambao ungekuwa mkubwa sana.
Serikali ya JK ilianzisha mchakato tukaambiwa umeme utakuwepo hadi kuuza Zambia na Kenya. Ghafala tukasikia gesi itaondoa tatizo na kuwa na ziada. Sasa tunasikia kuagizwa umeme
Kuunganishwa ni grid ya Afrika mashariki ni jambo jema, hata hivyo si jambo la kujivunia.
Tulitakiwa tunufaike na grid tukiangalia majirani zetu wa Rwanda, Burundi na Malawi
Majirani hawana source nzuri za umeme , ilikuwa fursa kwetu na si shangwe za kuagiza
Tunaposimama na kujivuna umeme wa bei rahisi ni kurahisha uwezo wetu wa kufikiri
Iweje Ethiopia watumie umeme wa maji kutuuzia wakwetu uwe ghali kiasi cha kuwasifia!!
Tume 'explore' sehemu zote hadi kudhani kuagiza umeme ni jambo la busara?
Tulijenga vipi Nyumbani ya mungu, Pangani falls, Mtera, Kidatu na sasa tudhani hatuna 'option'?
Kutumia umeme rahisi wa Ethiopia ni jambo la kushangaza.
Ukifika hapa nchini utakuwa rahisi kuliko wa Tanesco.
Tunajua kuna malipo ya infrastructure, lakini bado utakuwa rahisi. Something is wrong!