Mabere Marando sasa hivi ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kama sikosei. Katulizwa huko! In fact NCCR Mageuzi chini ya Mrema iliyumba sana kutokana na Mrema kuwa mropokaji majukwaani mara kwa mara na kina Marando na Lamwai kujikuta kila siku wako Mahakamani kumtetea mwenyekiti wao badala ya kufanya kazi zao za Kibunge na Kichama!
Pia inasemekana ni mbinu za CCM zilizotumika kukisambaratisha Chama, kumweka Lamwai benchi bila kazi yoyote na kisha kumrudisha CCM na kumpa kazi. Tangu hapo wote wakawa kimya kabisa!
Pia CCM mwaka 2005 waliweka nguvu nyingi sana kwenye majimbo yote ya uchaguzi ambayo wabunge wake walikuwa wa vyama vya Upinzani. Kwa mfano kwenye jimbo la Benedicto Mutungirehi ambaye alikuwa machachari bungeni kuliko Zitto Kabwe. Lakini la kuvunda halina ubani, wakamwekea nguvu nyingi Mutungirehi, akaibuka Zitto Kabwe!
Sijui kwa sasa Mutungirehi anafanya nini, lakini nina imani 2010 atagombea tena ubunge! Akirudi bungeni na kuongeza nguvu kwa kina Zitto na Slaa, na tukaapata wabunge wengine kama watano tu walio machachari, nchi itakwenda na bunge litakaa sawa!
Hawa kina Mramba, Yona, Patel, Mgonja na wenzao mnaowaona wana kesi mahakamani ni juhudi za wabunge wachache (na za JF pia), matunda yanaonekana na wanatakiwa kupewa moyona kuongezewa nguvu zaidi!