Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Lazima umpa
Hii sio vita ya madawa ni vita ya siasa!! Unless hatujui vita ya madawa ikoje!! Huwezi mshika mlevi au mtumiaji ukasema unapambana na madawa!!!

BTW yale majina ya jk mbona hayatajwi???
Lazima umpate mtumiaji ili akupeleke anapopatia hiyo huduma.
Mbona vituvingine viko wazi mkuu.
 
Hii vita inahitaji approach mpya ,matatizo ya madawa ya kulevya yapo kabla Makonda hajawa RC lakini hizo agency hazijawahi kufanya lolote na polisi wanaifahamu hii biashara vizuri na ni washiriki wakubwa kwenye hii biashara ndio maana umeona ile list waliokamatwa kuna polisi wengi.Hii vita inakuwa one man show sababu wafanyabiashara na vigogo wa idara za serikali ni wadau wa hii biashara.Hata Duterte anafanya one man show na amepata upinzani mkubwa sana lakini ameendelea kuwaua na wengi wamekimbia na hata wale waliokuwa wanataka kuingia kwenye biashara wanajua mambo yamebadilika. Vile vile madawa ya kulevya yanaingilia na kutokea DSM na pia ndio kuna watumiaji wakubwa

Makonda anapata upinzani kwa mambo mengine aliyofanya huko nyuma lakini kwa hili yuko sawa,kelele zake zinasababisha matatizo mengi yanazidi kujulikana
Mkuu ameniacha hoi kutaja majina watu wengine huku wengine akitaja kampuni wanazomiliki huu ni upuuzi mwingine,anataka kuniambia wamilik wa Yatch club,Palm beach,sea cliff hawana majina?This is rediculous
 
Kuna baadhi vyama mpaka leo havieleweki vinasimamia maslahi ya nani, kuna wawakilishi wao walikuwa wanapiga sana kelele juu ya madawa ya kulevya leo mtu anasimamia wao wanakuja juu kutetea hao wahusika kila siku mapovu yanawatoka juu ya mapapa wa madawa hamjui kuwa viongozi wenu pia ni wahusika wakuu wa madawa nani asiye urafiki wa Lowassa na Rostam, rostam na familia yake ni mmoja wa wahusika wakuu.
Je nani hajui kuhusu GWAJIMA ambaye ndiye alkua mlez wa CHADEMA nani hajui juu ya haya.

Naona humu tunashabikia tunapiga kelele juu ya kitu ambacho hatukijui, msifuate upepo nyie bendera.
Kwahiyo mkuu Lowasa nae papa au!!
 
Ukiamini Freeman Mbowe anauza madawa basi hata ukiambiwa your mother is a prostitute Mara moja utakubali na kutangaza kuwa huo ni ukweli


Jinsi pale Bilicanas palivyokuwa, ikiwa anaweza kuuza pombe na kufungua sehemu ya kuuzia na kuharibu jamii, mpaka underage walikuwa wanauzwa pale, unga utamshinda nini kuuza?

Tena huyo ndiyo suspect namba moja.
 
Bavicha leo hawaamini kilichotokea, walikuwa wanamshinikiza Makonda aachane na vidagaa ataje mapapa, kilichowakuta hawana hamu
Nyie ndo mmeingia kingi sio hao bavicha. Mlishabikia jina mboww kumbe sie huyo mnaemjua
 
Muilizeni kama ameandaa fidia kuwalipa iwapo hawatopatikana na ushahidi, hii kesi tamu sana asidhanie kuwataja kina mbowe au manji watamvumilia kuwaharibia jina

Hamna kumuharibia jina mtu. Mambo yashafanyiwa uchunguzi bwana.
 
