Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Kuna hidden agenda mbona mwenye St.Maria hajatajwa??
Mkuu kuna watu wanazungumza kiushabiki humu bila kujua madhara yake. Mbowe kwa siku nyingi anajijua kuwa anawindwa kisiasa, hivi ni wazimu gani waweza kumfanya akaingia kwenye biashara hatari huku akijua ana windwa kila mahala?
Ninachofikiri ni lengo la kumdhalilisha kisha awe muoga na kurudi nyuma. Hakika njama hizo haziwezi kamwe kushinda.
Yule ni KUB na kama alikuwa ana jambo la kuhojiwa sio stahili kwa Makonda kutamka eti aje ijumaa ahojiwe, wangeweza mfata Dodoma na kumhoji au IGP kumtumia wito. Kwani mtu akisema Majaliwa PM anahusika Makonda angeweza kutamka pale kuwa aje Ijumaa central?
Kibunge KUB na PM wana hadhi zinazoendana labda sie hatutaki kukubali tuu.
 
Lakini pia ulimsikia alipo sema wanataarifa
Wao siyo wajinga.
Tatizo watu wanaingiza siasa na umimi ndani ya mapambano
Ubaguzi wa nani atajwe nani asitajwe!!
Akiwa mpinzani marufuku kutajwa!!
Haiwezekani


wasiishie kutajwa funga kabisa nimeharibiwa mdogo wangu alikuwa na akili sana darasani akageuka kuwa teja mara ya mwisho alipona kuuliwa kwa kuchomwa moto alichukua blanket nyumbani akauze apate unga watu wakafikir kaiba kwa majirani alipigwa sana na aliamwagiwa mafuta mwenyekiti wa kijiji aliokoa maisha ya mdogo wangu kwa kuwatuliza raia baadae ukweli ukaja kujulikana alichukua nyumbani lakini baada ya kupona kuchomwa roho inaniuma sna tumempeleka soba kila mwisho wa mwez tunalipa laki mbili na nusu madawa hatar sana napenda ushahidi uwepo wenye nguvu


bado namuunga mkono makonda hapa hamna siasa kama azan na husein wametajwa sana manji kaongelewa sana kupitia yanga hakuna jipya ambalo wanasingiziwa hapo.

kila nikimuangalia mdogo wangu naumia sana kifo cha moto noma sana alichopona nacho kijana mdogo sna miaka 25
 
nilijiuliza hili swali tokea mwanzo na nitaendelea kujiuliza mpaka pale nitakapopata majibu halisi. sidhani kama kuna mwenye dhamira ya kweli ya kupambana na uuzaji na utumiaji Wa dawa za kulevya Bali naona mwisho Wa hili tunaweza kushuhudia viongozi wengi Wa upinzani wakiishia Kuleeeeeeeeeee! huenda hii ni mbinu Moja wapo waliyoamua kuja Nayo. Muda utasema
Mimi najuwa Manji ni Diwani wa CCM na Idd Azan ni CCM, hebu tuelezee vizuri mleta maada.
 
Wamemtafuta mbowe kila kona sasa wameamua kumbambikizia kesi za madawa ya kulevya ili kuua upinzani,makonda anatumiwa.
Ndiye anayetafutwa utaona kama watamuachia.
 
Vitu alivyoongea msukuma vingekuwa vya uongo Makonda angekana balaa lakin ni vya ukweli kapiga kimyaa
 
Rais wa JMT ni wakati sasa wa kumpa wizara ya mambo ya ndani huyu makonda. Ni mtu anayethubutu. Siyo pambo wa sasa
 
Wakuu Mimi kuanzia Leo siyo mwanachadema tena ni aibu kubwa sana mwenyekiti wetu kuwa na tuhuma kama hizi hata kama siyo kweli ni tuhuma kubwa kwake.

Nilivumilia ile ya kunywa Viroba Kwa sababu ni tabia binafsi ya mtu ila kwa hili la Kuuza dawa za kulevya limenichosha

Baada ya jina lake kutajwa nimedondosha simu yangu na kuvuja kioo kwa kweli imeniuma sana.
 
sasa watu wameamua kuja kwa ID tofauti manake siku ya kwanza walitumia ID zao feki kutetea 'sembe' leo wameumbuka. Mleta mada Manji ni Chadema?
 
Gud job.... bt publicity na sifa zitamwangusha.... mission itakua impossible....

Hizi media na siasa zinaua saaana uhalisia wa mambo.

Zinabadili mambo mingi saanah aiseee....

https://jamii.app/JFUserGuide media.
 
Hawa jamaa Tundu Lisu na Mbowe nilijua tu ni lazima wanauza na wanatumia Sembe!
Halafu walitaka tuwakabidhi nchi hawa wauwaji wa Vijana wetu? Yaani Mbowe na Tundu Lisu ndiyo wangekuwa Ikulu sasa hivi, hii Nchi kweli Mungu anatupenda!
.....
.....crechepolitical hahahaha
 
Msukuma anajipalia kaa la moto, kama hatokuwa ahusiki na yeye kwenye biashara basi, atakuwa anatumiwa kulizima ilo sakata la madawa ya kulevya na mapapa, ndo maana anakuja na hoja za makonda za kwenda US, UK na dubai ambazo kimsingi ni trike ambayo ishazoeleka kwa watanzania jinsi ya kuzima hot move nchini, refeer babu wa loliondo
 
Na rizi moja mbona hayupo coz nayeye si anahisiwa kama hao akina idd azan!!???
 
Back
Top Bottom