Hawa walio tajwa wanatakiwa wamfikishe jamaa mahakamani wadai kulipwa fidia ya kuchafuliwa majina. Huyu mpayukaji anatakiwa kufundishwa adabu sasa
sasa mbona kama umeshahukumu kuwa hawana hatia, wameitwa kwa mahojiano na ikiwezekana kuchangia kupata taarifa zaidi dhidi ya hao wauza/wasambazaji wa unga! kwani we hutaki wachangie katika mapambano?
 
Nataka kijua Huyo Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema,maana tusijekuwa tunadhani ndio yeye kumbe ni mwingine
Huyo ni Philemon Mbowe mfanyabiashara wa madawa ya kulevya.
 
Halafu unawapa taarifa Kwenye tv hata Mimi nitasafusha mzigo du jamani hii movie tamu
Wanakua chini ya uangalizi. Wakigusa tu mzigo wanadakwa red handed. Kutajwa hadharani imewakata ngebe. Sasa wanafatiliwa hadi simu zao so any stupid move wanaingia kingi
 
tunapinga madawa ya kulevya na kumuunga mkono makonda ila pakitokea ushahid umekosekana mahakamani pasijechukuliwa mapato yaliyofichwa kwa miaka miwili kwa kuchafuliwa watu wakadai fidia kutaja na kusibitisha vitu viwili tofauti wanajamvi.
 
Kwa nini asiwe TBC wanaondeshwa kwa kodi zetu?Nani anagharamia matangazo hayo pale mawingu?Jee ni walipa kodi wa jiji la Dar?au ni yeye mwenyewe ?ama anafadhiliwa kama alivohoji Musukuma kule bungeni??!


makonda alichofanya ni kuita waandishi wa habari wote kwa ujumla na sio clouds pekee

clouds wo wako kibiashara wanajua lazima watu wengi wataangalia ndio maana wakarusha mubashara
vituo vingine havikukatazwa kurusha mubashara n kila kituo na uwezo wake

mbona azam hauhoji na wao kurusha mubashara

msifikirie kuponda mda wote
 
Vita ya madawa ya kulevya iendeshwe hadharani hivi!! This must be a joke. Hii siasa tu. Huku ni kuchafuana mwisho wa siku mnaambiwa hmna hatia wakati mmeshautangazia ulimwengu mzima. Kwa mtindo huu wadanganyika wenye upeo finyu wanahadaiwa ili waanze kushangilia na kusifu. Hahahaaa hii ni kama mahakama ya mafisadi isiyo na washtakiwa. Wamepotea ghafla hakuna wa kumshitaki. It was plitics from the beginning

Naamini wewe BabM, pia una nia nzuri ya kupambana kwenye vita ya madawa ya kulevya. Kama niko sahihi, basi rekebisha mtazamo wako kuhusu njia sahihi ya kupigana vita hii.

Hakika, kukaa kimya kunaweza kuzaa matunda mazuri, lakini kuna ushahidi kwamba vita hii imekuwa ikiendeshwa kimyakimya, matokeo yake ni lawama kwa waliopewa dhamana ya kusimamia vita hii. Ati ni dagaa tu wanakamatwa!

Hivyo, ni sahihi wanaotuhumiwa kutajwa hadharani ili wananchi tuwajue na majina ambayo hayakutajwa yatajwe na wenye kuwafahamu uhusika wao.

BabM: kama una husika, au wamjua mhusika, salimisha taarifa. Ukitaja/ukitajwa, kwa vita ya madawa ya kulevya, utakuwa umejipunguzia 'pressure' ukawa na amani moyoni.
 
Tanzania hakuna kitu jina halisi, ukianza kutafuta Majina halisi utakesha hautampata mtu, utakuta mtu nyumbani anaitwa Moshi, Shuleni anaitwa John, kazini Mushi, basi mkanganyiko tu,
ila Mbowe ni Mbowe-chadema!
Umeanza kutafuta pa kutokea. Ndo maana huko kwenu kuna Lameck Madelu na mnamkubali hadi kumpa majukumu makuu taifani
 
Back
Top Bottom